Naombeni msaada wenu

Pole sana mkuu.. Jitahidi ukatembelee makaburi japo uone walipopumzishwa wapendwa wetu
 
sawa nitafanya hivo
Usiwaze sana kuhusu ndugu zako afu usijipe sana umuhimu kwao wakati hawaona umuhimu wako, focus na maisha yako jitahidi kufanya kazi kwa bidii pambania maisha yako acha kuwaza watu wasio kuwa na muda na wewe, Undugu kufaana sio kufanana. Ukienda kwenye kaburi la babu na bibi yako nenda kazike maumivu yako yote sijui mama au mdogo wako, ukirudi rudi na swala moja tuu kujiwazia wewe na mtoto usikubali kuishi tena na maumivu yakatae kwa jina la Yesu.
 
nimekuelewa sana. asante
 
Tatizo naloona hapa dadaangu Dadakidoti ni upweke wa kukosa mtu wa kukujali, wa kukuskiliza sauti yako ya ndani, wa kukupa faraja mpaka uyasahau uliyopitia. Vilevile hisia mbaya za huzuni huzuni iliyokomaa ikawa sononeko, angepatikanam mtu huyo hakika pengo lililoachwa na bibi,babu pamoja na mama asiekupenda litazibwa.

Kiukweli pekeako itakuwa ngumu kuyashinda unahitaji msaidizi hapa duniani, habari njema ni kwamba msaidizi alieko mbinguni MUNGU anakujali mwamini hajakuacha atakukumbuka very soon na utapona.

-Inasikitisha sana kwa uliyopitia tokea upo mdogo POLE SANA dadaangu, utaimarika zaidi, majaribu humpata kila mwanadamu hauko pekeako, tuko nawe tunakuombea utashinda, utayaweza, utapona, kwa jina la BWANA na MWOKOZI WETU YESU KRISTO, AMEN!
 
amen
 
Pole sana. Nenda katembelee makaburi yao haraka na roho yako itapona na furaha kurejea. Mungu akusaidie.
 
Pole sn. Kuwa na subra. Muombe Mungu. Jikaze sn kwa ajili ya mtt. Hio hali itapungua taratibu mwisho itaondoka kabisa. Ni suala la muda tu
 
Basi jitahidi uende kule na huko makaburini utasema shida zako zote,ila nadhani kuna namna umeathirika kisaikolojia.
Kama mtandao huu ungekuwa unaaminika bila shaka ungepata watu wanaoishi huko ulipo wakakusogeza sogeza maana inaonekana shida sio kubwa kiivo ila umejikatia tamaa tu
 
Pole nakushauri pata rafiki,rafiki ambae ataweza kuwasiliana na wewe muda wowote,atakutoa kwa mawazo na ukajiona uko wa thamani

You need some body…
Wewe unataka kumuongezea binti matatizo, hakuna mtu anaiona thamani yako zaidi yako, furaha ipo ndani yako sio mpaka utafute rafiki huyo rafiki yeye hana ishu za kufanya hadi awe anakuangalia wewe na yeye anaangaliwa na nani??
 
sawa shukrani sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…