Naombeni msaada wenu

Naombeni msaada wenu

Dadakidoti

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2024
Posts
399
Reaction score
1,409
Bila shaka wote mko poa kabisa.
Kidoti wenu nimerudi maji ya shingo nashindwa hata pa kuanzia. Kama familia yangu ya JF naombeni ushauri wenu wenda nikapata hata msaada.

Kama mnakumbuka nilileta uzi huu Kuna wengine hatujui tulipokosea
Sikuweza kuandika kila kitu. wengi mlisoma historia yangu na mnajua wapi nimepitia mpaka nilipo.
niwawachoshe moja kwa moja kwenye mada.

Katika maisha yangu watu ambao ndo walikuwa familia yangu ni babu na bibi zangu sababu wao ndio walikuwa wanasimama kama wazazi ninapopitia changamoto. Hasa hasa babu mzaa baba na bibi mzaa mama. kwa ufupi mwaka jana mwezi wa tatu mwishoni babu yangu alikufa. Kipindi msiba unatokea nilikuwa na wakati mgumu sana sababu sikuwa na kazi ya kueleweka na nilikuwa na mtoto mdogo. Hivyo sikuweza kwenda kanda ya ziwa msibani. wakati huo huo bibi yangu mzaa mama alikuwa Arusha kwa ajili ya matibabu alikuwa anaumwa baada ya kupata taarifa alinipigia simu kunipa pole na kunitia moyo sababu alijua jinsi nilivyokuwa nampenda babu yangu. akanisisitiza nimwangalie mtoto alijua nilivyokuwa nimeumia kutoweza kwenda kumzika babu yangu. alikuwa anasisitiza nisiangalie kitu kingine zaidi ya kumwangalia mtoto. nilitaka kuuza kibanda changu ili nipate nauli lakini bibi alikataa akaniahidi kuwa akirudi nyumbani atanitumia nauli nitaenda kuzuru kaburi.nikaona ni sawa nikamkubalia.

Ilikuwa ni ijumaa bibi alinipigia simu tliongea sana karibia masaa mawili. akinisisitiza akili yangu yote iwe kwa mtoto. Kesho yake ajabu napigiwa simu kuwa bibi yangu nae hayupo tena duniani ndani ya wiki mbili tu nilipoteza watu muhimu sana kwangu. walisafirisha mwili pia sikuweza hata kwenda kuzika. hakuna kipindi kigumu niliwahi kupitia kama kipindi hicho. sina kazi ya kueleweka nilikuwa nafanya kazi kwa mama ntilie nalipwa elfu tano angalau nipate kula na mtoto. Mama angu alikuja kumzika bibi lakini hakunipigia hata simu kujua angalau mimi na mtoto tunaendeleaje. kwa ufupi bibi ndo alikuwa kama mama yangu.

Mungu ni mwema nilifanikiwa kupata kazi ambayo naendelea nayo mpaka sasa namshukuru Mungu nipo vizuri japo si sana nina dhiki za kawaida kama za watu wengine. hatulali njaa na mtoto naweza kulipa ada kodi na kujikimu mahitaji yangu na mtoto. naweza kula nachokitamani. namshukuru sana Mungu kwa hilo.
ila kinachoniumiza toka itokee hiyo misiba sina amani nikiwakumbuka babu na bibi yangu naanza kulia. usiku silali nimekonda nimepungu kutoka 63kg mpaka 55kg.

usiku nikilala naweza kuota nipo kanda ya ziwa yaani naota makaburi naweza ota nimeenda kwa bibi lakini nyumba imejengwa makaburini. naweza kuota nipo mochwari yaani kwa ujumla sioti ndoto za kawaida. najikuta wakati mwingine natamani kufa labda naweza kupumzika lakini akili inaniambia ukifa huwezi kupumzika kwa amani kwa sababu mtoto wako hutakuwa umemuacha katika mazingira magumu sana. nimedhoofika sana kichwa kinaniuma kila siku nameza pain killer lakini kuna muda zinadunda.
samahani naombeni msaada wenu nipo njia panda.
 
Nilikuaga mbishi sana ila nilikuja kuelewa taratibu with evidence

Mkuu kiroho ukisha ota umerudi kwenu mara shuleni, basi ni direction ya nyayo zako kushikiliwa, kupelekea kutokupiga hatua maishani mwako.

Unakuw mtu wa manung'uniko sana

Mostly hali hio ni kutokana na mizimu ya ukoo , jina uliloitwa unaliishi kwa consquences zinaandama jina unaloenzi.

au laana ya kuletewa kutokana na husda.

So ushauri ni kuwa tafuta msaada wa kiroho zaidi ujiondee katika kifungo.
 
nimeenda mpaka kwa Mwamposa, nimebatizwa mpaka ubatizo wa maji mengi lakini bado.
 
Mkuu mwammposa sio Mungu. Uendedashaji wa ibada ya Mwamposa ni kwa ajili ya waliokubali kutapeliwa

Ingia pm nimekutumia namba ya padre mmoja aliepoa zanzibar.

Mpigie mida ya saa tatu na nusu usiku ndio muda wake

Ujitambulishe kwa heshima na uwe precise

Wala hataki hela yako ila ushirikiano wako ndio utampa nguvu ya kukuongoza sala na mombi maaalum.

Hakika utafunguliwa.
 
Bila shaka wote mko poa kabisa.
Kidoti wenu nimerudi maji ya shingo nashindwa hata pa kuanzia. Kama familia yangu ya JF naombeni ushauri wenu wenda nikapata hata msaada.

Kama mnakumbuka nilileta uzi huu Kuna wengine hatujui tulipokosea
Sikuweza kuandika kila kitu. wengi mlisoma historia yangu na mnajua wapi nimepitia mpaka nilipo.
niwawachoshe moja kwa moja kwenye mada.

Katika maisha yangu watu ambao ndo walikuwa familia yangu ni babu na bibi zangu sababu wao ndio walikuwa wanasimama kama wazazi ninapopitia changamoto. Hasa hasa babu mzaa baba na bibi mzaa mama. kwa ufupi mwaka jana mwezi wa tatu mwishoni babu yangu alikufa. Kipindi msiba unatokea nilikuwa na wakati mgumu sana sababu sikuwa na kazi ya kueleweka na nilikuwa na mtoto mdogo. Hivyo sikuweza kwenda kanda ya ziwa msibani. wakati huo huo bibi yangu mzaa mama alikuwa Arusha kwa ajili ya matibabu alikuwa anaumwa baada ya kupata taarifa alinipigia simu kunipa pole na kunitia moyo sababu alijua jinsi nilivyokuwa nampenda babu yangu. akanisisitiza nimwangalie mtoto alijua nilivyokuwa nimeumia kutoweza kwenda kumzika babu yangu. alikuwa anasisitiza nisiangalie kitu kingine zaidi ya kumwangalia mtoto. nilitaka kuuza kibanda changu ili nipate nauli lakini bibi alikataa akaniahidi kuwa akirudi nyumbani atanitumia nauli nitaenda kuzuru kaburi.nikaona ni sawa nikamkubalia.

Ilikuwa ni ijumaa bibi alinipigia simu tliongea sana karibia masaa mawili. akinisisitiza akili yangu yote iwe kwa mtoto. Kesho yake ajabu napigiwa simu kuwa bibi yangu nae hayupo tena duniani ndani ya wiki mbili tu nilipoteza watu muhimu sana kwangu. walisafirisha mwili pia sikuweza hata kwenda kuzika. hakuna kipindi kigumu niliwahi kupitia kama kipindi hicho. sina kazi ya kueleweka nilikuwa nafanya kazi kwa mama ntilie nalipwa elfu tano angalau nipate kula na mtoto. Mama angu alikuja kumzika bibi lakini hakunipigia hata simu kujua angalau mimi na mtoto tunaendeleaje. kwa ufupi bibi ndo alikuwa kama mama yangu.

Mungu ni mwema nilifanikiwa kupata kazi ambayo naendelea nayo mpaka sasa namshukuru Mungu nipo vizuri japo si sana nina dhiki za kawaida kama za watu wengine. hatulali njaa na mtoto naweza kulipa ada kodi na kujikimu mahitaji yangu na mtoto. naweza kula nachokitamani. namshukuru sana Mungu kwa hilo.
ila kinachoniumiza toka itokee hiyo misiba sina amani nikiwakumbuka babu na bibi yangu naanza kulia. usiku silali nimekonda nimepungu kutoka 63kg mpaka 55kg.

usiku nikilala naweza kuota nipo kanda ya ziwa yaani naota makaburi naweza ota nimeenda kwa bibi lakini nyumba imejengwa makaburini. naweza kuota nipo mochwari yaani kwa ujumla sioti ndoto za kawaida. najikuta wakati mwingine natamani kufa labda naweza kupumzika lakini akili inaniambia ukifa huwezi kupumzika kwa amani kwa sababu mtoto wako hutakuwa umemuacha katika mazingira magumu sana. nimedhoofika sana kichwa kinaniuma kila siku nameza pain killer lakini kuna muda zinadunda.
samahani naombeni msaada wenu nipo njia panda.
Muombe sana Mungu yupo na anakuona!Kuwa jasiri na utayashinda haya Hakika!
 
Pole sana Kwa hayo unayopitia.

Jambo la kumpoteza mtu wa karibu, unaweza kuomboleza Msiba wake Kwa muda mrefu kidogo, kumbukumbu zake sio rahisi kupotea.

Unachotakiwa kufanya ni kujitahidi uende ukazuru makaburi ya wapendwa wako.

Ukifika, waone watu wazima waeleze umekwenda kuzuru makaburi ya hao wapendwa wako

Kuna mambo ya kimila utafanyiwa, nawe utaacha kuota ndoto za namna hiyo.
 
Mkuu mwammposa sio Mungu. Mwamposa ni tapeli wz kiroho

Ingia pm nimekutumia namba ya padre mmoja aliepoa zanzibar.

Mpigie mida ya saa tatu na nusu usiku ndio muda wake

Ujitambulishe kwa heshima na uwe precise

Wala hataki hela yako ila ushirikiano wako ndio utampa nguvu ya kukuongoza sala na mombi maaalum.

Hakika utafunguliwa.
Mkuu kwa Padre tena, mbona wakatoliki wanatoka kwa hao Mapadre na wanakuja kwa mwamposa.
 
Kuna kitu bado hujakisema ambacho ndicho kiini cha changamoto unazopitia. Pata mtu sahihi wa kumueleza kila kitu kuhusu wewe na njia ulizopita mpaka kufikia hapo. Utasaidika vizuri sana na huo mzigo mabegani mwako utautua, utajiskia amani sana. Imani hufanya kazi na Ukweli na uwazi.
 
Back
Top Bottom