econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Hivi majuzi nimeota ndoto ambayo bado inanisumbua sana.
Hii ndoto ilikuwa inamhusu mwendazake Rais Magufuri. Niliota ilikuwa siku ya uzinduzi wa reli ya Chini kwa Chini au unaweza kuziita treni za kutumia umeme. Hivyo na Mimi nikaenda kwenye ufunguzi wa reli hiyo pamoja na wananchi wengi. Kama kawaida Rais alikuwa mbele tayari kwa kuzindua reli.
Cha kushangaza Rais alipoaangalia upande wa wananchi akaniona akaniita na kuniomba tuzindue pamoja naye ile reli. Nilijisikia hali ya Furaha na upendo kwa Rais pamoja kwamba nilikuwa simkubali kwa jinsi alivyokuwa anatupelekesha CHADEMA. Baadae akawa ananiuliza maswali na tunaongea wakati tunasubiri uzinduzi. Ghafla ndoto ikakatika nikashtuka usingizini.
Mpaka sasa sijafahamu maana ya ndoto hii, naombeni msaada. Naombeni ufafanuzi. Inakuwaje mtu niliyekuwa nina mchukia sana kwenye reality aniite kwa upendo kwenye ndoto halafu na mimi nimkubalie na kufuraia wakati in real life nisingeenda kwenye Jambo lake.