Naombeni taratibu za rufaa Wizara ya Elimu, mwanangu kapata division three wakati hana uwezo huo

Unachotaka kusema ni nini sasa!
 
Tunaandaa bomu la nuclear. Watoto hawajui chochote ila wana ma "A" "A" kwenye vyeti vyao. Hawajui kuongea, kusoma wala kuandika lugha yoyote, hawawezi kazi yoyote..... halafu eti ufaulu umeongezeka.
 
Dah mwanangu 2009 watu walifeli sana chunguza
 
Nimetoka kuongea na dada yangu kuna mtoto wa Kaka yetu ni mzito tena mzito hasa kiufupi tulikuwa tunasubiri amalize aolewe cha ajabu amepata division III kwa kweli familia nzima tumeshangaa.
Something is not right,hata majuzi kati nilikuwa namfanyia dogo application ya chuo kikuu nikashangaa Shule ya Serikali ina karibu division I 200 na usher nilijiuliza maswali mengi sana.
 
Kama waziri anabisha wazazi tuko tayali kuwaleta watoto mbele wahakikiwe! Siyo kwa ubaya lakini hata kama tunabebana siyo kwa style hii ni kuuwa taaluma makusudi au kwa bahati mbaya
 
Nimeshapeleka barua ya kupinga matokeo DoM nasubili majibu
 
Unaonekana ni mzazi ambae hauko serious na wanao,itakuwaje umwache huru kiiivyo,,kidaftari kimoja unamwangalia tu,hauko makini au huyo ni mtoto wa jirani yako kama si nduguyo.
 
Unaonekana ni mzazi ambae hauko serious na wanao,itakuwaje umwache huru kiiivyo,,kidaftari kimoja unamwangalia tu,hauko makini au huyo ni mtoto wa jirani yako kama si nduguyo.
Wewe ambae uko serious subili utakapozalishwa tutajua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…