Naombeni ufafanuzi wa faida na hasara za operesheni vijiji 1974

Naombeni ufafanuzi wa faida na hasara za operesheni vijiji 1974

Kabla ya kutaja faida na hasara ni vema ukapata picha kuwa enzi hizo mtu au familia au ukoo fulani ulikaa maeneo lilipo chimbuko la ukoo na mara nyingi ilikuwa ni ardhi yenye rutuba kando kando ya mito au eneo lenye uwanda mzuri wenye vijito na mifereji ya maji.
Mkusanyiko mkubwa wa watu ulipatikana kwenye ngazi ya tarafa ambako ndio kulikuwa na huduma za maduka hospitali na vituo vya polisi vilivyowajibika kwenye ngazi ya wilaya.
Huko kwenye ngazi ya tarafa ndiko watu walikuwa wakimiliki ardhi zao za asili na walijishughulisha na kilimo na ufugaji. Familia iliyofanikiwa zaidi wakati huo ilihusishwa na kusoma sana na kuajiriwa Serikalini au kufanya kazi kwenye mashirika ya dini.

Uanzishwaji wa vijiji uliirahisishia Serikali kupeleka huduma za msingi kwenye kijiji kilichoanzishwa na hivyo kuepuka gharama ya kumhudumia mtu au kaya moja moja kule aliko peke yake. Nimeshuhudia baadhi ya vijiji vilivyoanzishwa wakati huo, vikiwa vimefikia hadhi ya kuitwa mji... Mfano Nyakanazi
Hasara zilizojitokeza ni kupoteza umilili wa ardhi ya asili ambayo ilikuja kuwa mali ya Serikali kitu ambacho ni dhuruma ya wazi kufanyiwa mwananchi.
 
Kuna mashoga wa Dar walishikwa na kupelekwa geza ulole, baada ya miezi miwili mmoja, alikuwa maarufu sana Dar. akatoroka huko akawa anaonekana £Dar., anasema "heri ya jela kuliko huko, njaa tupu, mpaka mwanamme hakuna tena, ukiona ukuni umesimama ujuwe nyoka huyo, yamenishinda".
Habari dada yangu kipenzi
Kumbe upo

Ova
 
By force by power by 🔥 🔥 🔥
Inatoka order mnapewa mda , usipohama watu watakuja kukubeba wewe , mke na watoto tu.
Ni heri ukubali kuhama mapema unaweza kupewa msaada wa kubebewa vimbuzi vyako
 
Nasikia tu katika historia Mzee Nyerere alianzisha operesheni maalumu ya vijiji vya ujamaa..

Hali ilikuaje ilikuwa ni kwa force au kuhama kwa hiari.
Mwitikio ilikuaje je Kuna watu walipata madhara ya kisaikolojia na mali zao.je hilo zoezi lilifanikiwa na faida zake zipi?
Nyerere alianzisha miji midogo sio vijiji
Watu walihamishwa vijijini kwenye mashamba yao wakaenda kurundikwa kwenye ka mji watakapopewa maji shule na hospitali
Nyerete ndie aliua kilimo Tanzania kwa kuanzisha hivyo vi miji vyake

Toka hapo kilimo kikaanguka chali
 
Nasikia tu katika historia Mzee Nyerere alianzisha operesheni maalumu ya vijiji vya ujamaa.. Hali ilikuaje ilikuwa ni kwa force au kuhama kwa hiari. Mwitikio ilikuaje je Kuna watu walipata madhara ya kisaikolojia na mali zao.je hilo zoezi lilifanikiwa na faida zake zipi?
Nasikia tu katika historia Mzee Nyerere alianzisha operesheni maalumu ya vijiji vya ujamaa..

Hali ilikuaje ilikuwa ni kwa force au kuhama kwa hiari.
Mwitikio ilikuaje je Kuna watu walipata madhara ya kisaikolojia na mali zao.je hilo zoezi lilifanikiwa na faida zake zipi?
Binafsi naona faida kuliko hasara

Mimi wakati Naanza primary in 1979 nilikuta wazee wangu wakiwa happy na ule mfumo kwani huduma were concentrated to the designated areas
 
Kuna mashoga wa Dar walishikwa na kupelekwa geza ulole, baada ya miezi miwili mmoja, alikuwa maarufu sana Dar. akatoroka huko akawa anaonekana £Dar., anasema "heri ya jela kuliko huko, njaa tupu, mpaka mwanamme hakuna tena, ukiona ukuni umesimama ujuwe nyoka huyo, yamenishinda".
He!... Makubwa haya... Ukuni tena umesimama utadhani nyoka? 😲
 
Kuna mashoga wa Dar walishikwa na kupelekwa geza ulole, baada ya miezi miwili mmoja, alikuwa maarufu sana Dar. akatoroka huko akawa anaonekana £Dar., anasema "heri ya jela kuliko huko, njaa tupu, mpaka mwanamme hakuna tena, ukiona ukuni umesimama ujuwe nyoka huyo, yamenishinda".
Kwa nini mashoga wengi wanaotambulika tangu zamani wamekuwa wakitokea pwani??
 
AlhamduliLlah nilikuwepo.

Hakuna faida hata moja, hasara tupu. Watu wengi walidhalilishwa na wengi kufa na nchi mpaka leo mekuwa kama mkorogo wa kienyeji.
Naona Malaya wa zamani kanyanyua kisimi kujutia relocation

Pole sana changupapa
 
Nyerere alianzisha miji midogo sio vijiji
Watu walihamishwa vijijini kwenye mashamba yao wakaenda kurundikwa kwenye ka mji watakapopewa maji shule na hospitali
Nyerete ndie aliua kilimo Tanzania kwa kuanzisha hivyo vi miji vyake

Toka hapo kilimo kikaanguka chali
Zamani ardhi ilikuwa tupu watu wachache acha uongo ..hapakuwa na shida ya mashamba hata hspa dar es salaam watuwalikuwa wanalima na ardhi inabaki bila kulimwa
 
Nyerere alianzisha miji midogo sio vijiji
Watu walihamishwa vijijini kwenye mashamba yao wakaenda kurundikwa kwenye ka mji watakapopewa maji shule na hospitali
Nyerete ndie aliua kilimo Tanzania kwa kuanzisha hivyo vi miji vyake

Toka hapo kilimo kikaanguka chali
Fake news
 
Maswala haya ya kuhamisha watu yalisababisha kutoka kwa mgogoro mkubwa sana baina ya mkulima mkubwa sana wa mahindi anayekwenda kwa jina la Mwamwindi wa pale isimani Iringa na J. Nyerere.

Ilikuwa Noma zaidi ya Noma.
Ila ujasiri wa mwamwindi ni noma 🫡🫡🫡😀, unamfyatua RC risasi halafu unambeba mpaka kituoni..!
 
Kwa ujumla zoezi la vijiji vya ujamaa lilifanyika bila ridhaa ya wananchi, ndiyo sababu halikuendelea. Sehemu ambazo zoezi hili lilifanyika maendeleo yalirudi nyuma. Moja kati ya tatizo kubwa ilikuwa ni watu kuhamishwa mbali na mashamba yao, hivyo kufanya kilimo kuwa cha shida. Watu walihamishwa bila msaada wowote na hii iliwafanya wengi warudi kwenye umasikini. Watu walianza kuishi maisha ya kimji na kusababisha kuporomoka kwa maadili. Hayo ni baadhi tu ya hasara.
 
Kwa Dar es salaam, Chanika ndio mfano halisi wa kijiji cha ujamaa.
Ok. Kumbe na Chanika pia. Maana niliwahi kutembelea Mbande mwaka 1998 ikiwa ni sampuli ya Kijiji cha Ujamaa kwa miaka hiyo ya kati ya 1970s.
 
Asante mkuu.

Walitokea wapi? Una ushahidi wowote ule? Labda kutoka kwenye kitabu, gazeti, makala n.k hii itatusaidia sana baadhi ya watanzania ambao tunayasikia haya leo.
Asante
Vijiji vya Ujamaa vilianza 1974 kwa lengo la kuwakusanya wananchi kukaa pamoja kwa ukaribu na kuzalisha mali e.g kilimo na ufugaji. Sina ufahamu hao wakazi wa Mbande au Gezaulole serikali iliwaweka hapo kutokea wapi. Ila vitabu vimeainisha vijiji vingi vilivyokuwepo e.g Mbande, Chanika n.k. Vipo vitabu vilivyoandika kuhusu vijiji vya Ujamaa ktk Makala yake kama vile: SOCIALISM IN TANZANIA (1972); Volume 1. Kimehaririwa na Cliffe & Saul, J.S.
 
Back
Top Bottom