Naombeni ufafanuzi wa faida na hasara za operesheni vijiji 1974

By force by power by πŸ”₯ πŸ”₯ πŸ”₯
Inatoka order mnapewa mda , usipohama watu watakuja kukubeba wewe , mke na watoto tu.
Ni heri ukubali kuhama mapema unaweza kupewa msaada wa kubebewa vimbuzi vyako
Huu mchakamchaka uliwahi tokea huko Ussr mwaka 1936-1937 ikijulikana kama GREAT PURGE.
 
Tafuta hii riwaya ya Prof Kezilahabi utapata kitu kuhusu hayo mambo ya vijiji vya ujamaa!

BTW:Kama vingeendelea hadi leo hata baada ya ujamaa kufa yawezekana REA na RUWASA zingefanikiwa kufikia 99% ya kaya zote nchini hadi sasa maana watu walipangwa karibu karibu hivyo rahisi kuwapatia huduma za kijamii.
 
Asante.
Nimepata kianzio cha kuyajua na kuyaelewa masuala haya.

Ilihali ni vigumu, na mtu yeyote yule asikudanganye, ni vigumu kuanza kutoa ufafanuzi wa faida na hasara ya operesheni iliyotokea 1974 bila kutambua upeo wa ki jiografia na hususani, maeneo waliyonyofolewa watu na kubwagwa.

Yaani, watu walihamishwa kutoka maeneo yapi[kutoka sehemu yeyote ile nchini] na kupelekwa maeneo mengine yepi.

Hiyo juu ndiyo ilikuwa ni premise ya swali langu huko juu.

Hata hivyo nitajitahidi kufanya kuperuzi kitabu hicho na vyanzo vingine ili kupata maelezo ya kina kabla ya kutoa ufafanuzi unaoeleweka zaidi ya assumptions zilizotolewa na "magwiji" wanaonekana wana biases zao.

Asante Mwafrika.
 
Mwenye anajua ni kijiji gani(kimoja tu) kilichoanzishwa wakati huo, anijulishe.

Kiliitwaje?

Watu wanaodaiwa kuhamishwa,

Walitoka wapi?
Na walienda wapi?

Je, bado wapo? Na kama wapo mbona huwa hatuwasikii?

Nimekaa pale.
Geza ulole
 
Siku zote kufanya uchanganuzi wa hasara na faida hutegemea na mtazamo wa mtu au uzoefu watu aliyopitia au kuona. Hivyo, ni utata (complexity).
 
AlhamduliLlah nilikuwepo.

Hakuna faida hata moja, hasara tupu. Watu wengi walidhalilishwa na wengi kufa na nchi mpaka leo mekuwa kama mkorogo wa kienyeji.
Jazia nyama bibie, Ili sisi wa 2000 tujue Kwa undani zaidi, ikiwezekana tugome huyo mwenye heri kuitwa mtakatifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…