Naombeni ushauri chuo gani kizuri kwa kozi ya ICT

Naombeni ushauri chuo gani kizuri kwa kozi ya ICT

zigi 01

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2017
Posts
317
Reaction score
170
Naombeni ushauri chuo gani kizuri kwa kozi ya ICT kati ya vyuo hivyo hapo kwa level ya degree!. Chuo kizuri kwa kozi ya ict kati ya must, arusha tech na ardhi
 
ICT inategemea na kichwa chako , mapenzi katika course husika material nyingi zipo mtandaon ni wewe kusoma na kufanya practical, ukiweza ivyo utakuwa best katika kitu unachotaka kujua ila kumbuka uwez master field yote ICT kwa sababu ni pana sana chagua unachotaka( programming , Networking , system admin , database admin , system analysis and design , computer repair and maintenance and security )kuwa best ila ivyo vingine utakuwa na basic knowledge tu.
 
Kujibu swali lako kwangu Arusha Tech kwangu ni best kwasababu wako mature sana kwenye iyo Field.
 
Usichokijua mdogo wangu ni kwa waalimu wa vyuo wengi Tanzania wanafanana fanana tu

Mchawi kichwa chako na utayari wako
 
Nijuavyo mimi kitu chochote ukisomea hapa Tanzania soma vyuo ambavyo vina network kubwa ya kukuongezea uwezekano wa kukupa ajira hata kama huna connection, haya mambo ya kuwa nondo / kuiva ni kupotoshana kwa elimu ya bongo, mambo ya unondo waachie wahindi. wazungu, wachina, n.k. wanaobuni solutions, kufanya projects, kuanzisha start ups zinazofanikiwa, n.k.

Hivyo basi nashauri usome vyuo vyenye probability nzuri ya kukupa ajira kama UDSM kwasababu karibi 70% ya viongozi wa taasisi na mashirika wamesoma hapa na huwa hawasemi lakini kuna upendeleo flani wanawapa wahitimu wa udsm kwenye ajira na fursa nyinginezo kama scholarships, grants, n.k.

Vyuo vingine ni kama Mzumbe na Udom, ni vyuo vilivyoweza kutoa watu wengi waliosambaa kwenye yop system hivyo network yao sio haba,

Ukishindwa hapo nenda vyuo vingine kama DIT, MUST, Arusha Tech, n.k. Ni vyuo vya sayansi vinavyosifika kuwa vigumu na wanafunzi wao hujisifu wapo nondo lakini mwisho wa siku wakihitimu hawawezi kutumia unondo huo kujitegemea kubuni vitu au kufanya projects za maana kwasababu elimu ya bongo ipo nyuma sana katika ulimwengu wa kisasa, na wao wanaanza kugombania ajira.

Make a wise choice
 
Naombeni ushauri chuo gani kizuri kwa kozi ya ICT kati ya vyuo hivyo hapo kwa level ya degree!
Viko vyuo viwili.

1. Youtube (free).

2. Udemy (10usd/kozi).

Hibi vyuo hata walimu wa hivo vyuo ulivotaja huwa nao wanasoma huko.
 
Back
Top Bottom