Narudia tena,matatizo ya ndugu hayaishi,leo ukimaliza ya wadogo zako watakuja wajomba na mabinamu,huu ndiyo wakati wako kujipanga kumbuka una watoto pia muda siyo mrefu wanaanza kuhitaji shule hapo ndipo hutaweza kabisa kusimamisha hata slop ya chumba kimoja,familia yako bado inaweza kuendesheka kwa kujibanabana anzisha mradi wowote nje na mshahara hata kama uwe mdogo tu,utakusaidia kwanamna moja au nyingine,harafu punguza mambo yote ambayo unahisi siyo ya lazima kila mwezi najua mazoea yana tabu lakini ukiamua unaweza,laki saba kwa siku 28 ukizipangilia vizuri ni hela nyingi sana,ila ukiishi kama wanavyoishi maofisa laki saba ni hela ndogo mno.