Naombeni ushauri juu ya namna ya kupanga bajeti na kuiishi!!!!

Siri ya kupiga hatua ni kuwa bahiri mke na watoto hauishi nao sasa nyumba ya laki ya nini kwa mwezi,punguza kusaidia ndugu matatizo ya ndugu huwa hayaishi saidia zile shida za msingi tu
Asante kwa ushauri!Ninaishi pamoja na mke wangu pamoja na wanangu wawili.Siishi na wadogo zangu ndicho nilichomaanisha
 
Kingine mwanamke kama ni mama wa nyumbani mtafutie kimradi chochote awe anakusaidia hela ya chumvi na sabuni harafu wewe utatue mambo makubwa makubwa
Asante kwa ushauri!Nitaufanyia kazi.Hata hivyo hayo mambo makubwa makubwa unayosema ndiyo niyashughulikie ndiyo yananishinda.Mfano kuna mdogo wangu nimemsomesha hadi kidato cha nne,matokeo siyo mazuri ananidai nimpeleke private school aanze mwanzo nami huo uwezo siyo siri sina.Mbaya zaidi hata mtoto wa dadangu naye ananibana anadai anataka shule.Mdogo wangu wa pili toka mwisho nilichukua hadi mkopo benki aweze kusoma kozi ya afya,kamaliza ila ajira imebuma!!!
 
laki Saba haijui aitumiaje? Tena mbeya kwenye vyakula kibao vya Bei POA aiseee.Anyway hiyo nyumba ya laki moja Hama upesi uko mwenyewe vyumba viko Hadi vya elfu 15.kale kwa mama nitilie kwa siku elfu Tano inatosha kula kwa mwezi kwako laki moja unusu chumba elfu 15
Kaka Mbeya haiko kama tunavyofikiria!Sasa hivi maisha ni magumu.Vyakula bei iko juu!!Unaweza shangaa kukuta chakula kinauzwa bei nafuu Buguruni lakini hicho hicho tunakinunua bei kubwa Mbeya!Niko Mbeya mjini hapa bei za vyakula iko juu.Imefikia wakati watu wanatoka Mbeya na kwenda mkoa wa Rukwa kununua chakula!!!
 
Asante kwa ushauri!Nitaufanyia kazi.Hata hivyo hayo mambo makubwa makubwa unayosema ndiyo niyashughulikie ndiyo yananishinda.Mfano kuna mdogo wangu nimemsomesha hadi kidato cha nne,matokeo siyo mazuri ananidai nimpeleke private school aanze mwanzo nami huo uwezo siyo siri sina.Mbaya zaidi hata mtoto wa dadangu naye ananibana anadai anataka shule.Mdogo wangu wa pili toka mwisho nilichukua hadi mkopo benki aweze kusoma kozi ya afya,kamaliza ila ajira imebuma!!!
Narudia tena,matatizo ya ndugu hayaishi,leo ukimaliza ya wadogo zako watakuja wajomba na mabinamu,huu ndiyo wakati wako kujipanga kumbuka una watoto pia muda siyo mrefu wanaanza kuhitaji shule hapo ndipo hutaweza kabisa kusimamisha hata slop ya chumba kimoja,familia yako bado inaweza kuendesheka kwa kujibanabana anzisha mradi wowote nje na mshahara hata kama uwe mdogo tu,utakusaidia kwanamna moja au nyingine,harafu punguza mambo yote ambayo unahisi siyo ya lazima kila mwezi najua mazoea yana tabu lakini ukiamua unaweza,laki saba kwa siku 28 ukizipangilia vizuri ni hela nyingi sana,ila ukiishi kama wanavyoishi maofisa laki saba ni hela ndogo mno.
 
Kwa mwendo huu braza, sahau kufanya maendeleo, inaonekana una huruma kupitiliza, kama walivyosema wachangiaji waliopita saidia zile shida za msingi tu, hao wanaotaka private sijui nini, wanatakiwa wajue uchungu wa pesa hata kama unasomeshwa kayumba ukiwa na uchungu na pesa ya ada utasoma kwa nguvu zote, mtoto wa dada hana baba.
 
Wadogo zako wana umri gani?? Jibane uwawezeshe katika biashara (hata ndogo tu) itakayoweza kusupport maisha yao. That way hawato endelea kukutegemea wewe. Katika maisha lazima itafika point kila mtu atajitegemea kua chachu ya kuwafanya wadogo zako wajifunze kujitegemea. Pili kwanini usiishi na familia yako? Siku zote mji bora unajengwa na vichwa viwili ke na me, inaweza kua huendelei sababu hakuna mtu wa karibu zaidi anayeweza kukushauri.
Asante saaana kwa ushauri,nitaufanyia kazi!!!Naomba nirekebishe jambo moja ambalo naona nimeteleza kwenye uandishi.Ninaishi na mke pamoja na watoto wangu!Siishi na wadogo zangu!!!
 
Narudia tena,matatizo ya ndugu hayaishi,leo ukimaliza ya wadogo zako watakuja wajomba na mabinamu,huu ndiyo wakati wako kujipanga kumbuka una watoto pia muda siyo mrefu wanaanza kuhitaji shule hapo ndipo hutaweza kabisa kusimamisha hata slop ya chumba kimoja,familia yako bado inaweza kuendesheka kwa kujibanabana anzisha mradi wowote nje na mshahara hata kama uwe mdogo tu,utakusaidia kwanamna moja au nyingine,harafu punguza mambo yote ambayo unahisi siyo ya lazima kila mwezi najua mazoea yana tabu lakini ukiamua unaweza,laki saba kwa siku 28 ukizipangilia vizuri ni hela nyingi sana,ila ukiishi kama wanavyoishi maofisa laki saba ni hela ndogo mno.
Asante kwa ushauri nitaufanyia kazi!!
 
Get a beer... drink it well.. you will hv a way....
Asante kwa ushauri wako,ingawa situmii beer na soda sidhani kama kunywa beer kunaweza kunipa suluhu ya matatizo yangu!!Hapa nilipo kuna wanywa bia wengi lakini hakuna mwenye mafanikio hata mmoja labda huyo aliyekwenda Misri!!
 
Usipokuwa makin na ndugu kiukweli hautapiga hatua kamwe maana hyo hela ukiitazama kama ndogo lakini mwingine akiipata kama hiyo na akawa na upana Wa familia kama ulioyonayo atakuacha mbali sana kimaendeleo kikubwa kwa sasa iangalie familia yako kwa jicho la karibu ndugu hana uchungu na hizo fedha unazotoa. Mimi mdogo wangu alifeli nikapambana kumsomesha private tena boarding mwishoni akampiga mwalimu wake akafukuzwa shule yani sina hamu tena na ndugu aisee
 
Usikae na loosers.....ukikaa bar...ukakuta watu wanagonga beer za kutosha bila mawazo....na ww fanya hivyo hivyo jenga nao urafiki.....baadae mfaamiane....kisha waulize wao wanafanya shuhuli gani.....kama ni za halali stick to them you will get somewhere....hakuna watu wana connection kama walevi ama wanywaji.....tek it to the bank... goodnight
 
Usipokuwa makin na ndugu kiukweli hautapiga hatua kamwe maana hyo hela ukiitazama kama ndogo lakini mwingine akiipata kama hiyo na akawa na upana Wa familia kama ulioyonayo atakuacha mbali sana kimaendeleo kikubwa kwa sasa iangalie familia yako kwa jicho la karibu ndugu hana uchungu na hizo fedha unazotoa. Mimi mdogo wangu alifeli nikapambana kumsomesha private tena boarding mwishoni akampiga mwalimu wake akafukuzwa shule yani sina hamu tena na ndugu aisee
Asante sana kwa ushauri!!Unajua baada ya kuoa niliogopa sana kupunguza huduma kwa ndugu zangu kwa sababu kama unavyojua hawachelewi kumchukia mke na kudai labda kanipa mlungula si unajua tena jamii zetu hizi za kiafrika!!
 
Huruma iliyopitiliza inakuponza!
Wapo watu walisomesha koo zao(wa kwao & wa kikeni) & maisha yao yalibaki hivyo hivyo mpaka na wanakufa!... Mbaya zaidi hao waliosomeshwa wengine wako vizuri lakini waliwatupa waliowasomesha....Wala hawawakumbuki mayatima wao waliowaacha.
Usipokuwa makini huko ndipo unapoelekea!
 
Asante kwa ushauri!!
 
Pango sh.100,000/=
Ada ya mtoto sh.50,000/= kwa mwezi
Akiba sh.200,000/=
Maji na umeme sh.50,000/=
Chakula sh.200,000/=
Mavazi sh.50,000/=
Matibabu (Bima ya afya)
Sadaka sh.30,000/=
Mengineyo sh.20,000/=

Hapo huna cha ku-save budget yako tayari ipo tight...

Cc: mahondaw
 
Kwa mwendo huu braza, sahau kufanya maendeleo, inaonekana una huruma kupitiliza, kama walivyosema wachangiaji waliopita saidia zile shida za msingi tu, hao wanaotaka private sijui nini, wanatakiwa wajue uchungu wa pesa hata kama unasomeshwa kayumba ukiwa na uchungu na pesa ya ada utasoma kwa nguvu zote, mtoto wa dada hana baba.
Nashukuru kwa ushauri!Nitaufanyia kazi
 
Mkuu ninajitahidi kujibana lakini kila ninachohifadhi,mwezi hauishi na chenyewe kinaisha!!Sababu kubwa hata nihifadhi vipi shida hasa za wanafamilia zinatokea mara kwa mara!Labda sijui unamaanisha nini kwa hilo neno kuwa maisha ni kujibana!!!
Buni kamradi hata ka Kufuga kuku wa Mayai angalau Wachache km Mia hivi shemeji ausimamie, itasaidia kupunguza ukali wa maisha.
 
Unaposema 'shida za wanafamilia haziishi' ndio kwenye jibu lako. Anzia hapo....usitegemee utazimaliza shida za watu wote,fanya yale yaliyo ya muhimu tu,shida zingine kataa...ishi kibahili sio unaishi kama Mother Theresa hutatoboa ndugu
Kwa hiyo wewe hautaki kuiga mfano wa Mtakatifu Mama Theresa wa Calcutta???.
 
Back
Top Bottom