Naombeni ushauri juu ya namna ya kupanga bajeti na kuiishi!!!!

Bro unayumba sana.
Unayumba siyo kawaida.
Hivi ushapiga hesabu na ukapata jibu kabisa kwamba hicho kibarua chako kikiota majani utaishi vipi[emoji16]?

Kiufupi tu mimi nakushauri upunguze matumizi amabayo hayana ulazima sana + kutengeneza plan B.
Yaan mradi amabao utakuhakikishia kula. Fanya biashara, kilimo au ufugaji.
Vya kufanya vipo vingi. Panga na mke wako.
Hao wanafamilia nao angalia wasikurudishe nyuma pia. Wasaidie kiasi fulani siyo mpaka ushindwe kufanya mambo ya msingi.
Kw mfano huyo dogo aliyefeli form4. Fanya mopango umuwezeshe kupata shughuri ya kufanya. Usimurudishe xkul.
 
Nashukuru kwa ushauri nitaufanyia kazi
 
Ok
 
Unapofeli ni unapanga bajeti ndio una save.ukweli ni kwamba save kiasi kadhaa ndio upange budget,yaani labda unaseve laki mbili kwanza ndio ipange budget yako iangukie within 500k
 
Maana fupi ya Neno SALARY
S=Small
A=Amount
L=Limiting
A=And
R=Restricting
Y=You
 
Unapofeli ni unapanga bajeti ndio una save.ukweli ni kwamba save kiasi kadhaa ndio upange budget,yaani labda unaseve laki mbili kwanza ndio ipange budget yako iangukie within 500k
Ufafanuzi tafadhali bado sijakuelewa
 
Kwanza punguza Kodi ya nyumba,kapange nyumba ya 60000 kwa mwez mbeya mjin nyumba sio bei sana,nimeishi hapo for 10 years uyole,ituha,mama John hata I'd yako inamaanisha chumvi(nakijua kisafwa )
2_baada ya ku regulate Bei ya nyumba,bana matumiz nunua vitu vya kula vya jumla Pia Hao ndugu zako punguza msaada waambie upo vibaya ukifanya hivyo utakuwa na akiba nzuri tu
 
Ufafanuzi tafadhali bado sijakuelewa
Save kwanza kiasi cha pesa kwaajil ya maendelea pindi upatapo pesa/mshahara ndipo kiasi kilichobaki ndio ukitumie kwenye matumizi mengine ya kawaida yaan isiwe kinyume chake
 
Asante kwa ushauri nitaufanyia kazi!Maeneo uliyonitajia sijawahiishi huko ila itabidi niyazungukie nipate picha kamili!
 
Save kwanza kiasi cha pesa kwaajil ya maendelea pindi upatapo pesa/mshahara ndipo kiasi kilichobaki ndio ukitumie kwenye matumizi mengine ya kawaida yaan isiwe kinyume chake
Asante
 
Acha kuendekez familia saidia pale inapobid kila mtu anamikono akafanye kazi usipojitambua utazeeka hvohvo umri haumsubir mtu watoto wanakua majukumu yanaongezeka we unaezaje kuish na ndugu wote hao kwan kabla ya hapo hawakuwa na mahal pa kuishi M naona kujitambua n muhimu kuliko bajet unayoiomba
 
Asante kwa ushauri!Ninaishi na familia yangu tu!Ndugu siishinao!
 
Ni kweli nipo mkoa wa Rukwa na mara kadhaa hufika hapo Mbeya kikazi, Kiukweli bei ya Vyakula na Vitu Vingine ni Kubwa Tu Tofauti na Watu Wanavyosema

Maisha Mbeya Ni Ghali Basi Tu Vile Watu Wanapenda Kuongea Wasichokijua
 
Asante sana mkuu!!Huo ndio ukweli!Maisha ya Mbeya hayako kama yanavyosemwa na watu!Mfano kuna mwaka nilikuwa naelekea Dar,mtu mmoja akaniambia nimpelekee kilo 25 za mchele.Nilipokwenda sokoni na kumwambia gharama ilivyo aliniambia niache!Akadai bora anunue hapo Buguruni anapoishi!!
 
Asante kwa ushauri!Ninaishi na familia yangu tu!Ndugu siishinao!
Ok hata kama uishi nao bado wajengee kujitegemea full stop ujue kuna vtu vya msingi vya kusaidia na shida nyingine n za kawaida ambazo mtu anatatua mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…