Naombeni ushauri kuhusu huyu mwizi aliyepigwa Mtaani kwetu

Naombeni ushauri kuhusu huyu mwizi aliyepigwa Mtaani kwetu

Atakaa wiki
Nikutonye tu, kesi zinazoonekana nyepesi Kuna muda hugeuka kuwa ngumu na ukaishia kusota jela.

We endelea kuchati jamiiforums ubebwe halafu ukijifanya jeuri PP atakupeleka mahakamani.

Huko ukienda kukiri tu Eti ulikuwepo wakati raia wakimpiga ila wewe hukumpiga unakula mvua kwa makosa Yale Yale ya waliompiga.

Jiongeze fallah wewe 😬😬😬
Kwahiyo mkuu ni Bora useme hujakuepo
 
Kuna rafiki yangu tulimaliza pamoja O level, miaka ya 2006 seminari moja ipo kanda ya ziwa. kipindi tuko chuo, alipangiwa field Zanzibar. Ameamka asubuhi na mapema kuwahi usafiri na mabegi yake maana alifikia kwa kaka yake alikuwa mhadhiri UDSM. Kuna watu walikuwa wanamkimbiza mwizi, mwizi akafanikiwa kuwatoroka, bahati mbaya kwenye harakati za kumtafuta mwizi wakakutana na huyu rafiki yangu na mabegi yake. Jamaa bila hata kumhoji wakamuitia mwizi, walimpiga na kmwua pale Pale, na haikuwa mbali na kwa kaka yake. R.I.P Y.M Died young and innocent, ulikuwa jinias kwelikweli, waliua ndoto zako.
 
Huku mtaani kuna mwizi alichezea kichapo usiku baada ya kutuhumiwa ni mwizi na kama mnavyojua hili neno ukiitiwa usiku wa saa 7 hata kama sio mwizi raia wanapiga.

Sasa inasemekana kapona hajafa na polisi wanataka kumpitisha awatambue waliompiga na Mimi nilikua nimeenda kumshuhudia akichezea kipondo nawaza asijepata wenge akanijumuisha na Mimi kwamba nilimtembezea mkong'oto.

Nauliza hapa kama nikakamatwa na mimi natokaje kwenye huu msala wakuu sababu hapa JF ni kisima cha maarifa.
Ukiwa na hela utatoka chap.
 
Kweli wanaume mmepiga mwizi na hajafa, hayupo wodi mahututi na anapata jeuri ya kuja kutafuta waliompiga...!
 
Back
Top Bottom