Naombeni ushauri kuhusu mahusiano haya ya mama yangu na huyu mwanaume

Naombeni ushauri kuhusu mahusiano haya ya mama yangu na huyu mwanaume

Ofcourse naungana na mama yenu...she is right .mie nasemaga haya mambo usijudge..mama inaonekana hawezi ishi alone...anahitaji faraja..sema anakosea kuleta hapo mwanaume wake bora muwaambie wajomba..ila sio nyie alafu malizeni kusoma muondoke hapo mmpe mama wa watu uhuru..life is too short to complain!..msihukumu msije mkahukumiwa!
Wajomba huenda choka mbaya wanamtegemea dada Yao kwa pesa
 
Mama yenu hawezi kuishi bila mwanaume...
24+ muhame mkaishi kwenu, yupo hivyo miaka yote inaonekana tokea avunje sinia....mumuache mama afurahie mgegedo, vipi nyie??

Mnataka kugombea URITHI, baba wanne tofauti ni ishara mjitegemee...mtafute vyenu...hapo hamna chenu!

Everyday is Saturday.......................... 😎
Tatizo lipi hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo gani madame!
.
 
"Sisi sote miaka yetu ni 24+ na Mama yetu ni 52,Jambo linalotusumbua ni kuwa" Mama

Nyie watu wazima what are you doing at your mum's home......she has her own life leave her alone she sacrificed for you and educated you that's enough go away at 52 she still needs a man to entertain her.......nyie siwelewi kabisa wengine tumeanza maisha at 18 na timefanikiwa mkbali tu, hayo ya mama wenu

Sent using Jamii Forums mobile app


Naunga hoja kabisaaa!...ni vile maza hawez kuwaelezea wht she has been throu na rlshp zake nne!..so anamaumivu fulani moyoni...acha ajipoze jamani/! I like her
 
Habari zenu,

Naombeni ushauri na njia za kutatua tatizo hili.Ipo hivi kwenye tumbo la Mama yetu tulikuwa watoto 7 hadi Leo hii tupo 4. Katika watoto 7 tumezaliwa na Baba tofautitofauti 4. Katika hao baba zetu kuna moja wao ndio tumekuliwa kwake toka tukiwa wadogo badaye miaka 6 iliyopita Mama alitengana Nate.

Mama ni mtumishi wa umma, hivyo alinunua kiwanja na kujenga nyumba ambapo watoto wote 4 tuliongozana nae na kwenda kuishi nae, maana haikuwezekana kukaa tena kwa huyo baba mlezi sababu katika wathili.4 tuliobaki kati yetu 1 tu ndio mwanae kwahiyo ikabidi wote sisi sote tuongozane na mama. Ikumbuke kuwa katika sisi watoto 4, mtoto 1 hamjui baba yake wengine 2 Baba yao alifariki na mtoto 1 baba take ndio huyo aliyetulea.

Sisi sote miaka yetu ni 24+ na Mama yetu ni 52, jambo linalotusumbua ni kuwa Mama yetu ana mwanaume mwingine ambaye ni mume wa mtu. Jamaa huyu huwa anakuja na kulala hapa nyumbani karibu kila siku; huwa anasitisha kuja pale ambapo kaka yetu mkubwa akija nyumbani.

Ndugu na marafiki wamejaribu kumshauri mama kuwa tayari umri umekwenda na ana vijana wakubwa anatakiwa kuacha mambo hayo pasipo mafanikio, haelezeki wala haambiwi chochote. Kwa sasa tumefunga chuo sababu ya hii CORONA nipo hapa home naona aibu kijiji kizima kinatuzungumza.

Kaka yangu mkubwa alijaribu kuongea na muyo bwana mwaka jana; kwa kweli jamaa alisitisha kama miezi 2 hivi pasipo kuonekana, badaye ratiba ikaanza kama kawaida nimemjulisha kaka atafute siku 3 nyumbani tusaidiane kutatua tatizo hili. Pia, kila tukimsuhi Mama kuacha hiyo tabia majibu anayotupa ni kuwa huu mji ni wake na hamna aliyemsaidia kujenga hivyo anafanya chochote atakacho.

Ndugu zangu wana JF, naombeni msaada wa mawazo namna ya kutatua tatizo hili.
Pole sana.
 
Poleni,wanaowasimanga hapa hawajapitia mnayopitia. Duh mmetangishwa sana tangu utoton inaonekana maza hajatulia kabisaa. Hali hio muizoee tu

Kuna wamama/wababa hawashuriki,mapenzi ni upofu.
 
Ikiwaga hivyo hakunaga hata kikao😄😄😄..salute kwa sisy yao..lols..pesa ndo mchawi wao
Mkuu, ukute maza anawa-frustrate makusudi hawa vijana wahame..
Kawachoka labda kula kulala bure, KKB??
Kisha wanajidai wanaleta vibezi. 😀
Tujiulize kwann amuogope kaka mkubwa?
Huenda huyo bro tiyari ana maisha...

Madogo wakapige vibarua wakapange, waishi kimpango wao..hapo maza aweza gawa URITHI hiyo nyumba kwa ANKALI, na hawana cha kumfanya.

Everyday is Saturday...........................😎
 
Nimewazaaaa nikashindwa cha kuwashauri. Sababu huwezi sema mtumie ndugu as kila mtu ana mjomba wake, shangazi yake, baba mkubwa&mdogo wake, babu yake, yaani vululu vululu.

Cha msingi hapo kaeni mbali na matendo ya mama yenu msije mkaingia kwenye laana zisizo za lazima. Kwa kuwa mmeshamshauri na hashauriki kaeni kimya. Kuweni busy na mambo yenu wala msiwaze hayo matendo ya mama yenu kwani mtajipa stress za buree.
Unforgetable
kwa kweli mamaza huwa wanaharibu sana kuzaa na wanaume wengi
 
Back
Top Bottom