Naombeni Ushauri: Mke amenishtaki kuwa nimempiga

Kuna mtu nilimhisi kwa hiyo nick name lakini kwa uandishi huo nimemtoa,ila mpaka utumie hiyo nick name lazima nakufahamu,lakini jirekebishe wewe then think again kuhusu huyo wife.
 
Huyo hafai kuitwa mke, ni muhuni flani hivi ambaye ameshakuchoka na ukiendelea nae atakuja kukutoa roho
Mbona mnamuhukumu dada wa watu? Mnaogopa nini kumwambia ukweli jamaa? Jamaa amefeli kumpiga mkewe, tena inaonekana amempiga sana kiasi cha hadi kuuguzwa na wazazi....
 
Siku chache zilizopita tuligombana na wife wote tuliumia, lakini baadaye akaenda police kunishtaki kuwa nimempiga na jalada lipo Polisi.

Naombeni ushauri kukiepuka kikombe hiki.
Acha kupiga mwanamke.
 
Kisa cha kuambiwa huna mke na wewe unakubali ni nini sasa! Kwani magomvi hayatokeagi na watu wakafikishana mbali na wakarudi wakasameheana tena! Mbona we ulimpiga kiasi cha kwenda kutibiwa na kwao? Na yeye akiambiwa hana mume hapo je?
Kufikia hatua ya kupigana ni dalili mbaya kwenye mahusiano. Ipo siku mapanga yatahusika na kupotezeana uhai.
 
Ndik ujifunze

Mke hapigwi ngumi

Wazee wazamani walikuwa wanampiga kwa upande wa khanga......

Baadae wakawa wanatandika wake zao kwa mapande ya wax

Siku hizi mke anapigwa kwa Toyota Vanguard au Ford Everest....ukikosa unamtandika na IST


Kama una maguvu sana badala ya kipigana na mkeo chukua jembe kalime.......ngumi muachie Matumla
 
Umasikini bwana, eti mtu anapigana na mke wake.

Haya mambo huwezi sikia kwa matajiri.
Kama halijawai kukuta kaa kimya tu,yanatokea sana tu.pia nina ndugu in matajiri wa kutupwa na walikuwa wanapigana mpaka wakaachana.

Tatizo mnaidhani wanawake wa kizungu in sawa na wa kiafrika makuzi yanatofautiana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…