Naombeni ushauri: Mke wangu amejua kuwa nina mtoto kwa mwanamke mwingine

Naombeni ushauri: Mke wangu amejua kuwa nina mtoto kwa mwanamke mwingine

Kilawo

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2016
Posts
1,631
Reaction score
2,778
Tangu nimeoa saizi natimiza miaka saba ndani ya ndoa yetu na tumebahatika kupata watoto wawili.

Lakini hapa karibuni mke wangu amepata habari kuwa nina mtoto mwingine ambaye nimezalia kwa mwanamke mwingine sasa ananisumbua sana anataka asepe kwao.

1624007073899.png

UPDATE:jamani niwashukuru sana kwa ushauri wenu saizi nipo na naishi safi kabisa namke wangu mke wangu ni Mfanyakazi saizi anafatilia mkopo ili anipe pesa nifanyie biashara zangu Ahsanteni sana kwa ushauri.
 
Pole sana mkuu, zungumza na mkeo muweke wazi na utubu msameheane muendelee kulea familia yenu. By the way, huyo mtoto ulimzaa ukiwa tayari kwenye ndoa na mkeo au alimzaa kabla hujamuoa?

Kama ulimzaa kwa kumcgeat basi tafuta namna bira ya kumuelewesha nkeo, kiri majosa omba msamaha maana umekosea
 
Sasa mkuu tukushauri nini na wewe ndio muhusika. Si uamue kusema hiyo tuhuma ni ya uongo au yaukweli.

Kama ni ya ukweli ndio uamue kuishi na yupi kati ya hao wake zako wawili.

Na huyo mkeo hata kama alikuwa hachepuki, kwa tukio lako lazima afanye Revenge ya yeye kuanza kugawa nje kama ulivyofanya wewe.
 
Acha aende mlete huyo Mama mtoto mwingine ndani maisha yaendelee.kwani yeye ana k ya gold ama??
Watu wasizae kwanini?? Kisa yeye kaolewa.yaani ufe na watoto wawili mwanaume mzima ungeenda kujibu Nini kwa mola wako? Si Ni matumizi mabaya ya. Uumbaji au??
 
Raha ulikula kivyako ila shida unakuja tushee.😂

Anyway mkuu jitahidi kumuonyesha ya kuwa unampenda mkeo wakati huu unapalangana kumuelewesha hakikisha unatoa Hadi uchozi hata wa kibishi..🤣

Hali ikizidi tafuta wazee wamama wenye hekima waongee nae. Pia ukaribu wako uzidi maradufu epuka visingizio vya kimchepuko alasivyo yataibuliwa mengi zaidi.

Kama bado basi jua huo ndo muda muafaka wa kwenda kuroga..🤣🤣

Aya ya mwisho ni joke..
 
Kuna ushauri wa humu ndani wewe mtu na akili zako timamu ukiufuata, walaqhi' you're doomed..!!

Mtu anaongelea 'Ndoa' na siyo girlfriend jamani, kizazi chetu kimepotoka hatari..!!

Mtoa mada, tubu mbele za Mungu kwa dhati kabisa na umuombe usaidizi wake katika hili, kisha zungumza na mkeo wa Ndoa, itakuwa ngumu mwanzoni ila atakuja kukuelewa, na kila kitu kitakuwa sawa naamini..!!
 
Asante kwa ku-share nasi nina maswali mawili kabla yakusema lolote..
1: ulichepuka kupata huyo mtoto kwa mwanamke mwingine au ilikua kabla ya ndoa?
2: unataka wana-Jf tukusaidie nini?
 
Kama ulichepuka ukiwa ndani ya ndoa ni vizuri kujishusha ongea na Mke wako kwa kina ili muendelee na maisha kama kawaida.
 
Pole sana mkuu, zungumza na mkeo muweke wazi na utubu msameheane muendelee kulea familia yenu

By the way, huyo mtoto ulimzaa ukiwa tayari kwenye ndoa na mkeo au alimzaa kabla hujamuoa?

Kama ulimzaa kwa kumcgeat basi tafuta namna bira ya kumuelewesha nkeo, kiri majosa omba msamaha maana umekosea
Uyo mtoto na miezi sita tangu azaliwe.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Unatakiwa uijue kwanza mizania yako,

Yupi Ni ana umuhimu zaidi Kati ya uyo mwanao na uyo mkeo.

Kish maamuzi yako,
Yazingatie zaidi maslahi ya kipaumbele chako Kati ya hivyo viwili.
 
Back
Top Bottom