Naombeni ushauri: Mke wangu amejua kuwa nina mtoto kwa mwanamke mwingine

Naombeni ushauri: Mke wangu amejua kuwa nina mtoto kwa mwanamke mwingine

Asante kwa ku-share nasi.nina maswali mawili kabla yakusema lolote..
1: ulichepuka kupata huyo mtoto kwa mwanamke mwingine au ilikua kabla ya ndoa?
2: unataka wana-Jf tukusaidie nini?
Ushauri mke wangu anataka kuondoka kisa nimezalia kwa mwanamke mwingine .Sasa tumebahatika kujenga kibanda na tuna duka sasa anataka tugawame.
 
Unatakiwa uijue kwanza mizania yako,

Yupi Ni ana umuhimu zaidi Kati ya uyo mwanao na uyo mkeo.

Kish maamuzi yako,
Yazingatie zaidi maslahi ya kipaumbele chako Kati ya hivyo viwili.
Ni mke wangu wa ndoa na tuna watoto wawili wa kwwnza 4 na wapil 1na miez sita sasa mke wangy hataki kunielewa.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Unatakiwa uijue kwanza mizania yako,

Yupi Ni ana umuhimu zaidi Kati ya uyo mwanao na uyo mkeo.

Kish maamuzi yako,
Yazingatie zaidi maslahi ya kipaumbele chako Kati ya hivyo viwili.
Mkuu, kila mmoja ana umuhimu kwa uzito wake, cha msingi jamaa lazima ahakikishe analinda ndoa yake maana amemkosea mke kwa kumsaliti, lazima ajishushe na atumie busara kuzungumza na mke, kumbuka ana watoto wawili na mke wa ndoa
 
Ushauri mke wangu anataka kuondoka.kisa nimezalia kwa mwanamke mwingine .Sasa tumebahatika kujenga kibanda na tuna duka sasa anataka tugawame.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Usihofu,
Iyo ya kugawana hua haipo, Anakupima

Na huo Ni mtego
"on how strong you are"

Ukilegeza apo Kwenye kukutishia kugawana mali, UMEKWISHA.

Na
iyo ndio itakua silaha yake milele kukutikisa na kukunyanyasa kwa chochote atakacho ktk ndoa.

USIWE LEGE LEGE,
STAY STRONG AS A MAN and HEAD OF FAMILY.

Mali zisikupelekeshe mputa mputa mpk kukuondolea Utu na Uanaume Wako na kuondolea Total control ktk familia yako.
 
Ushauri mke wangu anataka kuondoka.kisa nimezalia kwa mwanamke mwingine .Sasa tumebahatika kujenga kibanda na tuna duka sasa anataka tugawame.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Mkuu pole sana kwa hilo. Najua kweli utakua katika wakati mgumu kufanya maamuzi, kiukweli kabisa mkuu umemkosea mke wako kwa kuzaa nje ya ndoa na wakati yeye alikua na uwezo huo pia.so cha kufanya hapo ni

1: kubali kosa lako kwake na muombe msamaha mkeo.tumia njia yoyote ile ambayo haitumuumiza zaidi kumuomba msamaha kumbuka mwanamke yoyoote yule anaendeshwa na kufanya maamuzi kwa hisia.

Kwa ufanisi mkubwa katika hili jaribu kumkumbusha malengo yenu katika ndoa na mkumbushe kwanini ulimchagua yeye mbele ya hao wengine ili kufikia malengo mliokua mmjiwekea.

2: Tubu dhambi zako kwa Mungu wako na omba ulinzi wa Mungu ili huyo Mwanamke mwenza asije tumiwa na ibilisi kuangamiza ndoa yako.pia kumbuka kumshukuru Mungu kwa ajili ya mkeo na muombe Mungu ampe Moyo mkuu wa kustahimili haya majaribu katika ndoa yake.

Ni hayo tu mkuu nikutakie kila la kheri katika kujenga ukuta uliobomoka katika ndoa yako. Mungu akutangulie......
 
Acha aende mlete huyo Mama mtoto mwingine ndani maisha yaendelee.kwani yeye ana k ya gold ama??
Watu wasizae kwanini?? Kisa yeye kaolewa.yaani ufe na watoto wawili mwanaume mzima ungeenda kujibu Nini kwa mola wako? Si Ni matumizi mabaya ya. Uumbaji au??
Tunapozungumza ndoa mama ni kile kiapo, kama ingekua ni rahisi namna hiyo watu wangekua wanazaa tu na kusingekua na sababu ya kuwa na ndoa, ndoa ni familia, kumbuka ana watoto wawili na mke wa ndoa, how do you feel hao watoto wakaenda kulelewa na mzazi mmoja kwa sababu ya usaliti wa mume?

Umejaribu kufikiria hayo maumivu anayoyapitia mke baada ya kugundua ndoa yao imesalitiwa? Vipi watoto ni wadogo lakini when they grow up watajua kwamba baba alisaliti ndoa na kuzaa nje na matokeo yake mfumo mzima wa maisha yao uliharibika, unajua implication ya hili jambo kwa ujumla?

Mimi nadhani jamaa ampe mke wake muda wa kuheal wasameheane walee watoto wao, lakini end of the day asitegemee tena kwamba things will be the same kwenye ndoa yao, upendo ule wa mwanzo hauwezi kuwepo, imani ile ya mwanzo na hata huruma, kwa kifupi things will change and he should be ready for that

Lets say akamchukua huyo mchepuko kuishi nae, unadhani ndio furaha yake yaitarejea? Lets say akamsaliti mchepuko tena akazaa nje, utamshauri amuache aanze kuishi na huyo mchepuko mwingine? There are times in life kila binaadamu anatamani awe na settled life ndio maana watu wanafanya maamuzi ya kuoa na kuanzisha familia
 
Wewe mwenyewe mtoa mada unafikiriaje uamuzi wa mkeo? Yuko sahihi au? Ukitafakari haya maswali kwa kina utapata suluhisho lako.
 
Mkuu, kila mmoja ana umuhimu kwa uzito wake, cha msingi jamaa lazima ahakikishe analinda ndoa yake maana amemkosea mke kwa kumsaliti, lazima ajishushe na atumie busara kuzungumza na mke, kumbuka ana watoto wawili na mke wa ndoa
Umeongea point,
BUSARA lazima itawale, na lazima ajishushe.

Ila inabidi awe na tahadhari sana, maana mwanamke keshaanza kutishia wagawane Mali.

Ata Kama kweli mwanaume kakosea, haimpi uhalali mwanamke kuanza kuongelea habari za kugawana Mali badala ya kuconcentrate na tatizo lililoko mezani. Kimaadili haiko SAWA.

Na Kama maadili yanakiukwa Kias icho,
JAMAA anapaswa kua ALERT na kurejea Kwenye UANAUME WA ASILI (MFUMO DUME) ili mwanamke arudi Kwenye mstari.

Akilegeza,
Mwanamke atampanda kichwani kwa mgongo wa tiketi ya KUGAWANA na JAMAA kwasababu keshaonekana Ni dhaifu Kwenye Mali, ATAFYATA MKIA.

Matokeo yake,
1.Atampiga marufuku kumleta nyumbani kwake , hivyo kumnyima haki ya msingi mwanae kuwatambua ndugu zake. Na JAMAA hatakua na la KUFANYA.

2. Ata akikubali amlete nyumbani, tambua kua atamnyanyasa Sana na sometimes Atafanya mbele ya baba ake anaona, na kwasababu JAMAA keshaonesha udhaifu wa hofu ya KUGAWANA, atafyta mkia.

Nnachomsihi,
Awe na BUSARA ila na BUSARA yenyewe iwe na mipaka.
 
Huyo mwanamke yuko sahihi kabisa.
Kuishi na Mwanaume asiye mwaminifu ni Bora kuachana ijulikane moja.

Yani mtu kaona afanye umalaya hadi aweke na alama ya kudumu?

Hapana aisee!
 
Umeongea point,
BUSARA lazima itawale, na lazima ajishushe.

Ila inabidi awe na tahadhari sana, maana mwanamke keshaanza kutishia wagawane Mali.

Ata Kama kweli mwanaume kakosea, haimpi uhalali mwanamke kuanza kuongelea habari za kugawana Mali
Huyo mke amekosa busara, ujasiri wa kuanza kuzungumzia mali anaupata wapi ilhali wana watoto, mwisho wa siku warithi wa hizo mali ni watoto sio mke, kama jamaa anaona inaleta shida ni heri akatafuta ushauri wa kisheria ikiwezekana aandike kwamba mali zake zote ni za watoto, wazazi watawndelea kusimamia mpaka watoto watakapojitambua
 
Mkeo atajiuliza maswali kwa hiyo kumbe yeye hakutoshelezi?

Atajiuliza Je anakasoro labda?

Yani mpaka ashki kwako zitakata !
 
Kama kulikuwa na wanaume wanammendea anawatolea nje sasa hivi ataanza kuwapa ushirikiano mkubwa.

Yani kuanzia sasa utaanza kumuona mabadiliko makubwa sana na si kazi akaanza kupendeza kuliko awali.
 
Umelikoroga linywe sasa!

Sasa hivi hutafurahia penzi la mkeo wala la hawara [emoji108][emoji108]

Dhamiri yako kama iko hai inakusuta na kukuhukumu kuwa na hatia kubwa.
 
Huyo mke amekosa busara, ujasiri wa kuanza kuzungumzia mali anaupata wapi ilhali wana watoto, mwisho wa siku warithi wa hizo mali ni watoto sio mke, kama jamaa anaona inaleta shida ni heri akatafuta ushauri wa kisheria ikiwezekana aandike kwamba mali zake zote ni za watoto, wazazi watawndelea kusimamia mpaka watoto watakapojitambua
Kuna wapuuzi wamemjaza kichwa, wanawake Kwenye Ndoa wanarubuniwa sana hasa zinapotokea sintofahamu Kama hizi Kwenye ndoa
 
Malizana na mkeo umuingize hawara yako ndani mlee mtoto wenu kwa furaha lakini Huyo alokuwa mkeo usimpe jakamoyo kwa starehe zako!
 
Huyo mwanamke ni mjinga sana anahitaji ushauri nasaha wa ndoa na maisha
Huyo mwanamke hakuja kwenye ndoa kwa kumaanisha alikuja kujaribu ndoa, eti anataka kuondoka kwasababu kama hii kweli? Kwani yeye wakati anaolewa alikutwa kaitunza BIKIRA yake??
 
Mbona ni kawaida sana hilo suala. Mwambie aongee vizuri na mashangingi ya mjini yamfunde
Nalog off
 
Back
Top Bottom