Naombeni ushauri: Mke wangu amejua kuwa nina mtoto kwa mwanamke mwingine

Naombeni ushauri: Mke wangu amejua kuwa nina mtoto kwa mwanamke mwingine

Kama kulikuwa na wanaume wanammendea anawatolea nje sasa hivi ataanza kuwapa ushirikiano mkubwa.

Yani kuanzia sasa utaanza kumuona mabadiliko makubwa sana na si kazi akaanza kupendeza kuliko awali.
Huyo mkewe naye azae nje unamheshimu mtu huku hajiheshimu aisee.
 
Ametoa mbili mkuu ,

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Usiseme ametoa Sema umeua watoto wawili wasio na hatia.. Uliwaadhibu adhabu ya kifo Hao Malaika kwa kosa lipi?? Tamaa zenu wanaadhibiwaje wao.. Damu yao itakulilia hadi siku ya mwisho wa maisha yako... Ni heri uue anayeweza kujitetea kuliko innocent creatures..
 
Mpeleke alle kwa mjumbe, huwa wanaushauri mzuri tu wala usiharakishe aondoke hapo
 
Sasa mkuu tukushauri nini na wewe ndio muhusika. Si uamue kusema hiyo tuhuma ni ya uongo au yaukweli.

Kama ni ya ukweli ndio uamue kuishi na yupi kati ya hao wake zako wawili.

Na huyo mkeo hata kama alikuwa hachepuki, kwa tukio lako lazima afanye Revenge ya yeye kuanza kugawa nje kama ulivyofanya wewe.
Wazo nzuri.
 
Acha uoga, nilidhani busara huongezeka kwa kadri ya umri!
 
Tangu nimeoa saizi natimiza miaka saba ndani ya ndoa yetu na tumebahatika kupata watoto wawili.

Lakini hapa karibuni mke wangu amepata habari kuwa nina mtoto mwingine ambaye nimezalia kwa mwanamke mwingine sasa ananisumbua sana anataka asepe kwao.

Huyo mtoto alikuwepo kabla ya ndoa au umempata ukiwa kwenye ndoa na mke wako?
 
Kasema amempata akiwa na ndoani.

Kasema mtoto ni mchanga wa miezi takribani 6 .
Dah.

Hapo kidogo ngoma yake nzito.

Ingekuwa mtoto kapatikana kabla ya ndoa tungekaa vizuri kiumeni kumsaidia jopo la mawakili wa utetezi kusawazisha mambo.

Hapo anatakiwa kiongozi wa dini anayejua maneno ya suluhu, pamoja na viongozi wa familia, wakae chini kuokoa jahazi. Na mwanamme anatakiwa kujishusha sana kuomba msamaha na kupanga familia itakaaje.

Vinginevyo ndoa pasu pasu watu wanagawana mbao.

Huyu mwanamme mwenzetu naye kauza timu.

Kama hakufanya makusudi, anachepukaje bila kujikinga na mambo haya wakati huu kuna mimba, kuna HIV, kuna mpaka Covid-19?

Yote maisha, cha muhimu kabisa ni kutunza familia, akiwamo na huyo kichanga asiye na hatia.
 
Ndo hivo mkuu .Mimi namchukua tu mtoto akae na wenzake maisha yaendelee.ukiondoka unamfaidisha Nani zaidi ya kuleta maafa kwa wanao?
Mashallah.

Nimekupenda bure.

Umemfanya Kiranga kasema Mashallah, mpaka mwenyewe nimecheka contradiction hii.

Before anybody jumps on this, its a purely cultural expession to me.
 
Mume wangu ana mtoto mmoja bahati nzuri Mama yake alishaolewa nahisi ana mwingine hapendi kukubali.asilimia 95 ya wanaume wana watoto nje either kabla ya ndoa or before.so wakati wako wa kuambiwa Kuna mtoto pokea tu maisha yaendelee.kesi ya infidelity kwangu haitokaa inipe shida as long hainiaffect mimi.na wanangu.kila mtu ana akili zake siwezi control akili ya mtu.iko nje ya uwezo wangu
 
Mashallah.

Nimekupenda bure.

Umemfanya Kiranga kasema Mashallah, mpaka mwenyewe nimecheka contradiction hii.

Before anybody jumps on this, its a purely cultural expession to me.
Ahaaa labda umeingiwa na jini la kiarabu
 
Tunapozungumza ndoa mama ni kile kiapo, kama ingekua ni rahisi namna hiyo watu wangekua wanazaa tu na kusingekua na sababu ya kuwa na ndoa, ndoa ni familia, kumbuka ana watoto wawili na mke wa ndoa, how do you feel hao watoto wakaenda kulelewa na mzazi mmoja kwa sababu ya usaliti wa mume?
Abriana .kiukweli nimetania tu
 
Ushauri mke wangu anataka kuondoka kisa nimezalia kwa mwanamke mwingine .Sasa tumebahatika kujenga kibanda na tuna duka sasa anataka tugawame.
Asilimia 70 ya nyuzi za JF kuhusu ndoa zitanifanya nisioe. Yani niko nasikitika mkeo anataka aondoke kwa uchungu wa wewe kuchepuka, kumbe yeye target yake ni kugawana mali.
 
Mwanamke yeyote anayetishia kuwa ataondoka kwenda kwao (kwa wazazi wake) hajakomaa kiakili.

Akikuambia anaondoka kwenda kwao mwambie nenda ila usirudi hadi nitakapokufuata
 
Back
Top Bottom