Naombeni ushauri: Mke wangu amejua kuwa nina mtoto kwa mwanamke mwingine

Naombeni ushauri: Mke wangu amejua kuwa nina mtoto kwa mwanamke mwingine

Mkuu kwa comment hii unaweza kumuolea mke wa pili kabla hajamaliza kufungasha virago.

Style ya Kanye West, kabla talaka haijakamilika ushatoka na model mpya mkali zaidi magazetini.
Huwa nawaambia mabinti zangu, pamoja na kwamba wanawake sio watu wa kuwachukulia umakini sana katika kila jambo lakini haina maana kwamba kila ujinga ni wa kuwachekea.

Ndoa ni zaidi ya kulalana kitandani, sio jambo la mzaha mzaha tu. Fikiria mkeo wa ndoa anakutishia eti "naondoka narudi nyumbani kwa wazazi wangu", mke wa ndoa anakuambia hivo na mdomo kauvuta ~ namwambia nenda lakini hakikisha unakaa na hao wazazi wako hadi nitakapokufuata [emoji16][emoji16]
 
Si gawana naye kila mtu aishi kivyake km mchepuko amekuwa na thamani kuliko mkeo? Kama hauna nia ya kuachana naye jishushe muelewane, jiroge uoe mchepuko hakuna rangi utaacha kuona maana njia ulizokuwa unatumia kumdanganya mkeo anazijua sasa oa afu ufanye kosa hata kuchelewa nusu saaa, gubu la hapo, kelele za umo ndani, utamkumbuka mkeo wa kwanza maana mchepuko naye lazima ataweka akilini kama ulikuwa na mke na ukawa naye lazima kuna mwingine uko naye nje......hakuna amani ni kushindana hump ndani
Saa zote kumbe ulikuwa hujatoa ushauri??
 
Kuna ushauri wa humu ndani wewe mtu na akili zako timamu ukiufuata, walaqhi' you're doomed..!!

Mtu anaongelea 'Ndoa' na siyo girlfriend jamani, kizazi chetu kimepotoka hatari..!!

Mtoa mada, tubu mbele za Mungu kwa dhati kabisa na umuombe usaidizi wake katika hili, kisha zungumza na mkeo wa Ndoa, itakuwa ngumu mwanzoni ila atakuja kukuelewa, na kila kitu kitakuwa sawa naamini..!!
Acha uchonganishi wewe, atubu kwa lipi? kama kabaka sawa au kazzaa na mke wa mtu
 
Kugawana mali ni haki yake, hawezi ondoka mtupu kwa muda aliokaa Kuna vitu amechangia wanaume wengi mnapenda mkiachana na mwanamke basi asipate popote pa kushika ndo furaha yenu
Sio furaha yangu kuona wanandoa wanaachana. Sasa kwanini aondoke wakati ana watoto wadogo mmoja miaka 4 na mwingine mwaka 1.

Wagawane mali akaishi mwenyewe atoke na waume za watu au viserengeti boys watoto wake waishi kwa tabu. Kisa tu mtoto mmoja wa nje?

Kugawana mali ni haki yake ila kwanini wafikie kuvunja ndoa.
 
Sio furaha yangu kuona wanandoa wanaachana. Sasa kwanini aondoke wakati ana watoto wadogo mmoja miaka 4 na mwingine mwaka 1. Wagawane mali akaishi mwenyewe atoke na waume za watu au viserengeti boys watoto wake waishi kwa tabu. Kisa tu mtoto mmoja wa nje?

Kugawana mali ni haki yake ila kwanini wafikie kuvunja ndoa.
Ukisema .unaonekana una uzoefu wa kuchepuka.me siondoki
 
Tangu nimeoa saizi natimiza miaka saba ndani ya ndoa yetu na tumebahatika kupata watoto wawili.

Lakini hapa karibuni mke wangu amepata habari kuwa nina mtoto mwingine ambaye nimezalia kwa mwanamke mwingine sasa ananisumbua sana anataka asepe kwao.

Muache asepe kwani ndgu yako,huyo mpita nja ila mtoto atabaki ndgu yako milele.
 
Ndo hivo mkuu .Mimi namchukua tu mtoto akae na wenzake maisha yaendelee.ukiondoka unamfaidisha Nani zaidi ya kuleta maafa kwa wanao?
Comment hii inaonyesha Ni jins gani ulivyo mwanamke MATURED. Bravo[emoji106]
 
Acha aende mlete huyo Mama mtoto mwingine ndani maisha yaendelee.kwani yeye ana k ya gold ama??
Watu wasizae kwanini?? Kisa yeye kaolewa.yaani ufe na watoto wawili mwanaume mzima ungeenda kujibu Nini kwa mola wako? Si Ni matumizi mabaya ya. Uumbaji au??
Inanishangaza.....
 
Kuandika huku jf flani Malaya hakumfanyi kuwa Malaya .uzoefu wa kuandika bila research Ni ziro tu.
Kila mtu ana style zake za kuishi
Kama hujui stress inaua basi chagua stress.


Nisome vizuri tena utaona sijaku attack wewe personal kuwa Malaya isipokuwa kama uta qualify kwenye hizo tabia anajua ni Mungu na wewe binafsi.

Niko makini sana na uandishi wangu always.

Nimejifunza tangu Mdogo namna ya uandishi wa mahusiano na mawasiliano.

Utaona huwa napenda kutumia nafsi ya tatu ktk kuelezea na si nafsi ya kwanza wala ya pili labda ibidi kufanya hivyo.

Kwa hiyo soma tena kisha jipime mwenyewe.
 
Kuihimili hili zigo inataka moyo sana
👉Umri mkubwa ndo wanaweza hili
👉Kama ke nae ashachepuka nje ya mumewe ama kuzaa nje akiwa kaolewa
👉Una roho mtakatifu

Vinginevyo hapo pagumu Sana sitaki hata kupawazia
 
Hii ishu upande wa pili ni ruksa hata wake wa nne.

Ila sasa nyie wenzetu mnatupinga na sheria zetu

Cha ajabu nyie mnafanya kimyakimya

Fanyeni marekebisho
Kuliko ivi mnavo fanya
Mnawatesa sana wamama
 
Ushauri bora muulize huyo Mkeo....,

Sababu akikubaliana na wewe kila kitu umemaliza; Anyway wanasema Zege ukishalikoroga halirudi tena kuwa sementi....,

kwahio kuwa mpole tu vumilia masimango na lawama kila ukifanya kosa dogo kwa muhusika kukumbushia ulivyofanya...
 
Ushauri mke wangu anataka kuondoka kisa nimezalia kwa mwanamke mwingine .Sasa tumebahatika kujenga kibanda na tuna duka sasa anataka tugawame.
Huyu anataka mali amepata sababu ya kusema,hakuna mkamilifu hapa duniani mngezungumza na kuyamaliza ila kama anataka mgawane mali basi ni mwenye tamaa.
 
Back
Top Bottom