Naombeni ushauri na muongozo wa kazi za viwandani

Double N

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
290
Reaction score
550
Habari ndgu zangu,

Kijana wenu hapa nimekuja kuomba msaada kwenu.

Kwasasa sina mtaji hivyo nimeamua kuliko kukaa bure tu na kusubiri vya kupewa nimeona bora nijikite huko VIWANDANI.

Hivyo basi nimekuja hapa kuomba kujuzwa namna ya kupata hizo kazi, natakiwa kua na nini na nini ili nipate kibarua viwandani?? Pia niko vyema kiafya ya akili na mwili ndio maana naingia huko.

Naomba kujua ni viwanda gani vina ujira mzuri kuliko vingine.

Nipo Dar es salaam wakuu, karibuni kwa maoni.
 
Hongera kijana mwenzangu hata mimi sina kazi nimekuwa nikizunguka viwandan kutafuta ajira bila mafanikio ila sijakataa tamaa, ili nilichogundua kwa viwanda ving n ngumu kupata kazi kama huna mtu wa kukushika mkono.
 
Hapa unatakiwa uwe na hela ya kuonga japokuwa hata 30 ama 50 ,mkono mtupu hua haulambwi
 
Ni viwanda gani ulivyojaribu mkuu?? Na majibu yao yalikuaje
 
Hapa unatakiwa uwe na hela ya kuonga japokuwa hata 30 ama 50 ,mkono mtupu hua haulambwi
Kuna mtu aliniambia kuna viwanda vunahutaji barua toka serikali ya mtaa kama cha backhresa!! Vipi hii imekaaje mkuu. Ni viwanda vyote vina kasumba ya rushwa??
 
Sehemu nyingi sasaivi wanapenda sana uwe na barua ya utambulisho wa eneo utokali.......sio viwanda vingi ila iyo nayo ni mojawapo ya kupata kazi,Fanya kitu kimoja nenda kwenye kiwanda chochote kile jifanye kama mjinga vile kisha piga nae story mlinzi wa getini kisha chukua mawasiliano yake kisha mdakishe hata buku 5 uone atakavyokumwagikia michongo yote ya humo ndani
 
Poapoa makini mzee, shukran sana.
 
Poapoa makini mzee, shukran sana.
toa hela upate kazi.damka asubuhi mapema nenda kwenye kiwanda husika onana na supervisor jaribu kuulizia uonyeshwe supervisors ongea naye kwa maneno shida yako ukiona anazingua mwambie utampa ela elfu 50 usiwe bahiri hiyo 50 utairudisha wiki tu ukiwa job.pia usitake kazi siku hiyo hiyo mwambie kesho asubuhi utakuja nayo hiyo 50 pia kuwa chilii chalii flani usiwe mpole mpole.nakuhakikishia kwa asilimia 80 hawezi kukuacha utakuja kunishukuru ndugu. usisahau mrejesho hapa jukwaani.
 
Kisanga ni kuipata iyo 50k mkuu.
Shukran kwa ushauri mkuu, nimeupokea
 
Habari ndgu zangu,

Kijana wenu hapa nimekuja kuomba msaada kwenu.

Kwasasa sina mtaji hivyo nimeamua kuliko kukaa bure tu na kusubiri vya kupewa nimeona bora nijikite huko VIWANDANI.

Hivyo basi nimekuja hapa kuomba kujuzwa namna ya kupata hizo kazi, natakiwa kua na nini na nini ili nipate kibarua viwandani?? Pia niko vyema kiafya ya akili na mwili ndio maana naingia huko.

Naomba kujua ni viwanda gani vina ujira mzuri kuliko vingine.

Nipo Dar es salaam wakuu, karibuni kwa maoni.
Funga safar mpaka mkuranga pwani kijij Cha mkiu Kuna kiwanda Cha tailiz pale ajila zpo kila kukicha
 
Mkuu naomba unipe details kidogo kutoka mbagala hadi huko nauli sh ngapi? Ili nijitathmini toka huku chanika nilipo nitatumia sh ngapi kwenda na kurudi. Maana kwasasa hali yangu mbaya sana kiuchumi na zaidi sina msaada
 
Kwa Bakhressa kazi za vibarua zipo kila siku pale Buguruni , unapeleka Barua ya serikali za mtaa Unaingia. ,

Utofauti kaz za pale Ni ngumu Sana ndo watu wanahitaji kila siku hivyo nenda kajionee mwenyewe utatupa. Mrejesho.
 
Yaah hii pia kuna mtu alishawahi kuniambia kua pale kazi zipo ila ni ngumu. Kwa hali ya sasa wacha mtu uende walau ukapate uzoefu wa kazi unakuaje.
 
Kwa Bakhressa kazi za vibarua zipo kila siku pale Buguruni , unapeleka Barua ya serikali za mtaa Unaingia. ,

Utofauti kaz za pale Ni ngumu Sana ndo watu wanahitaji kila siku hivyo nenda kajionee mwenyewe utatupa. Mrejesho.
Lakini samahan mkuu hivi ni saa ngapi hasa ni muda mzuri wa kupata apo kazi na je unamuona nani mkuu ila upaye hiyo kazi.
 
Pale nenda na barua ya utambulisho , ukifika utamuona mrinzi nenda kuanzia Ahsubui ya Saamoja J.3 hadi ijumaa au saa kumi na mbili ya jioni.

Angalizo :- kazi Ni ngumu
Unaweza kulipwa elf 6 Lakini kazi yake. Ningumu Sana.
 
Dah mkuu huo msisitizo wa kazi ngumu inaweza kuwa kweli ngoma ngumu. Lakini mkuu kupata ni uhakika?
 
Kwani mkuu masaa ya kazi hapo ni mangapi mkuu? Namaanisha huwa wanaingia saa ngapi na kutoka saa ngapi??
 
Dah mkuu huo msisitizo wa kazi ngumu inaweza kuwa kweli ngoma ngumu. Lakini mkuu kupata ni uhakika?
Sio huyo tu mkuu ni wengi ukiuliza wankupa huo msisitizo wa pale kua kazi ni ngumu. Kwahiyo tuweke akilini tu kua kazi pale ni ngumu twende tukiwa na mentality hiyo.
 
Back
Top Bottom