Pale nenda na barua ya utambulisho , ukifika utamuona mrinzi nenda kuanzia Ahsubui ya Saamoja J.3 hadi ijumaa au saa kumi na mbili ya jioni.
Angalizo :- kazi Ni ngumu
Unaweza kulipwa elf 6 Lakini kazi yake. Ningumu Sana.
Nakuunga mkono, mi nimewahi kwenda kweny hiko kiwanda kuomba kazi, aise lile ni gereza huru, unaeza ukabeba hata viroba buku mwisho wa siku hujui unalipwa sh ngp, Mara utaskia Leo mgao elf NNE Mara elfu tatu.
Jaman vijana wezang jarbun hata biashara lkn sio kuomba kazi kiwanda kile utakufa siku c zako , usalama wa kazi ni mdogo sana vumbi ya ngano ile inapenya mpk kunako mapafu, kazi ngumu malipo ya kishenzi usalama wa afya zero, aisee hawa mawaziri wa viwanda cjui wanafany miaka nenda miaka rudi.
Mle kazi ngumu na malipo yenyee ni ya dhulma , serikali ifanye jambo kuhusu vibarua wa viwanda wananyanyasika sana.