Naombeni ushauri: Nataka kumzuia mama yangu asiolewe tena baada ya baba kufariki

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Kwa zaidi ni kwamba anahitaji mwenza wa kuzungumza nae na siyo kwa hayo unayofikiria.

Mara nyingi tunasahau kwamba vijana wanakuwa busy sana kwenye mashughuliko yao na mama au baba huachwa mwenyewe tu kijijini au hata mjini. Anakuwa mpweke sana.

Usiangalie mpango wa fedha tu kuwa ndiyo huyo mjamaa atafaidika, lakini socially atakuwa amempa kampani kubwa mama.

Angekuwa kijana hapo ndiyo ningekuwa na wasiwasi kwa kweli.
 
Shida ni huyo mzee anataka kitonga mwambie bi mkubwa wako kama anataka kuolewa aende akaishi kwa huyo mzee
 
Mku usimbanie mze uwezi jua aliwekaga nadhiri atamuwowa .Kuliko atembee na vijana wadogo mwacheni amalizie uzee.
 
Kiongoz pole Sana kwani kinakuumiza! Lakini ujue wazee pia huhitaji kufarijiana Kuna muda anahtaji hata ataniane na wajukuu mpelekeen wajukuu Mara kwa Mara vinginevyo mwacheni akae na mzee mwenzake
 
Miaka 68 ? angejikalia zake alee wajukuu tu, na kama ataolewa basi akaishi huko huko kwa mumewe, si kumleta mume home.
 
Sasa mkuu we unashauri kipi ?

maana naona umechanganua vyema sana hapa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu acha mama aolewe Kama uyo mzee atakuja kuishi hapo home saw, ishi nao tu Kama wazazi maana ukianza kumpangia bmkubwa maisha utakuwa unamkosea chakufanya toa msaada uliondani ya uwezo wako
Mkuu umechangia ki legend sana
 
Ana takiwa kuwa tumia Baba zake wakubwa kumzui huyo Baba wakambo kuja kuishi hapo kwao kama ana taka aondoke na Mke wake mtarajiwa wakaishi Burundi [emoji1][emoji1][emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angekuwa katokea Rostam Aziz naamin hasinge kataa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama ako nae itakuwa ni mswahili sana miaka 68 anataka aoelewe ili iwejee???? POLE SANA kuna wamama wakifikaga 40 tu mume wake akifariki na ana watoto bhasi majukumu yanabaki inakuwa ndio ndoa yake wanaume wenyeww hao mwisho wa siku wampe maradhi alafu anaongeza mzigo usiokua na maana kwenye familia.
 
Hapo kwenye kuolewa hapana tatizo ila anatakiwa mzee achukue mkewake kama amempenda
 
Mara paap,,,mama anapiga simu 'babaenu mgonjwa hoi huku njooni mumchukue'.
 
Mama yako hana heshima hata kidogo, mzee vile kweli? Mmewe hata hajaoza kashawaza kuolewa? Hapana usikubali hayo mambo kama anataka kuolewa aende kwa huyo mzee na sio mzee aje kwenu.

Baba yangu alifariki akiwa na miaka 30, alimuacha mama akiwa mbichi just miaka 25 trust me mama hakuolewa alitulea na kutusomesha mpaka sasa ni tumekuwa wazima hatukuwahi kumuona mwanaume ndani kwetu .

Mama alikuwa mdogo ana shape matata mrefu, miguu mizuri, yaani kwa ufupi alikuwa mwanamke haswaa lakini hayo yote ya tamaa aliweka chini akajiheshimu na anaheshimika pale nyumbani.

Nilimuuliza kwa nini mama hukuolewa na ulikuwa bado mdogo? Akaniambia baba yenu alinipa maisha mazuri, kuanzia kuvaa, kula kila kitu niliwazidi wanawake wa kijiji hiki.sikuona mwanaume wa kumlinganisha na baba yako.mali aliniachia, watoto aliniachia niolewe kutafuta nini?

Mpaka sasa mama yangu ana nmiaka 50 hatujawahi kuona dalili yeyote ya kuwa na mahusiano, na alitulea kila mara akitusema kuwa tusome na tumpe heshima maana alibaki kwa ajili yetu.

Kijijini kwetu kila mtu umtolea mama mfano linapotokea swala mme wa fulani kafa mke kaolewa ,utasikia wakisema hivi nyie hamumuoni mama luckyline?

Mkuu usikubali ongeoa na mama yako mwambie kama hataki kuja kwako mjini, basi aolewe aende kwa huyo mzee.

Mama yako atawaletea shida, kesho na kesho kutwa mungu kamchukua mama yenu huyo mzee atagomea kwenye hiyo nyumba, mtaanza kuangaika mahakamani, usiruhusu huo ujinga kutokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…