Naombeni ushauri: Nataka kumzuia mama yangu asiolewe tena baada ya baba kufariki

Naombeni ushauri: Nataka kumzuia mama yangu asiolewe tena baada ya baba kufariki

Kama anataka kuolewa muache aolewe lakini hapo kwenu ahame
 
Mama yako hana heshima hata kidogo, mzee vile kweli? Mmewe hata hajaoza kashawaza kuolewa? Hapana usikubali hayo mambo kama anataka kuolewa aende kwa huyo mzee na sio mzee aje kwenu.
Mama yako ni mfano wa kuigwa. Baba yako alipata mke haswa! Yaani alibahatika kupata wife material mwenyewe(kama vijana wa sasa wanavyosema). Heko kwake!
 
Binafsi naona miezi 8 baada ya mzee kufariki ni michache sana. Angesubiri hata miaka 2. Pili huyo mzee kuishi kwa mama sio kabisa kwa mtazamo wangu. Mzee angejipanga awe na mji wake ndio amvute mama yenu. Siwezi hudumia huyo mdingi asilani. Ni haki yake mama kuwa na mahusiano maana mnampa vinono na vinamchangamsha. La msingi azingatie hayo
 
Binafsi naona miezi 8 baada ya mzee kufariki ni michache sana. Angesubiri hata miaka 2. Pili huyo mzee kuishi kwa mama sio kabisa kwa mtazamo wangu. Mzee angejipanga awe na mji wake ndio amvute mama yenu. Siwezi hudumia huyo mdingi asilani. Ni haki yake mama kuwa na mahusiano maana mnampa vinono na vinamchangamsha. La msingi azingatie hayo
Ukute mzee alikuwa anakulagaaa toka kitambo haiwezi kuwa ghafla hivi aiseee... Wapo wamama wabichi kabisa age ya 35 hivi huwaga inapita hata miaka kabla ya kuweka wazi wenza wao wapya yani huyu mama khaaa ananipa wasiwasi
 
Cha muhimu Mama akiolewa ahame kwenye mji Wa Baba yenu ahamie kwenye mji Wa huyo Mzee anayemuoa..

Vinginevyo huyo Mzee ana agenda yake nyingine dhidi ya huo Mji wenu.

Nadhani kama kuna Wazee Wa Ukoo hili suala watakusaidia kulisimamia vyema..

Koo nyingi haziwezi kukubali Mwanaume aoe Mke Wa marehemu Ndugu yao kisha ahamie kwenye Mji Wa Marehemu.. Na wengi ikitokea Mwanamke aliyefiwa na mume akaolewa basi wanamuondoa kwenye Familia yao, wanakuwa hawamtambui tena kama shemeji (Mwali) wao..
 
Ni rahisi sana kuchangia, na kushauri omba usikutane na kadhia ya mzazi asiye na busara mbele ya watotinwake, inaumiza sana, utaanza kufikiria toka mbali labda ili zee.lilikuwa linamuibia baba.

Siku nyingi, sasa kama kuoa kwa.nini.asiwe.resposible.kumbeba mke.wake kumpeleka kwake au kumpangishia.nyumba? Hata hivyo kuna.baadhi ya makabila mwanamke huwa hakubali kuzeeka
Kweli mkuu,kadhia yamzazi asiyejiheshimu inaumiza moyo Sana,nashukuru nashukuru mamayangu mzazi sio MTU wahovyo,nikweli kuna makibila Akina mama hawakubali kuzeeka,wanahitaji company mwanzo mwisho
 
68 anaolewa iweje tena
Duu mie maza ni wa 58 baba akafariki 12 so maza akiwa na 54 Ila sijawahi sikia Mambo Kama hayo.namie ndo nakomaa na maza nimemfanyia Kama ulivyomfanyia kumtunza Ila haiwezekani Kama anachepuka achepuke ni mwili wake
 
Habari ndugu zangu. Naombeni ushauri wenu juu ya mada tajwa.

Mzee wetu amefariki miezi 8 iliyopita baada ya maisha yake yote kuwa katika ndoa na mama yetu. Mama Sasa ana umri wa miaka 68. Kwa kipindi
Shida yako baada ya kifo cha baba yenu unachukulia mama yenu ameshakuwa Malaika hana hisia tena za kibinadamu.

Usiingilie maisha binafsi ya mama yako. Angekuwa dada yako unaweza kataa au kumpangia nani anamfaa ila sio mama.
 
Habari ndugu zangu. Naombeni ushauri wenu juu ya mada tajwa.

Mzee wetu amefariki miezi 8 iliyopita baada ya maisha yake yote kuwa katika ndoa na mama yetu. Mama Sasa ana umri wa miaka 68. Kwa kipindi chote tangu sisi watoto wake tuanze kujitegemea tumekuwa tukijitahidi kuwawekea mazingira mazuri ya wazee wetu.

Pamoja na kuwajengea nyumba yenye hadhi na ya kisasa lakini tumehakikisha wazee wetu wanaishi maisha standard kuanzia chakula na mahitaji yote kiasi kwamba familia ya mzee wetu imetazamwa kama familia yenye nafuu pale kijijini.

Juzi ndugu zangu waliopo kijijni wamenitaarifu kwamba kajitokeza mzee anasema anataka kumuoa bi mkubwa. Nikauliza akishamuoa ataondokanae kwa maana bi mkubwa atahama mji tuliomjengea na mzee? Wakaniambia hapana inavyoonyesha huyu mzee kafuata maisha mseleleko.

Binafsi nimejiuliza je ni sahihi mama alete mwanaume kwenye kitanda alicholala na mzee wetu? Je ni kweli nyumba tuliowajengea wazee wetu mama atumie kuishi na mzee mwingine? Alifanyalo mama sio kutufedhehesha sisi watoto tunaohakikisha anapatiwa chochote akitakacho?

Uamuzi wangu nimepanga kuvuruga mpango wa bi mkubwa. Nataka nimwite nimuombe nije niishi nae mjini kwa maisha yake yote ili nizuie mipango yake na akikataa nimepanga sitomuhudumia chochote maana Mimi ndie mwanawe mpendwa.

Je, ndugu uamuzi wangu huu nitakuwa namkosea mama yangu? Au nimwachie tu ahangaike na maisha yake? Kinachoumiza mzee muoaji mwenyewe kachoka mno hata ndala anazovaa ukute zina matundu nusu anagusa ardhi nusu malapa.

Naona kama bi mkubwa atatuongezea mzigo wa kuangalia watu wawili kwa maana akibaki mwenyewe inakuwa rahisi hata kumchukua wakati wowote. Ushauri wenu
Bro hujasema nyie ni dini gani,ushauri wangu hebu nenda kadhauriane na viongozi wa dini yenu utapata ufumbuzi mzuri sana

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Ndugu zetu wa kiislam ndiyo mifumo Yao Mama ata akiwa na watoto wakubwa na wajukuu bado atataka kuolewa na kuolewa mara nyingi nyingi wao Wana penda na kuachika mara nyingi napo Wana penda

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili siyo la dini ni pendekezo la mtu binafsi. Nitakupa mfano wa wazungu wakristo kama Elizabeth Taylor aliolewa mara 8 mpaka amezeeka bado anaendelea kuolewa. Mwingine ni Zsa Zsa Gabor naye aliolewa kama mara 8 au tisa. Mifano hiyo ni kwa vile wao walikuwa waigizaji maarufu lakini naamini wako wengi ambao siyo maarufu wanaendelea na maisha yao ya kuolewa na kuachika.
 
Angalia furaha ya mama MKUU.. achana na hayo mengine
 
Kumzuia huwezi na wala sio haki, yeye kama.binadamu anataka mtu wa kuwa nae na kumfariji....kuhusu nyumba na mali huenda hata sio kinanchompa raha au amani mama, kwahiyo muhimu mkae mzungumze kuwa mali za mzee zitabaki kuwa za familia yaani mama na nyie watoto hata wakioana na huyo baba wa kufikia.
Bora lipi awe na ma boyfriend au aolewe?

Kuishi na wewe pia sio suluhisho, fikiria maisha yako yote uishi mahali halafu mwishoni uhamishowe mji mpya, unakuwa mgeni huna marafiki wala jamaa, sio poa.
 
68 siyo lazima kuolewa na wala siyo muhimu. Ila usipazimushe. Jaribu kutumia wazee wa hekima wa Rika la mama washauri.
 
Bado najifunza. Ili uelewe hili lazima ujifunze kwa Walio na rika la Mama. Huduma usikate kwa Mama, Unaweza kuta wakati wote umekuwa ukihudimia mama na Huyu baba ( Mpenzi wa mama). Wenda wameshalala kitanda cha Baba mara nyingi tu. Unafikiri Marehemu Baba apendi Mama apate faraja. ?
 
Back
Top Bottom