Naombeni ushauri ndugu zangu napitia kipindi kigumu mno.

Ay_sher

Member
Joined
Oct 24, 2024
Posts
17
Reaction score
40
Habari za wakati huu,
Waswahili husema penye wengi pana mengi.
Naombeni mnisaidie katika hili ndugu zangu, Hapa nilipo sina kazi wala hata mtaji wa kufanya chochote sina, napambana lakini naona hali bado si nzuri, kinacho nipa mawazo ni kwamba nina mdogo wangu wa kidato cha nne bado hajaripoti shule mpaka sasa kwa kukosa karo, Na kumpeleka shule ya serikali ni ngumu mnoo tofauti na wanafunzi wa primary wanaoweza toka private wakarudi serikalini.
Ada ni 800k kwa mwaka yaani 200k per term plus baadhi ya michango ya form four kama laki moja na kadhaa hivi lakini imeshindikana! Yaani mpaka najiona nna msongo wa mawazo sana na Shule hawataki kumpokea na mambo ya usajili nahisi yapo njiani. Tumeshirikisha ndugu lakini hatuja fanikiwa,
Naombeni mnisaidie mwenye chochote walau ushauri yaani sioni pa kuanzia aisee!
Natanguliza shukrani zangu.
 
Hawa wanaofungua ID mpya ili waombe pesa, au kuleta shida hizi mjihadhari nao sana.

Ni wazoefu huku/humu JF, pia wanayafahamu mapungufu ya wana JF.

Kuna watu wamelizwa humu kama hamjifunzi basi tuwe na kumbukumbu.
 
Habari za wakati huu,
Waswahili husema penye wengi pana mengi.
Naombeni mnisaidie katika hili ndugu zangu, Hapa nilipo sina kazi wala hata mtaji wa kufanya chochote sina, napambana lakini naona hali bado si nzuri, kinacho nipa mawazo ni kwamba nina mdogo wangu wa kidato cha nne bado hajaripoti shule mpaka sasa kwa kukosa karo, Na kumpeleka shule ya serikali ni ngumu mnoo tofauti na wanafunzi wa primary wanaoweza toka private wakarudi serikalini.
Ada ni 800k kwa mwaka yaani 200k per term plus baadhi ya michango ya form four kama laki moja na kadhaa hivi lakini imeshindikana! Yaani mpaka najiona nna msongo wa mawazo sana na Shule hawataki kumpokea na mambo ya usajili nahisi yapo njiani. Tumeshirikisha ndugu lakini hatuja fanikiwa,
Naombeni mnisaidie mwenye chochote walau ushauri yaani sioni pa kuanzia aisee!
Natanguliza shukrani zangu.
Una jinsia gani?
 
Uza baadhi ya vitu mlivyonavyo umlipie dogo shule. Bakisha hata 50k uanze na biashara ndogondogo.
 
Back
Top Bottom