Naombeni Ushauri nimedisco chuo tangu mwaka wa pili na nyumbani wanajua naendelea na masomo na huu ndiyo mwaka wa mwisho

Naunga mkono hoja👏👏
 
Hela unatumiwa unakula tu bila kujiongeza.
Akili iliyofeli masomo inafeli vipi hata kujiongeza kujiingiza kwenye uwinga...

Kosa kubwa umefanya hapo.

Laiti ungejiingiza kwenye business then ukitusua ndipo ungekuja kufunguka.

Hapo ungekuwa umejihakikishia point 3 tena za mezani mbele ya familia, kwa sababu hakuna anayechukia maendeleo. Tena hapa ungeanza kwa kuwaomba msamaha then ukawaambia hela waliyokuwa wanakutumia ulifanyia hivi na matokeo yake ndio haya.
 
Tukushauri nini sasa..wee endelea na maandalizi ya graduation!
 
Hayo mengine ni yake hapa ameomba ushauri tu..
 
Hayo mengine ni yake hapa ameomba ushauri tu..
Hapo unambania kupata ushauri wa kumfaa,hapo anaweza kutokea mtaalamu akakuambia hizo ni dalili za ugonjwa wa akili ,sasa wewe unamwekea wigo,kama nae karidhia poa.
 
Katika maisha nilijifunza kwamba hautakiwi kuyaficha matatizo kwa wale ambao wanaotakiwa kukusaidia hasa ndugu.
 
Waambie ume carry somo /masomo mawili inabidi ukariri mwaka.
 
"Bahati Mbaya Sana,,Uongo Mara Zote Huwaga Haudumu".
 
Umeomba ushauri too late. Ungefunguka since ulipoyaona matokeo ningekupa ABC maana na mimi yalinikuta kama hayo miaka 5 ilopita, niliweka mazingira flan hadi leo hakuna aliyeelewa ukweli n upi, and sikuwa na wazo la kuhangaika na mfumo wa Elimu tena.

Now niko zangu kitaa. Maisha yanaenda poa tu kwa namna nyngne
 
Ukweli utakuweka huru, waambie ukweli ndg zako.
Vyuo na TCU wekeni utaratibu wa Wazazi au Walezi kuwa na access ya kuona progress za watoto wao wawapo vyuoni, vijana wanazidi kuwa wa hovyo.
 
Waambie wazazi au walezi wako ukweli ili wasiendelee kuharibu pesa kukutumia wakati husomi.Ukweli humweka mtu kuwa huru
 
Njoo geto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…