Gemini Are Forever
JF-Expert Member
- Sep 10, 2019
- 1,598
- 2,905
Habari wanajukwaa,
Nipo kwenye eneo ambalo maji ni changamoto kubwa sana, tatizo kubwa ni kwamba maji yanayopatikana hapa ni ya chumvi (hayafai kunywa moja kwa moja, pengine hata kuoga wala kufulia).
Kutokana na hali hiyo, nimekuwa na wazo la kuanzisha huduma ya kusafisha maji kwa kutumia teknolojia ya Reverse Osmosis (RO) kisha kuyauza kwa wakazi wa eneo hili kwa mfumo wa madumu (20L, 10L nk).
Lengo langu ni kutatua changamoto hii ya maji salama kwa wakazi, huku pia nikiwa nimejiajiri kupitia huduma hii.
Kwa sasa bado sijaanza chochote, sina uelewa mkubwa kuhusu vifaa, gharama za awali, upatikanaji wa mashine sahihi, wala taratibu za kitaalamu. Ndiyo maana nimeona niwashirikishe ninyi nipate:
-Ushauri kuhusu hatua sahihi za kuanzia
-Aina bora za mitambo ya RO kwa mazingira ya vijijini au miji midogo
-Changamoto zinazoweza kujitokeza
-Mawazo mengine yatakayosaidia kuboresha hili wazo kabla sijaanza
Nitashukuru sana kwa ushauri wowote kutoka kwa yeyote aliye na uzoefu, maarifa au hata maoni ya ziada.
Ahsanteni sana.