💧 Mpangilio wa Mfumo wa RO – Lita 2,000 kwa Siku
1. Vichujio vya Awali (Pre-filtration)
- Sediment filter: Huondoa mchanga na uchafu mkubwa.
- Activated Carbon (AC): Huondoa harufu, klorini, na uchafu wa kemikali.
- Wound Filter: Huchuja chembechembe nyepesi kabla ya kuingia kwenye membrane ya RO.
2. Booster Pump
- Hupandisha shinikizo la maji kutoka kwenye chanzo hadi kwenye membrane ya RO. Kawaida inahitaji shinikizo la 8–12 bar kwa ajili ya membrane 4″.
3. Membrane ya RO (4″ TFC)
- Moja ya membrane 4″ x 40″ inatoa takriban 1,500–2,000L kwa siku, kulingana na ubora wa maji ya chanzo.
- Maji safi (permeate) yatatoka kwa membrane na kuingia kwenye tanki la kuhifadhia.
4. UV Purifier
- Husaidia kuua bakteria na vijidudu kwenye maji safi baada ya kupita kwenye membrane.
5. Tanki la Maji Safi
- Hifadhi maji safi kwa matumizi. Inapaswa kuwa na uwezo wa kuhifadhi angalau 1,500–2,000L ili kufanikisha matumizi ya kila siku.
6. Utupaji wa Maji Taka (Brine)
- Maji yaliyosalia kutoka kwenye membrane (brine) hutupwa au kutumika kwa matumizi mengine yasiyo ya kunywa kama umwagiliaji.
📍 Mzunguko wa Maji (Flow Layout)
Maji ya feed → Sediment filter → AC filter → Wound filter → Booster pump → Membrane RO → post AC filter &UV → Tanki la Maji Safi
↓
Maji Taka (Brine)
💰 Makadirio ya Gharama ya Mfumo wa RO – Lita 2,000 kwa Siku
- Membrane ya RO (4″ x 40″): Tsh ~700,000/= inaweza kuwa zaidi ya moja kwa ufanisi zaidi
- Booster pump: Tsh ~180,000/=
- Vichujio (Sediment, Carbon, Wound): Tsh ~300,000/=
- UV Purifier: Tsh ~700,000/=( si lazima)
- Tanki la Maji Safi: Tsh ~500,000/=
- Installation & Accessories( fittings, valve, pipes na controller : Tsh ~500,000/=
- Gharama nyinginezo kama umeme, solar , Sehemu ambapo mfumo utafungwa nk
Jumla ya Gharama: Tsh -2800000/=
Note: Hii ni rough estimation kulingana na uzoefu.
🧾 Matengenezo na warrant
- Vichujio: Badilisha kila miezi 2–6.
- Membrane: Badilisha kila mwaka 2–3 (kutegemea na ubora wa maji ya feed).
- UV sterilizer : Badilisha kila mwaka.
Hii ni mifumo ya kawaida inayotumika kwa kiwango kidogo cha uzalishaji kama hiki (lita 2,000 kwa siku). Ikiwa unahitaji mfumo mkubwa au wa kisasa zaidi, unaweza kubadilisha baadhi ya vifaa au kuongeza sehemu zingine ili kuongeza ufanisi.
Wasiliana nami 0758404554.
Tuchambue zaidi.