Naombeni ushauri wa Biashara ya vitenge kutoka Zambia

Upo sahihi ofisini wanakaa na kikosi cha fast track kipo doria vitenge dakika yeyote unapoteza hela huyo mwenye Vitenge alikuwepo aliona wacha wavichukue atawafata baadae kuliko kuanza kumkamata na yeye atoe hela harafu aje atoe hela ya mzigo tena..
 
Umtafute chama kabla msimu wa ligi kuu kuanza atakupa full details atakuunganisha na watu wake we unapokea tu mzigo tunduma
 
Mkuu pale TV zipo nyingi 55 inch zinauzwa usd 200 na kuendelea ingawaje zipo za pungufu ya hapo kutokana na model yake hizo ni Sumsung..
Huwa sielewi kwa nini nchi zinazotuzunguka bidhaa bei ziko chini? Kwetu tatizo ni nini?

Maana hata Uganda bei kitonga shida ipo Mtukula.
 
Pole sana bwana yohimbe..[emoji1][emoji1]
Ndio wabongo walio wengi walivyo,roho za kwanini na za kichawi, ndio mana maskin ni wengi , na matajir wachache,
Actually nilishakumbwa na kadhia kama hio, dogo ni tajiri kweli kweli mpakani kule , ila ndio akaingia mitini
 
Ahsante mkuu, pole pia.
 
Ulifanya kosa kubwa sana hapa mkuu..
Wema wako umekuponza, biashara inatakiwa mkubaliane na mfaidike wote wawili, ungempa conditions zako, ungemuambia akutumie hizo sample wewe , ndio wewe kwa muda wako ungewatafuta wateja ukiwapata na wakipenda sample, unamwambia pisi kdhaa zinaitajika mkubaliane kabisaa mwanzon, tuma mzigo nakutumia hela au unaenda kufata mwenyewe na pesa, vyovyote vile ungefanya, alimrad tu mpate faida wote, ila kwa wabongo wa saiv asilimia 10 tu anawwza kukuonesha anapochukulia mzigo au akakupa mzigo uuze kwwa wteja wako umpe hela yake na hapo kwenye kuuza ukaweka cha juu upate faida..unatakiwa kucheza na akili za watu wapumbavu wenye tabia hio ya kibinafsi
 
Yule jamaa ana roho mbaya tuu kwanza hajawahi kuniambia anachukulia wapi huko zambia bado hataki niende alitaka awe ananiagizia yeye, kingine aliniambia nitafute wateja yeye ndio aongee nao so nilifanya basi tuu lakini nilikua nishajua ni mtu wa namna gani.
 
Aisee ni noma.
 
Huwa sielewi kwa nini nchi zinazotuzunguka bidhaa bei ziko chini? Kwetu tatizo ni nini?

Maana hata Uganda bei kitonga shida ipo Mtukula.
Sisi tuna kodi kubwa bidhaa zinatoka sehemu moja kwa hiyo Nchi yetu ina kodi kubwa sana hata magari Uganda yapo bei ndogo pamoja na Parts zake zipo Nchi bidhaa za watoto chini ya miaka minne hawatozi kodi kwa hiyo wanauza bei ndogo sana na hii 18% VAT ni kubwa kulinganisha na hizo Nchi..
 
Hakuna biashara tamu kama za magendo ila kikubwa ni kuroga na kuwa mbabe tu na mwisho pesa iwepo mkononi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…