Naombeni ushauri wa chaguo sahihi kati ya haya

Mkuu unaona nyingi..100k natuma kwa wazee,200k nalipa rent,300k usafiri job,vocha na kula kazini,100k kusaidia ndugu na michango ya hapa na pale nabaki na 300k nasave au kipindi kile sina vitu vya ndani nanunua so sio nyingi
Kwa huu mchanganuo inaonekana una matumizi mabaya sana ya pesa yaani usafiri tu pekee yake unatumia elfu kumi kwa siku!

Na hta io kodi ya nyumba bado ni kubwa sana ukizingatia mnachanga wote

Ushauri wangu tafuta sehemu ambao decent ya hta laki na nusu, usafiri wa kwenda kazini panda daladala halafu pia acha kujifanya msamaria mwema kumsaidia kila mtu we bado kijana jikite kwenye kutengeneza future yako coz miaka saba ijayo itakuwa ni majuto kwako kwa kushindwa kuitumia vizuri fursa ulionayo sasa.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Wewe nunua kiwanja badala ya gari
 
Acha upumbavu
Uishi maisha ya kujionyesha kisa?
Ishi maisha yako ww
 
Nunua pikipiki ya kijanja achana na boxer izi nunua 250 au zenye cc kuanzia 200 nakwambia wataanza kukuazia wao wenyewe nakuona walifanya mistek Mimi wenzangu walinicheka mmoja ana crown mwingine wish mwingine Nissan' duals saivi kila week end nikiwa home wanapishana kuomba funguo
 
Huu unaitwa ugonjwa wa 'Keeping up with the Jonenes' na unatuathiri vijana wengi.

Hata mimi nimekutana na similar scenario ya kutaka kununua Beamer ya almost 50m ili niwe sawa na vijana wenzangu wa Forex Ontario na Elikanafx ila nikafikiria na kuona haina maana kwa sababu mimi si wa mizunguko mingi plus tayari naishi sehemu ambayo yote nayohitaji yako karibu karibu.

Kilichonisaidia ni kufikiria 20 years ahead. Ni nadra kumkuta kijana alieishi maisha makubwa in 20s akawa anafanya hivyo hivyo in 40s na kuendelea. Its more wise kuwekeza katika kipindi hiki kuliko kufanya matumizi ya kushinikizwa.

Fanya tathmini angalia wapi unaweza kuizalisha pesa yako ikawa zaidi. Na usidhani kuwa kuna mtu anakufikiria kihivyo. Kila mtu ana shida zake katika maisha ambazo ni muhimu kuliko wewe kuwa na gari.
 
Mwezi wa kumi na mwingine mwezi wa 12
Asa hapo kwa mtiririko huo wa mwezi wa 10, mwingine wa 12, mwingine wa 1, na mwingine wa mwisho mwezi wa 2 inaonesha dhahiri kuwa hao jamaa zako wameigana na kwa maana hiyo upeo wa akili zao ni wa kiwango kimoja kwa sababu si kweli watu wanne mkawa na uhitaji wa gari katika kipindi kilichokaribiana kama hivo.
Bila kukuvunjia heshima wewe ndo chongo katika vipofu kwa kusita kwako na kuja kuomba ushauri huku JF.
Kuna ule msemo unasema "if u are the best in your group then it's time to leave" kwa maana ya kwamba haifai kuzungukwa na marafiki ambao wote umewazidi upeo na hivyo basi inabidi uvunje nao urafiki na kutafuta marafiki waliokuzidi upeo ambao wataenda kukupa changamoto na kukuvuta kwenda juu zaidi kimafanikio.
Na kumbuka "growth requires separation" kwahiyo usihofu kuhusu kuwapoteza hao jamaa zako ni sehemu tu ya safari ya kufikia mafaniko.
 
Naomba nije PM mkuu.
 
Nyeto inasave sana life
 
Bro sio poa…Ni rahisi kusema.Wote asubuhi wanaondoka na ndinga zao mimi nachukua boda kweli?
Ndo uwezo wako ulipo.

Haya maisha usije ukashindana hata mara moja.

There will alqays be somebody better than you.

Cha kufanya kaza buti piga mishe ufanye vitu vya maana zaidi. Chukua kiwanja lipa kwa installments za kila mwezi.
 
Sku waite weka hennessy wale tigo ukiwarekod utaifurahia maisha
 
Acha Ukolo Jenga Nyumba Duniani Hakuna Baba Mwenye Gari
 
nunua pikipiki mpya hlf hiyo hela inayobaki kanunue uwanja zen uanze kujenga usipende maisha ya kushindana na vigari vya mkopo
 
Ununue Gari Kisa Wenzako Wanayo?
Mnashindana Kwenye Maisha
Tengeneza Maisha Yako
Ila Wewe Unaonekana Chawa Sana Ndiyo Shida Yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…