Naombeni ushauri wa haraka: Ndoa mwezi mmoja, mimba miezi miwili

Naombeni ushauri wa haraka: Ndoa mwezi mmoja, mimba miezi miwili

Simply hakuna kipimo kinachoweza kusema exactly umri wa mimba zaidi ultrasound inakadria tu afu pia dr atauliza mara ya mwisho period lini, Sasa hilo na kusema mimba ina mwezi na week tatu linahitaji evidance beyond dought .Busara inahitajika kufanya maamuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa, ahsante
 
acha kuwadanganya watu sasa apo kuna kipimo gan cha uvumilivu yaan ugongewe then ulete maswala ya uvumilivu aseeeeee

Sent using Jamii Forums mobile app
Anaweza kuwa hajagongewa, labda kakutana na kanesi ka field kameambiwa mara ya mwisho kuona hedhi kakakurupuka, kama wameoana na sku iyoiyo ama baada ya sku mbili akapata mimba je? Wakianzia na sku ameona sku zake huo muda si unafika???
 
Haya Mambo Mengi Sana Kama US & IRAN
Meza Ya Duara Ni Muhimu Sana
Vinginevyo Aibu Kwa Watu Wote
 
sikuwa na ufahamu huu, nitaunganisha baadae....lakini anasema walitumia ultra sound
Hata ultrasound wasomaji wanakuwa km wanabashiri, sa zingine kiumbe anakuwa mdoogo kuliko umri wa mimba au kakubwa kuliko umri wa mimba ndo maana ata anayekuwa anapiga anauliza uliza mara ya mwisho kupata hedhi ili aunganishe na picha yake 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Mkuu kuna mambo hayahitaji ushauri mbona! Uyo mwanamke kaliwa pembeni kama anataka kulea bao la mtu sawa lakini kama hayupo tayari basi amuache huyo mwanamke kiroho safi.

Kwanza, ajiridhishe beyond reasonable doubts.

Anyways.

Kila mtu ashinde mechi zake!
 
Mshauri akapime sehemu nyingine tofauti maana si kila mtu anaweza kusoma utra sound,kuna ndugu yangu alifanya kipimo cha utra sound akaambiwa amebeba mtoto mmoja lakini akajifungua mapacha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ondoa kimoja kwenye maelezo yako, kati ya neno Zahanati ama Ultra sound ili habari yako iwe na ukweli kidogo.


Sent from my iPhone using JamiiForums
oh, nimeyanukuu tu maelezo....inawezekana limechanganywa hilo neno 'zahanati' lkn hakuna utungaji kwenye hii hoja mkuu
 
Kwa sehemu kubwa hiyo mimba ni yake. Umri wa mimba huhesabiwa kuanzia tarehe ya mwisho kuona siku zake mwanamke. Na sio siku aliyolala na mume.

Suala la pili ni kuwa, kama walitumia ultrasound, nayo pia huweza kuwa mbele ya muda au nyuma ya muda. Asimsingizie uzinzi binti wa watu. Kama ànaona sio wake, asubiri azaliwe na kisha mtoto akikua ataambiwa baba yako aliwahi kukukataa ukiwa tumboni.

Pia, humu watu hawana hata ndoa wala hawana uzoefu mambo ya uzazi lkn wamekimbilia kutoa ushauri! Mnaweza vunja ndoa, kama huna weledi wa suala fulani sio lazima kuweka comment.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom