Kinumbo
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 3,039
- 5,560
Habari zenu wapambanaji
Leo niko mbele yenu kutaka ushauri wa kimawazo kutoka kwenu ndugu zangu. Niko kwenye mpango wa kuingia kwenye kilimo kwa kumanisha hasa. Nina bajeti ya kiasi cha Tsh. 5M, hivyo kutokana na hicho kiasi niko mbele yenu kutaka ushauri wa mawazo kwa haya yafuatayo.
Nahitaji kufanya kilimo biashara na pia nahitaji ku dili na mazao ya biashara, hivyo naomba ushauri ni fanye hasa kilimo cha zao/mazao gani? Swali langu kuu ni hilo, nataka ushauri kutokana na nchi yetu Tanzania ni mazao gani ya biashara ambayo nikifanya ni hot cake. Nafahamu watu wanafanya kilimo cha Mahindi, Mpunga, Maharage, Nyanya nakadhalika. Binafsi nilihitaji ni komae na zao moja la biashara hivyo naomba ushauri wenu kwenye hilo.
Pia napenda kufahamu ni wapi ndani ya Tanzania hii zao husika linakubali kutokana na hali ya hewa, mfano ukiniambia fanya kilimo cha mpunga ningependa kujua ni wapi zao hilo niende kufanya ambapo unaona linakubali zaidi. Kutokana na kiasi changu napenda kuanza na heka tatu, nimedhamilia kuingia kwenye kilimo kwa msimu huu.
Natanguliza shukrani za dhati kwenu nyote, niko hapa nasubiri ushauri wenu. Ushauri wenu nitauzingatia kwa kina, asanteni sana.
Karibu.