Naombeni ushauri wana jamii juu ya uhusiano nilionao kwa mpenzi wangu

Naombeni ushauri wana jamii juu ya uhusiano nilionao kwa mpenzi wangu

Kwa sababu moyo wangu ulishafanya maamuzi sahihi ya kukuoa wewe as my super wife sioni sababu ya kuendelea kusubiria mmakonde wa mtwara, kifupi wewe watosha my wife 😘
Kama utaweza mambo ya sasa unaingia Tarime nijuze 😹🙌🏾
 
Kama utaweza mambo ya sasa unaingia Tarime nijuze 😹🙌🏾
Hilo kwangu sio tatizo kabisa as I told you before, moyo wangu ulishakupenda na akili na moyo vyote vimekuwa na ushirikiano wa asilimia 💯 katika kufanya maamuzi sahihi kabisa juu yako mke wangu mpenzi.

In short, hata ungesema upo ulaya au upo kaunti ya nyeri au kisumu nipo tayari mke wangu mpenzi ❣️ 😘
 
Hilo kwangu sio tatizo kabisa as I told you before, moyo wangu ulishakupenda na akili na moyo vyote vimekuwa na ushirikiano wa asilimia 💯 katika kufanya maamuzi sahihi kabisa juu yako mke wangu mpenzi.

In short, hata ungesema upo ulaya au upo kaunti ya nyeri au kisumu nipo tayari mke wangu mpenzi ❣️ 😘
Aya njoo sasa💔
 
Wewe ni tatizo sana.
Miaka 8 kwenye uchumba umeshindwa kumpa mimba.
Alafu huna maamuzi ya kiume manaake Ata ulichokuja kuomba ushauri hueleweki unataka kushauriwa Nini?
Muache Binti wa watu akaolewe na mwanaume acha kumzibia ridhiki
Hahaha
 
Miaka nane ulikua unataka kugundua nini na hapa unataka tukushauri nini
 
Nina msichana niko kwenye uhusiano nae yapata mwaka wa8 sasa, lakini kwenye maisha ya uhusiano kamili ni miaka6, wa 7 na wa8 imeikuwa ni miaka ambayo changamoto,misukosuko,kugombana na kufikia hatua ya kuvunja kwa uhusiano.

Shida ilianzia pale ambapo ameniona mm siendi kumchumbia kwao hpo ndo ugomvi umeanzia, nimeanza kum'bembeleza juu y hlo tangia 2024 na nikamwbia nipo tayr kuja, nkiwa nimeandaa safari ya kwenda kwao akaniomba pesa ya mtaji wa biashara (150k) na nimmnunulie smartphone ya (200k) nikamjibu sina pesa kwani najiandaa kuja kwenu na mpaka kumalizika kwa taratibu za awali za posa ni wastani wa(200k)+naul nend rudi (100k).

Ebwan hapo ndio ukawa mwanzo rasmi wa yeye kuniambia simfai,hataki kuwa na mimi tena niendelee na maisha yangu mengine, hataki nifike kwao kutoa posa nisijisumbue. Nimebembeleza takribani mwaka mzima lakini hataki. Sasa nami nimemjibu kuwa nipo tayari kuachana nae.

Chaa ajabu ananilaumu,ananitumia sms kupitia mitandao ya kijamii(DM) ananiambia nimemkosea sana. sijui nifanyeje maana nishamkubalia tuachane lakini bado ananitfuta sana
Pole kwa changamoto
Kwani mna umri gani?maana i can tell dada maturity bado..afterall wanawake hawajuagi nini wanataka so mwanaume ukisimama vizuri utamsaidia kujitambua.Hebu mkae muongee na wewe ujue nini unataka kwa mke
 
nimeanza kum'bembeleza juu y hlo tangia 2024 na nikamwbia nipo tayr kuja,
Ulikuwa unabembeleza nini kijana, tambua ndoa sio kitu cha kubembeleza. Ni makubaliano ya watu wawili walio tayari kuunganisha hisia zao na kuishi pamoja.

Kosa lako la kwanza ni KUBEMBELEZA. Usirudie.
akaniomba pesa ya mtaji wa biashara (150k) na nimmnunulie smartphone ya (200k)
Naona kipato chenu sio kikubwa sana. Haya, anataka mtaji wa 150K na Smartfone ya 200K. Je anataka kufanya biashara ya mtandaoni?

1. Ikiwa ni hapana, huyo bado hajitambui achana nae.
2. Kwanini akuwekee masharti ya kabla ya kwenda kujitambulisha kwao umfanyie vitu hivyo? Huyo sidhani kama utadumu nae kwenye ndoa

ndio ukawa mwanzo rasmi wa yeye kuniambia simfai,hataki kuwa na mimi tena niendelee na maisha yangu mengine, hataki nifike kwao
Hivi ni vionjo tu anakupa. Kwa ujumla wake hilo ndio jibu sahihi, HAUMFAI. HATAKI KUWA NA WEWE.

Endelea kubembeleza moto utakuwakia zaidi ukishakuwa nao karibu, utalipata joto halisi. Uchumba tu hivyo, mke inakuwaje.
Nimebembeleza takribani mwaka mzima lakini hataki. Sasa nami nimemjibu kuwa nipo tayari kuachana nae.
Bado tu unaendelea kubembeleza mwaka mzima, mwanamke kakwambia Haufai, haulewi? Baadae uje kuanza kutusumbua na ushauri wa mke kakunyima tendo, kakufokea nk.

Unajibu upo tayari kuachana nae wakati yeye alishakuacha. Si ukae kimya.

Wanaume ukitaka kumwacha mwanamke unatimka kimyakimya ili yeye ndio ajue kuwa amekuacha kumbe umeona hakufai. Pita zako kimya mpotezee.

KAA KIMYA, UNAJIBU NINI SASA WAKATI ULISHAACHWA KITAMBO. USIWE BOYA KIJANA WANGU.
Chaa ajabu ananilaumu,ananitumia sms kupitia mitandao ya kijamii(DM) ananiambia nimemkosea sana
Keshaona anakumudu anaweza kufanya chochote anachojisikia kukwambia. Akiandika sms lazima ujibu. Jifunze kupotezea sms na simu zake, kuwa mwanaume.
sijui nifanyeje maana nishamkubalia tuachane lakini bado ananitfuta sana
Endelea kubembeleza mpaka ifike miaka 10, karne moja.

Tumbaf kabisa unatuaibisha wanaume, yaani mpaka hapa bado hujajua nini unatakiwa kufanya?

Si kila mwamamke ana sifa ya kuwa mke.
 
Mpo kwenye uhusiano ambao haujui unahusiana na nini...
 
Mapenzi hayashauriki! Ila mahusiano ya miaka 8 si ni kama ndoa tu
 
Back
Top Bottom