nimeanza kum'bembeleza juu y hlo tangia 2024 na nikamwbia nipo tayr kuja,
Ulikuwa unabembeleza nini kijana, tambua ndoa sio kitu cha kubembeleza. Ni makubaliano ya watu wawili walio tayari kuunganisha hisia zao na kuishi pamoja.
Kosa lako la kwanza ni KUBEMBELEZA. Usirudie.
akaniomba pesa ya mtaji wa biashara (150k) na nimmnunulie smartphone ya (200k)
Naona kipato chenu sio kikubwa sana. Haya, anataka mtaji wa 150K na Smartfone ya 200K. Je anataka kufanya biashara ya mtandaoni?
1. Ikiwa ni hapana, huyo bado hajitambui achana nae.
2. Kwanini akuwekee masharti ya kabla ya kwenda kujitambulisha kwao umfanyie vitu hivyo? Huyo sidhani kama utadumu nae kwenye ndoa
ndio ukawa mwanzo rasmi wa yeye kuniambia simfai,hataki kuwa na mimi tena niendelee na maisha yangu mengine, hataki nifike kwao
Hivi ni vionjo tu anakupa. Kwa ujumla wake hilo ndio jibu sahihi, HAUMFAI. HATAKI KUWA NA WEWE.
Endelea kubembeleza moto utakuwakia zaidi ukishakuwa nao karibu, utalipata joto halisi. Uchumba tu hivyo, mke inakuwaje.
Nimebembeleza takribani mwaka mzima lakini hataki. Sasa nami nimemjibu kuwa nipo tayari kuachana nae.
Bado tu unaendelea kubembeleza mwaka mzima, mwanamke kakwambia Haufai, haulewi? Baadae uje kuanza kutusumbua na ushauri wa mke kakunyima tendo, kakufokea nk.
Unajibu upo tayari kuachana nae wakati yeye alishakuacha. Si ukae kimya.
Wanaume ukitaka kumwacha mwanamke unatimka kimyakimya ili yeye ndio ajue kuwa amekuacha kumbe umeona hakufai. Pita zako kimya mpotezee.
KAA KIMYA, UNAJIBU NINI SASA WAKATI ULISHAACHWA KITAMBO. USIWE BOYA KIJANA WANGU.
Chaa ajabu ananilaumu,ananitumia sms kupitia mitandao ya kijamii(DM) ananiambia nimemkosea sana
Keshaona anakumudu anaweza kufanya chochote anachojisikia kukwambia. Akiandika sms lazima ujibu. Jifunze kupotezea sms na simu zake, kuwa mwanaume.
sijui nifanyeje maana nishamkubalia tuachane lakini bado ananitfuta sana
Endelea kubembeleza mpaka ifike miaka 10, karne moja.
Tumbaf kabisa unatuaibisha wanaume, yaani mpaka hapa bado hujajua nini unatakiwa kufanya?
Si kila mwamamke ana sifa ya kuwa mke.