Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 373
- 829
Naitwa James ni mwezi wa pili sasa tangu nihamie kwenye nyumba moja yenye wapangaji wengi maeneo ya Mwananyamala.
Kwenye nyumba hii tuko wapangaji watatu...wanawake wawili pamoja na mimi.
Mara nyingi mimi hurudi nyumbani usiku na wala sina mazoea na wapangaji wenzangu. Cha kushangza juzi usiku nimerudi nyumbani nikakuta mlangoni kwangu mfuko wa plastiki umefungwa vizuri...
kwanza nikaogopa kuufungua lakini nikajipa moyo nikauchukua nikaingia nao ndani na kuufungua.
Nilichokikikuta ndani kilinishangaza ni ndala nyeupe zenye michoro ya moyo (love) na kibarua kidogo kimendikwa...."Kaka samahani kama nimekukwaza nimekuona kila asubuhi ukienda chooni na ndala zilizochakaa sana nikaona nikununulie ndala hizo kama zawadi...samahani narudia tena kuomba msamaha kama nimekukwaza ni mimi Belinda jirani yako chumba cha kati.
Nakutakia usiku mwema." Baada ya kusoma kibarua hiko nimekuwa na mawazo sana na asubuhi yake niliwahi sana kuondoka ilimradi nisionane naye.
JM LIBRARY