Naombeni wenye kujua haya mambo, naona kama nina kitu Cha kipekee

Naombeni wenye kujua haya mambo, naona kama nina kitu Cha kipekee

Wajuzi wa mambo haya,

Naomba nirudi nyuma kidogo,nilikuwa mdogo bado nina kumbukumbu yapata miaka 29 nyuma,
Nilikuwa na uwezo wa kuona vitu au kitu kibaya,au kujua ni lini tutapata wageni na nilikuwa nikimwambia mama,

Mamangu ni mwana maombi sana na maombi yake juu yetu ni kama umetufunika na ulinzi Fulani maana alikuwa ananitamkia hata kipindi naenda kusoma mbali alikuwa akisema maneno Fulani kufika kule naona kama vile au nitapokelewa Fulani hivi shuleni na kupendwa sana na hata kipindi nakosa chakula pale shuleni kutokana na shule zetu za bweni mnafahamu kama huna nguvu utateseka sana,ila ilichukua miezi kadhaa,na nilikuwa natoroka na kwenda vijini vya karibu na nitapewa chakula huko na kurudi nikiwa safi,

Mamangu alikuwa na utaratibu wa kuleta wana maombi nyumbani kwetu na tulikuwa wale walokole kweli kweli.Hapo ndo niliposikia sauti kwenye ndoto kuwa mbona hutaki kuokoka na wewe piga Magoti uokoke,nikawa mgumu kidogo nikaona kama nguvu Ile ni kubwa nikalipuka pale Moja kwa Moja na kusema Nahitaji kuokoka na kupiga Magoti na kuongozwa maneno siku hiyo hiyo,

Baada ya hapo niliishi kwenye huo ulokole ila nilikuja kutereza kutokana na hizi shule zetu za mbali ,ila Kila nikipita karibu na kanisa,huwa nilikuwa naumia sana kwa nini Mimi sijaenda kanisani,hiyo hali na hiyo nguvu iliendelea kunitesa moyo hivyo,

Na kipindi nikianza kusoma biblia huwa najihisi nguvu Fulani hivi ya kuona vitu kwa watu wengine,

Na hii ndo inanitesa zaidi naweza kupanda daladala nikiwa kwenye mizunguko yangu au wakati wa kwenda kazini nikahisi mbele Kuna ajali na nikifika mbele naona ajali,imekuwa ikiniongoza hivyo ,au nitapanda gari konda asinidai au labda nikikumbuka Huwa Nampa au nisilipe,au naweza kula mgahawani na nikalipa ela na kurudishiwa chenji zaidi Kuna mda narudisha na Kuna mda nakuwa Sina ela nakaa kimya,

Pia naweza kumuona mtu nikamwambia ukweli juu ya jambo analopitia,na nimekuwa nikimwambia mwanamke ambaye nipo naye kwa harakati ya kutaka kumuoa na amekuwa akiniamini sana kutokana na Mimi kumwambia mambo ya familia yake na mpaka nimekuwa nikimwambia ukweli na hata kumwambia hujawahi kuingiliwa na mwanaume hapo ndo alibaki kuwa hoi nikaja kumwambia kuhusu mamake na wadogo zake na kaka yake,

Na hii jambo imekuwa nikijihisi kuwa Kuna nguvu Fulani nyuma yangu ,na hii ya kuona ajali imekuwa ikinisumbua sana maana nimekuwa najitahidi kuikemea sana lakini naona Bado,na kwa sasa naona hii nguvu inanituma sana kuwaombea wagonjwa maana nafanya kazi kwenye hospitali na hii nguvu inazidi kuwa kubwa.

Kuna rafiki yangu alinidhulumu ela zangu na kushirikiana na mchumba ambaye nilitaka kumuoa nilisema maneno machache tu juu Yao,walipata ajali mwendelezo na kupita wakati mgumu sana,na Bado wanaoitishwa kwenye moto huo huo ,

Naombeni kama Kuna watu wa mambo ya kiroho kuhusu mambo haya najiona wa tofauti sana
Kaka hiyo ni nguvu ya Mungu. Ingia instagram tafuta account inaitwa Anointed Room pale utaona mwongozo
 
Mungu anisaidie na kunitia nguvu katika hili,anaponitia nguvu nasimama na kuweza kwa jina lake ,maana ni mkuu wa mambo yote.

Na wakati hata kazini huwa nawaambia hata ndugu wa wagonjwa kuwa ndugu yenu mimba yake ni mtoto wa kiume au wakike naona kama kitu kinanisukuma na kumwambia amebeba mtoto wa aina hii,ila nawasihi sana asimwambie,

Ila wapo wajawazito wanasema huyu mtoto ananisumbua tumboni sijui atakuwa wa aina gani,na muuliza nikutabirie,anasema ndio na Mimi namuuliza unampenda wa aina gani ,namjibu Mungu akupe wa moyo wako

Mwingine anasema nimezaa wa kike sana,nwambie basi huyo ni wa kike au wa kiume na huwa nawafuatilie pale wodini na kuona haya maajabu
Na me naomba unieleze tafadhali kuhusu uzao na ajira
 
Hongera mkuu watu kama nyie mko wachache.. ambao mnaweza onyeshwa jambo kabla halijatokea... kuna mtu ambaye namfahamu yeye anaweza onyeshwa jambo kwenye ndoto kama ni kifo au ajali akimwambie muhusika basi halitatokea kwa ukubwa.. ila asipo mwambia linatokea kwa ukubwa.. hvy unapaswa kuomba sana mkuu. Ni karama hiyo.
 
Hahahaha Ila jf Raha Sana Yani, huwa najiuliza wasiojua hii platform Yani wanakosa mengi. Mkuu Rudi kwenye wokovu achana na ya kaisari hiyo itakuafanya uishi kwa amani na ufanye uvuvi was watu
 
Mungu anisaidie na kunitia nguvu katika hili,anaponitia nguvu nasimama na kuweza kwa jina lake ,maana ni mkuu wa mambo yote.

Na wakati hata kazini huwa nawaambia hata ndugu wa wagonjwa kuwa ndugu yenu mimba yake ni mtoto wa kiume au wakike naona kama kitu kinanisukuma na kumwambia amebeba mtoto wa aina hii,ila nawasihi sana asimwambie,

Ila wapo wajawazito wanasema huyu mtoto ananisumbua tumboni sijui atakuwa wa aina gani,na muuliza nikutabirie,anasema ndio na Mimi namuuliza unampenda wa aina gani ,namjibu Mungu akupe wa moyo wako

Mwingine anasema nimezaa wa kike sana,nwambie basi huyo ni wa kike au wa kiume na huwa nawafuatilie pale wodini na kuona haya maajabu
Omba sana,tafuta Uso wa Bwana!kaa vzr na Mungu!mbona utaona makubwa zaidi ya hayo,kutoa unabii ni sehemu ndogo sana Mungu amekuweka hapo makusudi anataka akutumie zaidi.

Hiki ni kipindi cha uamsho mkubwa kabla Yesu hajarudi, ss ww unaekutana sana na watu,wagonjwa,hebu usiache kuwaambia habari za wokovu! Na Mungu akutie nguvu tu,,utabibu na karama ya uponyaji,plus kuona ,Mungu ana makusudi yake kuweka ndani yako kwa sbb
Ili umsaidie mtu lzm uone tatizo ni nn kwanza!
Kwahiyo mpendwa tumia vzr hizo karama usiishiea kutoa unabii tu,waambie habari za Yesu!
Tupo nyakati za mwisho.hubiri wokovu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amen [emoji1666][emoji1666]
 
Back
Top Bottom