Naona Barabara ya Sam Nujoma maeneo Mlimani City imeanza kufumuliwa, ni BRT phase 5?

Tulisikia Jangwani wameshakopa saa yeyote wataanza kazi.
 
Wapuuzi tu, njia mbadala zote zimefungwa wanaingiza gharama sana kwa Watanzania. Maana inabid mtu aunge gari au matumiz makubwa ya mafuta. Pia kunachelewesha watu kwenda ktk shughul za kiuchumi.

Pia wafanyabiashara hasa bodaboda na wauza maduka wanathirika sana na hili vumbi.. imagine unauza nguo alaf nje wamechimbua vumbi la kutosha pia entrance imefungwa hakuna mteja anaeweza ku access kiurahisi hapo dukan kwako. Na hakuna dalili za kukamilika haraka, kodi unayolipa ipo pale pale.

Mie nashauri wangemalizana na hiyo ya Airport mfano pale Njia panda ya segerea gari si chini ya elf 5 kwa siku inabidi zizunguke umbali wa kilometer 5 ili kupata access ya kwenda Tabata. Just imagine ni kiasi gani cha mafuta kinateketea hapo.
 
Inashangaza sana, mradi wa Mbagala ungeanza, maana upo tayari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…