Uchaguzi 2020 Naona CHADEMA inavyokwenda kuishangaza Dunia

Uchaguzi 2020 Naona CHADEMA inavyokwenda kuishangaza Dunia

CCM, kwa msaada wa jeshi la polisi, TUME Dhaifu ya uchaguzi na mbinu zingine za hovyo kama za nguvu, ikiwamo vitisho kwa wananchi, rushwa na uongo wamekuwa wakibadirisha marais kwa msemo wa kupokezana vijiti.

Kuna ukweli fulani katika hilo, toka ameendoka madarakani mwalimu nyerere tumeona marais wote waliofuata kuondoa huyu wa sasa, wakielekeza uchumi wa nchi kwenye mikono ya sekta binafsi kutoka kwenye uchumi unaosimamiwa na serikali kkt misingi ya sera za ujamaa na kujitegemea.

Mpaka wakati Kikwete anaondoka madarakani, uchumi wa Tanzania ulikuwa mikoni mwa sekta binafsi kwa zaidi ya asilimia 75%, hizi 25% zinatokana na serikali kuendelea kuwa na mashirika kadhaa machache yaliyokuwa yakijiendesha kwa ushindani na makampuni binafsi, ushiriki wa serikali kwenye sekta ya elimu, afya, kilimo huku sekta binafsi iniendelea kujitanua kwa kasi sana katika sekta hizo kwa namna iliyokuwa ikiongeza tija zaidi.

Tungepata Rais, mwenye fikra bora zaidi ya waliotangulia, ambaye angejikita katika kukusanya kodi na kusimiamia sekta za kiuchumi badala ya kuwa mshiriki na mshindanrkuwa mbali zaidi kiuchumi, lakini kilichojitokeza ni kwamba ukuaji wa sekta binafsi ni kama umezuiwa, kwa fikra zilizopitwa na wakati na zisizo na mashiko hata katika uchumi wa kimataifa.
 
Back
Top Bottom