GE2025 Naona dalili ya watu wengi kutojitokeza kesho. Je, Mgombea asipopata 50% itakuwaje?

GE2025 Naona dalili ya watu wengi kutojitokeza kesho. Je, Mgombea asipopata 50% itakuwaje?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Sheria yetu ni ya aliyepata majority vote hata kama ni asilimia 20.

Pili hata ingekua asilimia 51 ni asilimia 51 ya waliojitokeza kupiga kura si ya waliojiandikisha.
Uongo unachukiza

Uchaguzi uliopita wa 2020 waliopiga kura walikua ni 49% ya waliojiandikisha
Uchaguzi wa 2010 waliopiga kura ilikua ni 43% ya waliojiandikisha

Idadi ya waliojiandikisha na wataopiga kura haina uhusiano kwenye kumpata mshindi.
 
Sheria mama ya taifa letu inasemaje?

Sheria ya uchaguzi inasemaje?

Maana kuna dalili ya 30% ya wapiga kura kujitokeza.
Tanzania ni first past the post so hata ukipata 30% ila wagombea wengine below that unatangazwa tu.
 
Waliofuatilia kampeni mikutanoni ni 25M
Waliofutilia mtandaoni ni 164M hii ni ndani na nje ya nchi.
Wapo waliofuatilia redioni na kwenye Radio na vyombo vingine kama nanhii na nanhii.
Hawezi kupata chini ya % 50 sio rahisi. Sema anawezapata 99+++
 
Yale malori yanamwaga watu kesho wakajaze vituo, vikijaa tuu hata kama watu wasipopiga kura idadi wataipika wanavyojua wao
 
Bongo hata kura 2 zinakupa mamlaka ya kuongoza nchi. Yani yako na mme wako au mke wako unaongoza nchi...
 
Dogo nimempa kazi ya kuchukua orodha ya ndugu wanaoenda kutiki. Baada ya hapo tusijuane. Shida zake apeleke ofisi za CCM
 
Nchi yetu haina mambo ya 50% hapa ni anayepata nyingi kumzidi mwenzake.

Hata wakipiga watu 100 atakayepata nyingi ni huyo huyo.
 
Back
Top Bottom