Babu Kijiwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2010
- 4,830
- 4,729
Zipo sababu nyingi ambazo ningeorodhesha zote huenda vidole vingeuma kwa ku type ila kwa leo nataka niwatajie sababu chache tu, kwanini naona fahari kuitwa kijana wa Lumumba.
jingalao
- Mgombea wangu anaendelea kutandika reli yakisasa SGR, hivi mmeona lile jengo la stesheni makao makuu Dar, lile lenye umbo la Tanzanite? Mmeona mahandaki? Mmeona usanifu na ubunifu wapekee ktk mradi huu? Haya yote yanafanya nijivunie kuitwa kijana wa Lumumba.
- Mgombea wangu kaboresha bandari ya Dar es Salaam, Mtwara na Tanga, tembelea bandari hizi ujionee mambo makubwa yanayofanyika utapiga saluti.
- Mgombea wangu kajenga Mfugale na Ubungo Interchange. Mmewahi kupita pale na magari yenu? Mlijisikiaje? Ni mambo aliyofanya mgombea wangu.
- Mgombea wangu kajenga vituo vya Afya, Zahanati, Hospitali za Wilaya, Mikoa, Rufaa na Kanda, Kaboresha upatikanaji wa huduma za Afya, kudadadeki zunguka nchi nzima utaniambia mwenyewe.
- Mgombea wangu kakata mirija ya ufisadi, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka kwa waliofanya hivyo, sasahivi ukienda ofisi yoyote ya Umma ukikaa nje unaweza fuatwa na mkurugenzi akiomba kukusikiliza. Saluti kwako mgombea wangu.
- Mgombea wangu kasambaza umeme na sasa vimesalia vijiji elfu 3 tu Tanzania nzima kuwaka umeme, utaniambia nini?
- Mgombea wangu kajenga miradi mikubwa ya maji nchini tena ya kihistoria.
- Mgombea wangu kahamishia serikali Dodoma na jiji la Dodoma kwasasa limenoga, tafuta nauli uje Dodoma kujionea maajabu.
- Mgombea wangu kajenga network kubwa sana ya barabara nchini tena kwa kasi ya ajabu.
- Mgombea wangu kamalizia jengo la terminal 3 ktk Airport ya Mwalimu Nyerere. Lissu akija atajionea japo namhurumia kwakuwa hata hiyo nafasi ya kugombea wanamtosa na kumpa Membe.
- Mgombea wangu katandika masoko yakisasa kwenye miji 16 ya kimkakati, vituo vya mabasi ya abiria, sehemu za kupumzikia nk.
- Mgombea wangu kalipia cash kununua Madege 11 na 8 tayari yanapishana huku na huko ktk anga la Tanzania na anga la kimataifa. Kumbuka katoa cash, hatudaiwi na mtu ndo maana kuna nyakati anatoa bure kusaidia Watanzania maana hakuna anaye tudai.
- Mgombea wangu anajenga bwawa la kuzalisha umeme Megawatt 2100 baada ya kukamilisha, bei ya umeme itashuka sana.
- Mgombea wangu kanunua rada 4 mpya na kutuhakikishia usalama wa anga letu.
- Mgombea wetu kaondoa kero kwa wajasiriamali wadogo, nimevaa kitambulisho changu hapa nauza mikate yangu saaafi stand ya mabasi ya mikoani hakuna anaye niuliza ushuru, nasomesha, nimejenga makazi yangu, nafurahia kuitwa kijana wa Lumumba.
- Mgombea wangu kakomesha ujangili, wanyama sasa wanazaliana kwa raha zao, hadi wengine imebidi wapelekwe Dodoma na kwenye hifadhi ya Burigi Chato.
- Mgombea wangu kapanua viwanja vya ndege na amesha tangaza tenda ya kujenga bonge la uwanja jijini Dodoma.
- Mgombea wangu katatua migogoro ya wakulima na wafugaji iliyopelekea mauaji huko Morogoro na Manyara.
- Mgombea wangu kaanza mradi wa majaribio kusambaza huduma ya Gas majumbani huko Mtwara ktk eneo la Railway
- Mgombea wangu karekebisha mikataba ya hovyo na wawekezaji ktk sekta za madini, mawasiliano nk
- Mgombea wangu ameidhibiti Corona kwa uwezo wa Mungu
- Mgombea wangu kanunua Meli mpya na kufanya ukarabati wa meli zilizokuwa zimechoka.
- Mgombea wangu kajenga uzio kuzunguka eneo lenye madini ya Tanzanite matokeo yake Laizer kavunja rekodi ya Dunia.
- Timu ya taifa imefika AFCON na Samatta anacheza ligi kuu ya Uingereza
- Treni sasa inafika Kilimanjaro na Arusha wataiona soon
- Elimu bure, maboresho ya shule za vipaji maalumu na vyuo vikuu
- Mikopo ya elimu ya juu
jingalao