Naona kama Wanawake wengi hawapiki chakula cha waume zao

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
2,406
Reaction score
8,039
Nikienda migahawani huwa naona wanaohudhuria kula kila siku migahawani ni wababa na vijana tena wenye ndoa zao, ni mara chache sana kukuta mdada anakula kila siku migahawani.

Mimi ni bachela, sasa sijajua faida ya ndoa ni nini, kama wanaume waliooa nao wanakula migahawani kila mara kama mimi.

Siamini kama population yote ya wanaume wanaokula mgahawani Kila siku hawana wake wa kuwapikia nyumbani, Explanation ninayoweza kuja nayo ni kuwa wake zao wanakataa kuwapikia.
 
Shida tunaiga kila kitu cha duniani tudai ni UTANDAWAZI ilihali wenzetu hawaigi vyetu, mbona Wachina hadi leo hii hawajaiga mtindo wa kuvaa suruali(jinsi) zilizochanika chanika kama vichaa?

Yani Ke avae chupi(bikini) iliyoacha matako nnje ili aonekane ni mjanja anayeenda na wakati nakati huo ni UTUNDUWAZI?

Mapenzi ya tamthilia za kifilipino waachie watoto wenyewe, sisi wahenga tunapikiwa na tunaendelea na mfumo dume kwa mila na desturi za kibantu.

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Mfano mke niko gongo la mboto Mume anafanya kazi mwenge ina maana chakula cha mchana nimpikie nimpelekeaa au aje yeye akili za namna gani hizi
Unataka kusema kwamba jioni/ usiku huwa huoni foleni ya wanaume migahawani! Kuna tatizo mahali na kama mtoa hoja anavyosema haiwezekani wote hao wakawa mabachela.
 
Duuh sasa kama mke anakusaidia majukumu yako ya kutafuta pesa na kulipia bills, wewe unashindwa nini kumsaidia na yeye majukumu yake au kutafuta housegirl.

Na huu ndiyo ubinafsi mkubwa ambao wanaume wengi wa kiafrika mnao, hiki kizazi sijui kinaelekea wapi aisee.

Yaani asubuhi mnatoka wote kwenda kazini then mnarudi usiku wote mmechoka, halafu unataka mkeo aingie jikoni afanye kila kitu peke yake wewe umekaa miguu juu.

Kama unaona hauwezi oa mwanamke ambaye hajasoma na hana kazi wala biashara yoyote ili umuweke ndani awe mama wa nyumbani tu, uwe unamhudumia kwa kila kitu hadi hela ya mafuta na kitana anakuomba wewe.

Yaani siku hizi ndoa imekuwa mwiba na mzigo kwa wanawake na ndiyo maana wengi wanaona bora wawe single mothers wazalishwe waachwe walee wenyewe tu, hata kama jamii itawasema wako tayari wavumilie kuliko kuolewa.

Kuwahudumia wake zenu hamtaki mnataka nao watafute hela eti siku hizi maisha kusaidiana, ila ninyi kuwasaidia majukumu yao mnaona taabu mnawaacha wapambane na hali zao halafu wakiwanyima unyumba kwa sababu ya uchovu mnalalamika,

Bora zamani tu ambapo wanaume hawakutaka haya mambo ya kusaidiana maisha, wanawake walikuwa wanashinda tu nyumbani wanapata muda wa kutekeleza majukumu yao huku wanaume ndiyo wanatafuta kwa ajili ya wake na watoto,

Ila siku hizi mtu anataka mtafute wote na bado majukumu yako utimize kikamilifu anashindwa hata kujiongeza kukusaidia, mwisho wa siku mwanamke ndiyo anajikuta ana majukumu mengi kuliko mwanaume wakati mwanaume ni kiongozi na mwanamke ni msaidizi tu.
 
Shida tunaiga kila kitu cha duniani tudai ni UTANDAWAZI ilihali wenzetu hawaigi vyetu, mbona Wachina hadi leo hii hawajaiga mtindo wa kuvaa suruali(jinsi) zilizochanika chanika kama vichaa?

Yani Ke avae chupi(bikini) iliyoacha matako nnje ili aonekane ni mjanja anayeenda na wakati nakati huo ni UTUNDUWAZI?

Mapenzi ya tamthilia za kifilipino waachie watoto wenyewe, sisi wahenga tunapikiwa na tunaendelea na mfumo dume kwa mila na desturi za kibantu.

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
I hope huyo mkeo bado unamhudumia na hakusaidii majukumu yako ya kutafuta pesa
 
Nikienda migahawani huwa naona wanaohudhuria kula kila siku migahawani ni wababa na vijana tena wenye ndoa zao, ni mara chache sana kukuta mdada anakula kila siku migahawani.

Mimi ni bachela, sasa sijajua faida ya ndoa ni nini, kama wanaume waliooa nao wanakula migahawani kila mara kama mimi.

Siamini kama population yote ya wanaume wanaokula mgahawani Kila siku hawana wake wa kuwapikia nyumbani, Explanation ninayoweza kuja nayo ni kuwa wake zao wanakataa kuwapikia.
Nani alisema kwamba ukioa mke wako lazima akupikie au wewe umpikie?
 
Kuna sababu tofauti ila mi naona hizi
1.Kuna wababa wachoyo wao wanakula migahawani vizuri utakuta anakula supu ya kuku na mipochopocho kibao nyumbani ugali kachumbari na hagusi.
2.Wanaume wengi kazi zetu ni za kutwa nzima hivyo tunashindwa kwenda kula nyumbani so Asubuhi na Mchana tunakula migahawani.
3.Wapo ambao hawajaoa na hawajui kupika ama wavivu.
4.Kuna wanaokula migahawani kwa sababu ya nyumbani anapikiwa hovyo au wana ugomvi na mkewe
5.Mazoea..mfano brother wangu hata akishindaga home huwa hawezi kunywa chai ya nyumbani kwake na akijitahidi basi chai tupu.

Ongezea zingine.
 
I hope huyo mkeo bado unamhudumia na hakusaidii majukumu yako ya kutafuta pesa
Imeandikwa;

Mwamke atazaa kwq uchungu na Mwanaume atakula kwa jasho, yani "Asiyefanya kazi na asile"

Mke anafanya kazi za nyumbani tu, kunizalia watoto na kuwalea.

Hadithi za vijiweni eti "tafuta Mwanamke anayefanya kazi ili msaidiane maisha" hatimaye unaoa kazi badala ya Mke mwema ni uwoga wa maisha na undezi.

Wangapi wameoa Wanawake wenye kazi ilihali wamekuwa na migogoro tela na maisha ya kawaida kiuchumi?

Mafanikio ni juhudi binafsi zikiambatana na baraka za Mungu la sivyo unawezajikuta unafukuza upepo kwa kujitutumua kwa akili zako na bidii za kazi lakini usifanikiwe popote kimaendeleo.

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
KUA UYAONE
Nikienda migahawani huwa naona wanaohudhuria kula kila siku migahawani ni wababa na vijana tena wenye ndoa zao, ni mara chache sana kukuta mdada anakula kila siku migahawani.

Mimi ni bachela, sasa sijajua faida ya ndoa ni nini, kama wanaume waliooa nao wanakula migahawani kila mara kama mimi.

Siamini kama population yote ya wanaume wanaokula mgahawani Kila siku hawana wake wa kuwapikia nyumbani, Explanation ninayoweza kuja nayo ni kuwa wake zao wanakataa kuwapikia.
 
Duuh sasa kama mke anakusaidia majukumu yako ya kutafuta pesa na kulipia bills, wewe unashindwa nini kumsaidia na yeye majukumu yake au kutafuta housegirl.

Na huu ndiyo ubinafsi mkubwa ambao wanaume wengi wa kiafrika mnao, hiki kizazi sijui kinaelekea wapi aisee.

Yaani asubuhi mnatoka wote kwenda kazini then mnarudi usiku wote mmechoka, halafu unataka mkeo aingie jikoni afanye kila kitu peke yake wewe umekaa miguu juu.

Kama unaona hauwezi oa mwanamke ambaye hajasoma na hana kazi wala biashara yoyote ili umuweke ndani awe mama wa nyumbani tu, uwe unamhudumia kwa kila kitu hadi hela ya mafuta na kitana anakuomba wewe.

Yaani siku hizi ndoa imekuwa mwiba na mzigo kwa wanawake na ndiyo maana wengi wanaona bora wawe single mothers wazalishwe waachwe walee wenyewe tu, hata kama jamii itawasema wako tayari wavumilie kuliko kuolewa.

Kuwahudumia wake zenu hamtaki mnataka nao watafute hela eti siku hizi maisha kusaidiana, ila ninyi kuwasaidia majukumu yao mnaona taabu mnawaacha wapambane na hali zao halafu wakiwanyima unyumba kwa sababu ya uchovu mnalalamika,

Bora zamani tu ambapo wanaume hawakutaka haya mambo ya kusaidiana maisha, wanawake walikuwa wanashinda tu nyumbani wanapata muda wa kutekeleza majukumu yao huku wanaume ndiyo wanatafuta kwa ajili ya wake na watoto,

Ila siku hizi mtu anataka mtafute wote na bado majukumu yako utimize kikamilifu anashindwa hata kujiongeza kukusaidia, mwisho wa siku mwanamke ndiyo anajikuta ana majukumu mengi kuliko mwanaume wakati mwanaume ni kiongozi na mwanamke ni msaidizi tu.
Kuna mwanamke mmoja namfahamu, ni ndugu yangu na ni mama tu wa nyumbani, hachangii chochote kwenye kipato cha familia, mme wake anafanya kazi Nzuri ya kuendesha scania za kupeleka mizigo nchi jirani, na Kipesa mume anahudumia familia vizuri tu, lakini kazi ya kupika msosi wa mume, mara nyingi, asilimia 90% anaachiwaga housegirl, hapo unasemaje, Raha ya mke anipikie bhana Karma
 
Duuh sasa kama mke anakusaidia majukumu yako ya kutafuta pesa na kulipia bills, wewe unashindwa nini kumsaidia na yeye majukumu yake au kutafuta housegirl.

Na huu ndiyo ubinafsi mkubwa ambao wanaume wengi wa kiafrika mnao, hiki kizazi sijui kinaelekea wapi aisee.

Yaani asubuhi mnatoka wote kwenda kazini then mnarudi usiku wote mmechoka, halafu unataka mkeo aingie jikoni afanye kila kitu peke yake wewe umekaa miguu juu.

Kama unaona hauwezi oa mwanamke ambaye hajasoma na hana kazi wala biashara yoyote ili umuweke ndani awe mama wa nyumbani tu, uwe unamhudumia kwa kila kitu hadi hela ya mafuta na kitana anakuomba wewe.

Yaani siku hizi ndoa imekuwa mwiba na mzigo kwa wanawake na ndiyo maana wengi wanaona bora wawe single mothers wazalishwe waachwe walee wenyewe tu, hata kama jamii itawasema wako tayari wavumilie kuliko kuolewa.

Kuwahudumia wake zenu hamtaki mnataka nao watafute hela eti siku hizi maisha kusaidiana, ila ninyi kuwasaidia majukumu yao mnaona taabu mnawaacha wapambane na hali zao halafu wakiwanyima unyumba kwa sababu ya uchovu mnalalamika,

Bora zamani tu ambapo wanaume hawakutaka haya mambo ya kusaidiana maisha, wanawake walikuwa wanashinda tu nyumbani wanapata muda wa kutekeleza majukumu yao huku wanaume ndiyo wanatafuta kwa ajili ya wake na watoto,

Ila siku hizi mtu anataka mtafute wote na bado majukumu yako utimize kikamilifu anashindwa hata kujiongeza kukusaidia, mwisho wa siku mwanamke ndiyo anajikuta ana majukumu mengi kuliko mwanaume wakati mwanaume ni kiongozi na mwanamke ni msaidizi tu.

Acha kupotosha na kupenda kitonga.
 
Mfano mke niko Gongo la mboto Mume anafanya kazi Mwenge ina maana chakula cha mchana nimpikie nimpelekeaa au aje yeye akili za namna gani hizi
Mnaishi wote au kila mmoja anaish kivyake,,,?? swala la kula mchana mgahawan iko sawa,, veep kuhusu night imekaaje hapo,,,

Sent from my SH-02J using JamiiForums mobile app
 
1.Hamna kitu kizuri kama kula chakula kilichopikwa na mke wako.

2.Hamna kizuri kama kula pamoja hasa chakula cha jioni kwenye meza moja, mume, mke na watoto. Hiki kitu kizuri sana kinajenga umoja na uimara wa familia,kinamsaidia hata mzazi kujua yanayo endelea kwenye familia na watoto wako, japo siku hizi watoto walio wengi wananyimwa nafasi hii na wazazi wao kila mtu yupo busy ,kutoka 12 asubuhi kurudi 4 usiku watoto washalala,weekend ikifika wanaenda kushinda bar na marafiki zao.

Nisiwe mwongo mimi moja ya vigezo vyangu mwanamke nitakaye muoa lazime ajue kupika na lazima katika wiki, basi siku tano lazima tule mlo wa jioni kwenye meza moja na watoto FULL STOP ,ubeijing,hawa 50/50 naomba Mungu wanipitie pembeni kabisa.
 
Back
Top Bottom