Naona nikienda kuwa academician, nimechoka ajira kwenye private sector

Naona nikienda kuwa academician, nimechoka ajira kwenye private sector

Mikhail Tal

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2016
Posts
421
Reaction score
778
Kiukweli wakuu, mimi ni mmoja wa watu ambao kwa sasa nazipigania hizi ajira za u tutorial assistant kwa kiu kubwa sana.

Ni kwamba nipo kwenye private sector lakini ki uhalisia kabisa baada ya kujitafakari, nimeona endapo nitabaki huku nilipo kwa sasa, sio tu kwamba uchumi wangu utadumaa ila kwa level ya stress nahisi naweza pia nisiishi a quality life ambayo naiota.

Option nnayoichukua ya tutorial assistant itakuwa na mshahara pungufu mara mbili ya unaopata sasa ila kiukweli naona kama ubora wa maisha utakuwa mkubwa.

Halafu kingine ni kwamba, hizi nchi zetu miaka 15 wataokuja kuifaidi ni wasomi kwahiyo nimeoa nichukue huu mrengo wa kuwa academician ili hii miaka 5 au 7 inayokuja nihakikishe napata kabisa na PhD.

Nimekaa chini ninefikiria nimegundua hapa nilipo inawezekana nacheza makidamakida. Watu wapo kwenye academic wanakula good time sana aisee, kuna research, consultation zinawaingizia hela ndefu sana.. Halafu pia free time kibao.

Kuna jamaa aliweka uzi hapa kuhusu uzuri wa kazi za U tutorial na u assistant lecturer watu wengi wakamdharau.. ila kwa kweli naomba nimuunge mkono. Sisi tulio kwenye sekta binafsi kama mshahara wako ni chini ya milioni 7 kwa mwezi wewe jua bado unaishi maisha ya chini sana kulinganisha academician. Ukitaka kuligundua hilo, angalia maisha ya academician wengi na vitu wanavomiliki. Na ndio sababu ni mara chache sana mtu akishaingia kuwa academician akaacha akaenda kufanya ajira nyingine ila nimeshuhudia mara nyingi watu wakiacha kazi mpaka benki kuu na kwenda kuwa academician.

Utumishi naombeni sana mfanye mambo fasta fasta.. nimeomba nafasi nyingi sana najua lazima ntaambulia japo moja, nimechoka kupelekeshwa na vilaza huku kwenye private sector.
 
Daa yaani mtu Ni muhasibu Kwenye UN agencies analipwa 6m, na allowance Kama zote, umlinganishe,na muhasibu wa Tamisemi anayelipwa laki 7
Hapo mkataba miaka mitano baada ya hapo anarudi benchi kusugua matako ajira yake sio ya kudumu

Hapo hana cha mafao ya kustaafu

Amekalia kuti kavu mda wowote wanakuondoa inategemea mabosi wameamkaje

Huna uhuru
 
Mpaka moyo umedunda,private sector kumbe Kuna watu wanapokea million 7,na nimfanyakazi tu hayupo kwenye board may be,kumbe nipo mbali na dunia .
Haha amka mkuu private sector hasa kwenye NGOs za kimataifa Watu wanavuta mipunga mirefu na wametulia tu

Halafu motivational speakers wanatudanganya eti bongo kutoboa hadi uwe mfanyabiashara tu

Watu mnadhani bongo waajiriwa wote wana njaa
 
Back
Top Bottom