Mleta mada nadhani uendelee kufanya research yako vizuri hasa unapodhani ukiwa academician unakuwa free zaidi na workload inapungua. Workload ukiwa academician inaweza kuwa kubwa pengine kuliko hata huko kwenye NGOs unazosema. Lecturers wengi huwa wanakosa hata muda wa kujibu emails. Wakati mwingine wanajibu hata baada ya wiki kutokana na wingi wa majukumu yao. Wanafanyia kazi emails zilizo urgent tu na ambazo zipo kwenye circle ya mazingira yao ya kazi.
Sema utofauti wa huko kwenye NGO na kwenye U-lecturer ni kuwa;
i) Kwenye mazingira ya vyuo vikuu mambo mengi yanakuwa well organized na more cordinated. Kwahiyo unakuta mambo ni mengi ila yanaenda very systematic tofauti na ilivyo huko kwenye NGO
ii) Kwenye vyuo vikuu mostly una-work independently na pressure iliyopo ni kati yako na majukumu yaliyo mbele yako. Tofauti na huko kwenye NGO ambako, tofauti na workload kuwa kubwa, bado unakuwa na pressure za boss wako.
iii) Ukiwa chuo kikuu hasa vyuo vya serikali na ukafikia level ya kuwa lecturer unakuwa huru zaidi kufanya maamuzi ya kipi ufanye kwa wakati upi, unaweza hata kuahirisha kipindi ukaendelea na shughuli nyingine mfano kazi za research na ukakipanga hicho kipindi wakati mwingine na wanafunzi wako. Tofauti na kwenye NGO ambako huwezi jifanyia maamuzi mwenyewe bila kuwa ana consequences.
iv) Hata hivyo, haimanishi ya kuwa unakuwa huru jumla. Na kwenyewe kunakuwa na administrators kama wakuu wa idara, college n.k ambako unawajibika kwao.
Mambo mengine kama kupanda vyeo, kuongeza elimu, maslahi naomba nisigusie maana watu wengi wameyazungumzia huko juu.