Yani wanaume ninachoweza kuwashauri ni kwamba, kama mmeamua kutumia hiyo midoli tumieni kwa lengo la kujifurahisha wenyewe, na siyo kwa lengo la kuwakomoa wanawake kwamba wajirekebishe hicho kitu hakiwezekani
Wanawake wa sasa hawajali tena kuhusu ndoa wala familia ukilinganisha na wa zamani, na ndio maana siku hizi ni kawaida kusikia wakiambizana wazae tu walau wapate watoto wa kuja kuwalea uzeeni, wasihangaike na wanaume tena
Yani kama mnafanya hayo kwa kuwakomoa wanawake na kutegemea watabadilika, mtakuwa dissapointed sana pale ambapo mtashangaa ndio kwanza wanatafuta njia nyingine mbadala ya wao nao kujifurahisha, kuliko kuwabembeleza ninyi au kubadilika kwa ajili yenu
Hizi zama tulizofikia siyo tena zama za kumtishia mwanamke ndoa au kufanya ndoa kuwa fimbo ya kumchapia mwanamke, na zamani kilichokuwa kinawafanya wanawake wawe desperate na ndoa ni mitazamo tu ya jamii dhidi yao, kitu ambacho kwa sasa kimepungua
Ndio maana mnaona siku hizi idadi ya single mothers inaongezeka pamoja na kutukanwa kote lakini hawajali ndio kwanza wanazidi, maana zamani wengi walikuwa wanaogopa kuzaa na kutokuolewa sababu ya maneno ya jamii tu, lakini si kwamba walikuwa hawataki sasa imagine huko tunakoelekea
Sasa hivi wameamua kutia nta masikio wanafanya wanavyojisikia na hatimaye jamii nayo imepunguza zile stereotypes dhidi ya mwanamke, na taratibu zitaenda zitaisha maana sasa hivi dunia imebadilika watu wamesoma wana exposure za kila aina, na huko tunakoelekea ndio ndoa zinazidi kupoteza umuhimu wake
So kama mmeamua kuoa midoli ndugu zangu hakikisheni mnafanya hilo kwa dhati ya mioyo yenu na si kwa kubeep na kuwasikilizia wanawake hawa wa sasa na wa kesho eti kama watabadilika nawaambia mtashangazwa, vinginevyo endeleeni kusubiria hicho kipindi ambacho sijui wanawake saba watamfuata mwanaume mmoja awaoe, (kama ambavyo wayahudi bado wanasubiri masihi wao azaliwe) wakati ukweli uko clear kabisa tunakoelekea