Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Mohamedex121

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2022
Posts
1,725
Reaction score
3,271
Habarini wakuu! Ni mimi kijana wenu humu jamiiforums nina miaka 21, kama mnavyojuwa umri huu bado nipo masomoni chuo flani hivi apa dar na bado nipo home.

Sasa tuludi kwenye mada, unajua nini hapa home sipaelewi sikuhizi nimekuwa nikichukiwa pasipo na sababu za msingi, hasa bi mkubwa amekuwa mtu wakunifokea fokea hadi majirani huwa wanasikia jinsi ninavyofokewa. Majuzi kati hapa niliambiwa sikuhizi hapo home sifanyi kazi na ninachelewa kurudi nyumbani, nikiwauliza wazazi wangu ni kazi gani wanataka mimi nizifanye hapa nyumbani naambiwa nioshe vyombo, mara nifyeke majani na mikazi mengine kibao.

Okay siku na kipingamizi kwasababu hawa ni wazazi wangu hivo ni wajibu kuwasikiliza na sio kwamba siku za nyuma nilikuwa sifanyikazi? Hapana ni kutokana na majukumu ya masomo huku chuoni yananibana sana hivo nakuwa mtu sio wakushinda nyumbani maana mda wote na huku chuoni huwa na baki mpaka saa 3 au nne usiku ndio narudi home. Nafanya hivi ili nikimbie majukumu ya nyumbani ila baadae nahisi wazazi wangu walinishukizia.

Anyway sasa kila nikifanya kazi za hapa nyumba bado maneno yanakuwa mengi mara uwambie urudie kuosha vyombo mara mbili wakati apo vyombo ushaosha na vinan'gaa bila shida , ukitoka hapo mara uwambiwe chooni unaachafua mara hausafishi mara unaingiza mchanga mara uwambiwe uliacha mavi leo asubuhi yaani maneno yanakuwa mengi halafu bimkubwa anaongea kwasauti kubwa hadi majirani wanasikia

Mimi hali hii sipendezwi nayo, naona wazazi wangu kama wameanza kunichoka, hapa nafanya mpango mwisho wa mwezi huu nichomoke hapa home najua mwanzo wa kujitegemea huwa mgumu ila potelea mbali siwezi kuendelea kukaa home huku nikidharirishwa na maneno ya bimkubwa.

Anyway natafuta chumba bei iwe 50k maeneo kuanzia ubungo kibo, kona mpaka kimara korogwe. Kama unaona au unasikia kuna chumba kinapangishwa maeneo hayo anipange sasa. Wakuu #natanguliza shukuran
 
Pole sana kuna wazazi na walezi wengine huchangia kuharibu watoto manyanyaso yanakuwa mengi mm nishawahi ishi maisha kama hayo nilivumilia mpaka muda ulipofika nikaondoka
Acha tu hapa naishi na wazazi wangu tena wakunizaa ila naona manyanyaso yamekuwa mengi hapa nyumbani ngoja nichomoke mwisho wa mwezi huu
 
Mtoto Kwa wazazi hakui... Tena Kwa huo umri wako Bado unaonekana mtoto angalau ungekuwa na 25 wangekuchukulia mtu mzima.

So vitu ambavyo mzazi wako anaona ni kawaida kabisa kukwambia, wewe unachukulia manyanyaso Kwa kuwa Kwa umri huo wewe unajiona tayari ni mtu mzima na yawezekana pia baadhi ya kazi unaona ni za kike hupaswi kufanya.

Chagua njia utayochagua ila hakikisha ukihama hapo usiwaongezee majukumu, maana wazazi wengi wanatarajia ikifika umri Fulani basi majukumu Kwa watoto wao hasa wa kiume yanapungua.

Sio ukapange huko uanze kuomba pesa za chakula na mahitaji mengine home, unawaongezea Budget zinazoepukika.
 
Hapana mkuu unajua kuna maneno mzazi akiyaongea unajua kabisa hapa mzazi anakunyanyasa hivi kweli mimi na umri wangu huu niachae mavi chooni hebu mkuu think twice, sikuwahi kuambiwa hivi hapo nyuma. Na suala la kuanza kupanga chumba tayari nimeshaweka mipango yangu fresh nina akiba yangu ya boom kama 200k nahisi itanitosha kabisa kuanzia maisha
 
Duuh mi nina 20 lkn mbona hivyo vitu havipo kwangu 🤔
 
Back
Top Bottom