Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Kwa umri wako Wazazi wamekuonea. Kama una boom I think unaweza kuishi kwako.
Boom lipo mkuu nasubiria awamu hii ya pili mwezi huu nijumlishe na akiba I think itanitosha kabisa kuanza kujitegemea
 
Huyo maza Mnyaki nini/ Maana watu wa kule wana makoo makubwa akiongea bucha. msewe mnasikia [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
[emoji38][emoji38] acha tu mkuu yaani maza akiongea mtaa mzima utajuwa tu kuwa leo mudi hajaosha vyombo yaani hadi zarau madogo wanakuletea mtaani utasikia kaka mudi kaoshe vyombo
 
[emoji38][emoji38] acha tu mkuu yaani maza akiongea mtaa mzima utajuwa tu kuwa leo mudi hajaosha vyombo yaani hadi zarau madogo wanakuletea mtaani utasikia kaka mudi kaoshe vyombo
Kama una boom kapange mtaani, hata share geto na msela maisha yaende
 
Habarini wakuu! Ni mimi kijana wenu humu jamiiforums nina miaka 21, kama mnavyojuwa umri huu bado nipo masomoni chuo flani hivi apa dar na bado nipo home.

Sasa tuludi kwenye mada, unajua nini hapa home sipaelewi sikuhizi nimekuwa nikichukiwa pasipo na sababu za msingi, hasa bi mkubwa amekuwa mtu wakunifokea fokea hadi majirani huwa wanasikia jinsi ninavyofokewa. Majuzi kati hapa niliambiwa sikuhizi hapo home sifanyi kazi na ninachelewa kurudi nyumbani, nikiwauliza wazazi wangu ni kazi gani wanataka mimi nizifanye hapa nyumbani naambiwa nioshe vyombo, mara nifyeke majani na mikazi mengine kibao.

Okay siku na kipingamizi kwasababu hawa ni wazazi wangu hivo ni wajibu kuwasikiliza na sio kwamba siku za nyuma nilikuwa sifanyikazi? Hapana ni kutokana na majukumu ya masomo huku chuoni yananibana sana hivo nakuwa mtu sio wakushinda nyumbani maana mda wote na huku chuoni huwa na baki mpaka saa 3 au nne usiku ndio narudi home. Nafanya hivi ili nikimbie majukumu ya nyumbani ila baadae nahisi wazazi wangu walinishukizia.

Anyway sasa kila nikifanya kazi za hapa nyumba bado maneno yanakuwa mengi mara uwambie urudie kuosha vyombo mara mbili wakati apo vyombo ushaosha na vinan'gaa bila shida , ukitoka hapo mara uwambiwe chooni unaachafua mara hausafishi mara unaingiza mchanga mara uwambiwe uliacha mavi leo asubuhi yaani maneno yanakuwa mengi halafu bimkubwa anaongea kwasauti kubwa hadi majirani wanasikia

Mimi hali hii sipendezwi nayo, naona wazazi wangu kama wameanza kunichoka, hapa nafanya mpango mwisho wa mwezi huu nichomoke hapa home najua mwanzo wa kujitegemea huwa mgumu ila potelea mbali siwezi kuendelea kukaa home huku nikidharirishwa na maneno ya bimkubwa.

Anyway natafuta chumba bei iwe 50k maeneo kuanzia ubungo kibo, kona mpaka kimara korogwe. Kama unaona au unasikia kuna chumba kinapangishwa maeneo hayo anipange sasa. Wakuu #natanguliza shukuran
Yani umeona swala lako wewe na familia yako tena WAZAZI wako ndio litapatiwa suluhisho humu,acha akili za kijinga kijana huo ujana usikupeleke pupa hivyo,Mzazi ana wajibu wa kukuambia chochote ikiwa hakileti madhara kwako na sijaona sababu ya wewe kulalama humu kisa tu kuambiwa ufanye MAJUKUMU ya HAPO NYUMBANI,kabla haujawa na miaka mpaka leo wamepambana,wamekupigania vya kutosha mpaka sasa hapo ulipo,huna haja ya kulalama mtandaoni humu hakuna msaada mkuu.

Rudi tena kwa Mama kapige magoti kamuombe msamaha huwezi jua kuna kitu ulifanya ama yeye anahisi kuna kitu mbele huko utafanya ambacho si kizuri.Kama waliweza kugundua wakati wewe bado ni mtoto mdogo hujui kuongea,wewe ni KUCHEKA na KULIA pindi ukipata maradhi hata ya tumbo basi Mzazi anajua hata kama huja muambia.

Heshima iwafikie WAZAZI WETU WOTE haijalishi wametulea katika mazingira Gani.

Tatizo la vijana wa sasa tunapenda sana USASA maisha ya TV na MTANDAONI {GLOBALIZATION} angalia WAZAZI WETU pindi walivyokuwa na umri kama wako walikuwa wanapewa majukumu gani kwao kwa WAZAZI WAO.

AHSANTE.

Sent from my V2204 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom