Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Kwani amesema awaheshimu ?au wao ndio Wana msakama kila siku na kumfanya ashundwe kujiamini Hadi anambiwa kak mudi kaoshe vyombeee na nk .....
Dr vip ....
Sasa nyumbani yupo yeye na mama yake,anataka Nani amuoshee vyombo?
 
Ndugu yangu ndugu yangu.... nakuita tena Ndugu yangu! Usijaribu kuondoka hapo home kiholela hivyo utajuta sana.

Ki kawaida hauna shughul ya kukuingia kipato.

Maisha ya kujitegemea sio rahis kama unavyofikiri kuna watu walipanga na wana Kazi zao kbs ila mambo yaliwazidi wakarudi home (Kurudisha Mpira kwa Kipa)

Ni heri utukanwe na Wazazi kuliko na walimwengu..

Unayajua matusi ya FATHER HOUSE wewe?!
 
Comment bora kabisa...dogo anajiona kakua, anadanganywa na kadegree uchwara...aje kitaa sasa maji ataita mmaaa
Degree yenyewe bado hajaipata. Nimemwambia kama ataondoka home, atleast aondoke kwa wema. Akitumia hasira,hatoboi.

Manyanyaso ya home ni afadhali kuliko msoto wa kitaa ambao haujui.
 


"Nafanya hivi ili nikimbie majukumu ya nyumbani ila baadae nahisi wazazi wangu walinishukizia."

Huna adabu, nenda tu ukipata shida utakuwa na adabu kwa wazazi wako.
 
Wewe huja hustle bado,nimesoma historia ya utoto ya Magdalena Sakaya yule dada wa cuf aisee alihustle na alitii hadi akatoboa.Itafute imo humu humu jf
 
Sema wewe ndugu,maana Kuna watu wanamjaza ujinga.
 
Pole kaka, mimi nakushauri uendelee kukaza tu hapo home hadi umalize chuo (ni ngumu lakini komaa).
 
Sema wewe ndugu,maana Kuna watu wanamjaza ujinga.
Yeye anawaza kodi tu.

Kuna bills nyingi na liabilities kibao.

Kuna gharama za chakula etc

Kuna gharama za matibabu (Ukizingatia uliondoka home kwa mbwembwe) Wazaz watakuangalia tu.

Kuna gharama za Mavazi

Sio kila siku hela ipo.

Ukipanga kuna vishawishi vya ngono na starehe nyingi ambazo zinahitaji pesa.

Kupanga kutamuongezea stress nyingi zaidi, huwenda hata Chuo asifanye vzr.

Mimi nilipanga wakati nipo Chuo kuna muda nilishindia Uji wa sembe, na nyumbani chakula kipo hadi wanawapa Kuku.
 
Tukiwambia watu Kuna wazazi wanateza watoto wao Wana kataha


Mm mwenyewe nilioyapitia kwa kaka angu siwezi sahaugi nakikumbuka nalia kbsa

Ila SAS nimetuliaa nimekuwa kma adui SAS Sina hamu nae
Alikufanyaje brother yako ?
 
Tukiwambia watu Kuna wazazi wanateza watoto wao Wana kataha


Mm mwenyewe nilioyapitia kwa kaka angu siwezi sahaugi nakikumbuka nalia kbsa

Ila SAS nimetuliaa nimekuwa kma adui SAS Sina hamu nae
Pole sana na izi mambo ndiyo huchagiza mtoto kuharibika kisaikolojia.

Unakuta kijana muda wote ni mtu wa wasiwasi, mawazo na kupoteza hali ya kujiamini kwenye mambo yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…