Naondoka Bungeni bila Mume wangu, Naondoka na Aibu na Mikopo ya kutisha

Naondoka Bungeni bila Mume wangu, Naondoka na Aibu na Mikopo ya kutisha

Sasa uongozi si sifa na ujuzi unao anza na kuwaongoza wale wanaokuzunguka na yale yanayokuzunguka na kujiongoza weww pia. Mbona huku ustawi wa jamii tunashuhudia uongozi hauna hata jinsia? Yaani Me au Ke wote wanaweza na kuna wakati wote hawawezi tu. Kwani kama wanaume ndiyo wote wanaweza uongozi, inakuwaje tuna wababa wametelekeza watoto wao, wanabaka na kulawiti watoto wao, wanajaza mimba watoto wa shule, na wana jazba wanapiga watu tu hawana skills za mazungumzo na ndiyo wamejaa huko magereza? Unadhani huo ndiyo uongozi sasa? Na wakati wakifanya vurugu hizo mbona zigo aachiwa mama? Halafu mtoto akikua utaona wengine wanajirudisha na stori za ohhh mama fulani naona tumekuza mtoto nasikia yuko kidato cha 6? Acha fujo rafiki. Uongozi siyo miliki ya kijinsia
Natumaini wewe ni mkristo na unafaham tangu ngazi ya familia mwanaume ndiyo kichwa au kiongozi,hata lile lililokuwa taifa teule zamani hawakuwai kuwa na mkuu wa nchi mwanamke,haya ya leo ni kukengeuka tu Kwa binadam,ila kama ambavyo binadam hana uwezo wa kupaa angani ndivyo mwanamke pia hana uwezo wa kuongoza
 
Daktari asikuumize kichwa huyo mwananchi. Inawezekana anatokea Kwenye zile jamii ambazo hadi sasa haziamini katika usawa wa kijinsia na fursa sawa. Bado wanadhani dunia inazunguka katika muktadha wa vijiji vyao.
Kama wizara nadhani mna kazi kubwa sana ya kuendelea kutoa elimu kwa hii jamii yenye mtazamo huo ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo utaikuta ikiwa na cases nyingi za Gender Based Violence.
Acha uchawa basi mkuu,mwanamke hakuumbwa kuja kumuongoza mwanaume katika ngazi yoyote Ile
 
Hizi ndiyo akili mbovu za wanawake 😁😁😁 kwa hiyo kwa hoja hii na fafan7zi uliyo toa , unatuambia kuwa duniani hakuna mwanamke asiye faa kwenye uongozi maana wote wanaweza kuzaa na kulea watoto wao ....nimegundua nazungumza na mtu mwenye akili finyu sana ....sasa nataka kukuelim8sha AKILI YA UONGOZI NDIYO AKILI HADIMU SANA HATA KWA WANAUME NI WACHACHE TU WALIYO NAYO ILA KWA WANAWAKE HAKUNA ALIYE NA AKILI YA UONGOZI....hoja yako ya kuzaa ni uouuzi kwa sababu kama ni hivyo basi binadamu asilimia 99 wana akili ya uongozi
Hivi unajua unayemjibu lakini?
 
Huyuu namjua vizri tuuu ,ni mbunge mmoja wa Jimbo maarufuu ,huko kwenye mkoa maarufu sana hapa Tz.

Nikiconnect doti kadhaa kadhaaa ,sasa ivi hana ndoa nazani hata majina yake yapo tofauti na alipoanza ubunge ,nampa pole ndugu yangu.
Code Rahisi sana...huyu Demu inaelekea ubunge wenyewe aliupata kwa kuvuliwa Pichu
 
Natumaini wewe ni mkristo na unafaham tangu ngazi ya familia mwanaume ndiyo kichwa au kiongozi,hata lile lililokuwa taifa teule zamani hawakuwai kuwa na mkuu wa nchi mwanamke,haya ya leo ni kukengeuka tu Kwa binadam,ila kama ambavyo binadam hana uwezo wa kupaa angani ndivyo mwanamke pia hana uwezo wa kuongoza
Hilo la uongozi kwenye taasis ya familia kila siku nalisema hivyo hivyo kama wewe ulivyosema na naliishi kwamba, kwenye familia niliko, mkuu wa familia na msemaji wa mwisho ni mume wangu. Ila pamoja na hayo, bado kuna majukumu ya mama ambayo nayafanya na walio chini yangu kwenye eneo la jukumu hilo wanajua mimi ni kiongozi na lisipofanyika vizuri jukumu hilo, mkuu wa kaya ataniona mimi mzembe.

Sasa tutofautishe uongozi wa kwenye taasis ya familia na wa kwenye taasisi za umma ambako, ni vitu 2 tofauti na mahitaji ya kujaza nafasi za uongozi wa taasis ambazo siyo za kifamilia ni mengine kabisaaa.

Habari za asubuhi jamani, maana kasalamu nako muhimu kwenye uongozi😅
 
Daktari asikuumize kichwa huyo mwananchi. Inawezekana anatokea Kwenye zile jamii ambazo hadi sasa haziamini katika usawa wa kijinsia na fursa sawa. Bado wanadhani dunia inazunguka katika muktadha wa vijiji vyao.
Kama wizara nadhani mna kazi kubwa sana ya kuendelea kutoa elimu kwa hii jamii yenye mtazamo huo ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo utaikuta ikiwa na cases nyingi za Gender Based Violence.
Mkuu huwezi kujizuia kidoogo ukaficha Munkari wa uchawa? Nakumbuka tabia yako Primary uliwahi kumkumbusha mwalimu kuwa kasahau kutoa adhabu kwa wale waliopata marks chini ya 50 somo lake.
 
Daktari asikuumize kichwa huyo mwananchi. Inawezekana anatokea Kwenye zile jamii ambazo hadi sasa haziamini katika usawa wa kijinsia na fursa sawa. Bado wanadhani dunia inazunguka katika muktadha wa vijiji vyao.
Kama wizara nadhani mna kazi kubwa sana ya kuendelea kutoa elimu kwa hii jamii yenye mtazamo huo ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo utaikuta ikiwa na cases nyingi za Gender Based Violence.
Umenena vema kabisa, kuna watu wengine wanadhani, maisha ya huko waliko ndiyo mwongozo wa dunia yote.
 
Inafanana na story ya uncle wangu na mkewe,😭 uncle alitishiwa na mkewe aliepata Ubunge kwa kuteuliwa na Rais.Ikabidi awe mpole...aliishi maisha ya upweke mno😭.Maana mkewe baada ya kupata Ubunge akaingizwa kwenye hizo kamati,akuna rangi ambayo uncle akuiona Toka kwa mkewe.Mungu amtie nguvu huyu mwenye story katika Uzi huu🙏
Mkuu mtu yoyote akipata pesa nyingi nyingi lazima atabadilika tu, ata wewe sasa hivi kama ulikua unaingiza laki 9 kwamwezi na ghafra ukapata Uteuzi wa Ubunge na ukaanza kupokea posho nyingi na safari za kwenda Ulaya lazima utabadiliia tu.
 
Hilo la uongozi kwenye taasis ya familia kila siku nalisema hivyo hivyo kama wewe ulivyosema na naliishi kwamba, kwenye familia niliko, mkuu wa familia na msemaji wa mwisho ni mume wangu. Ila pamoja na hayo, bado kuna majukumu ya mama ambayo nayafanya na walio chini yangu kwenye eneo la jukumu hilo wanajua mimi ni kiongozi na lisipofanyika vizuri jukumu hilo, mkuu wa kaya ataniona mimi mzembe.

Sasa tutofautishe uongozi wa kwenye taasis ya familia na wa kwenye taasisi za umma ambako, ni vitu 2 tofauti na mahitaji ya kujaza nafasi za uongozi wa taasis ambazo siyo za kifamilia ni mengine kabisaaa.

Habari za asubuhi jamani, maana kasalamu nako muhimu kwenye uongozi😅
Hongera Dkt, umepambana bila kuchoka toka usiku ushuke kwenye SGR mpaka sasa, and you look and comment very positive, anyway congratulations Madam Honourable
 
Kuna mbunge mmoja anabonge shape/zigo sijui kama wazee wamjengoni wamemkosa. Ila sio bungeni hata makazini, huku wengine wanagongwa kupitia vyeo, wengine kupitia safari bosi anamwambia husiponipa husafiri nk na huko safarini tena,mazoea mazoea mfanyakazi mwenzake nae anamgonga.Wapo wenye misimamo ila wachache sana.
 
Pole sana dada E Matikoooo kwa hayo yaliyokukuta. Wahenga waliasa kuwa tamaa mbele mauti nyuma. Ndiyo maana wakati mwingine uheshimiwa ni uishiwa hasa unapokuwa wa watu wasio na kumbukumbu wala huruma. Huna haja ya kulalamika wala kusikitika. Umevuna ulichopanda.
Hapana familia ya E Matik naijua vizuri sana. Iko stable. Hana madeni. Kifupi hakuna changamoto zozote anazopitia ktk familia yake, kama zipo ni zile za kawaida kila mtu hupitia.
 
Back
Top Bottom