Kwa haya uliyoandika na nilivyoyasoma nakumbuka maneno niliyowahi kuelezwa na wakubwa wangu kuwa "Mpumbavu akinyamaza huwezi kujua upumbavu wake" sasa kwa kuzungumza kwako tu nimekujua kuwa wewe ni Mpumbavu. Dr. Slaa si msaliti kwa CHADEMA Bali msaliti wenu Chadema ni mwenyekiti wenu Freeman Mbowe kwa akili ndogo aliyokuwa NATO na tamaa binafsi ameona ni heri amtupe Dr. Slaa na kumkumbatia fisadi maarufu hapa Tanzania ambaye hata wenzake wa chama chake ambao kafanya nao Kazi miaka mingi wanamjua kuwa ni fisadi na mwizi aliyekubuhu na wakamtimua katika uongozi.
Kwa MTU mwenye akili timamu asingefanya jambo la hatari kama hili alilolifanya mwenyekiti wenu Mbowe. Hivi amemuamini nini Edward Lowassa mpaka kumpa nafasi ya kuwa mgombea wenu wa uraisi. Lowassa hana usafi wowote na doa lake halikuanzia katika kashfa ya Richmond tu bali hata baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere alishamjua siku nyingi na aliusema ufisadi wake waziwazi na hakumficha kipindi kile cha mwaka 1995. Je Mbowe hajui hilo? Kwa maneno yake machache tu ya uongo kuwa eti muhusika mkuu wa Richmond alikuwa in raisi Kikwete basis nanyi kwa akili zenu ndogo mumeridhika bila ya kufanya utafiti wowote na munakaa majukwaani na kuanza kuutangazia umma kuwa Lowassa in msafi sana ila mfumo ndiyo mchafu wakati mumesahau huyo mfumo mchafu no wa Lowassa na marafiki zake Andrew Change, Rostam Aziz, Karamagi wengineo.
Dr. Wilboad Slaa no MTU mkweli na mwenye heshima yake katika jamii ya kitanzania na nje ya Tanzania na alishamtaja huyu huyu Lowassa katika ile list of shame ya mafisadi papa wa Tanzania na bafo anayaamini maneno yake ni sahihi. No hero aonekane ni msaliti kwa CHADEMA na UKAWA kuliko kuwa msaliti kwa taifa kwa kumpigia kampeni na kumsafisha Mwizi ambaye akishika ikulu tu ataleta ufisadi mkubwa nchini.
Namshangaa na namdharau kabisa huyu Process njaa Kali wa CUF Prof. Lipumba kwa elimu yake na usomi wake ameshindwa kujua kwamba Lowassa si MTU sahihi kwao ila ni mtego tu hafai kuwa mgombea wao. Lakini cha kushangaza yeye amekuwa mstari wa mbele kumsafisha na kumpigia debe in aibu sana kwake na kwa uprofesa wake.