Naota ndoto kila siku nipo na mdogo wangu aliyefariki

Naota ndoto kila siku nipo na mdogo wangu aliyefariki

Kifo chake ni vile vifo vinaitwa pre mature deaths,yaani kifo kabla ya wakati,mara nyingi watu wa namna hyo huwa hawaendi mahali pa nafsi za kupumzikia bali huwa wanakuepo tu maeneo yetu mpaka pale Watapoitwa na Mungu kwa wakati wake sahihi...Kauli yake wa mwisho ndiyo ina utata,labda alisema kwa utani tu ila ina maana kubwa.Ni wazi kuwa bado yupo na wewe kiroho na anajiskia vzr kuwa na wewe,japo si kawaida na si kwa namna ya kibinadamu.Inauma ila anatakiwa aende tu coz yeye ni mfu na wewe ni hai,hamuwezi kuwa pamoja,ingawa itamuuma sana.
Shukran mkuu inabid nkubar siponae Tena azid kupumzika kwa aman
 
[emoji31][emoji31][emoji31] huyo ndio mlinzi wako na furahia unavyo muona kwenye ndoto iko siku atakufunia mambo mazito !
Ubarikiwe na pole sana!
 
Wakuu naomba ushauri wenu Mimi ni mtoto wa pili Kati ya familia ya watoto watano Nina miaka 29 miaka mitatu nyuma nilipata msiba wa mdog angu tuliyefuatana ambaye mpaka kifo chake kinatokea alikuwa Yuko kidato Cha nne kifo chake kilitokea ghalfa tu

Shida yangu Kila siku naota ndoto Niko pamoja nae kweny mazingira mapya tukiongea au tunaenda sehemu Fulani au tupo mazingira Fulani nakosa amani kabisa

Note siku anaaga dunia akiwa mikononi mwangu aliniambia Kaka naenda Ila nitakuwa nawe siku zote😭😣
Omba sana ,kemea hiyo hali.Kataa roho ya mauti.Hii ndoto inaonyesha na wewe utakufa ukaungane na mdogo wako .Yes kufa kupo ila at 29 ni mdogo sana.Unajua kuna watu wanakufa kabla ya nyakati zao.
Kumbuka habari ya Ayubu,Mungu alimwambia sheitwani afanye yote ila asiguse uhai wa Ayubu,that means hata Shetani anaweza ondoa uhai wa mtu.
 
Kama ni muislam zidisha toba hasa swala za usiku.
 
Mimi baba yangu mzazi amefariki kama miaka miwili imepita na huwa namuotaga sana na mara nyingi ananifundisha vitu vya kufanya.
Malaika wetu ndio hao, wana kuja kwa sura ambayo umeizoea usije kupanic!
Stay well brother!
 
Nilimpenda Sana blood brother Kuna muda nikimkumbuka moyo unauma 3 years now lkn naona Kama nmemzika juzi tu
Mkuu Dunia ngumu sana, me na sister angu huyo mwaka wa saba huu umeisha ila mpaka kesho inaniuma sana nikimkumbuka.
 
Ndugu na wazazi wetu waliotutoka huwa Tupo nao pamoja ndani ya nyumba zetu kila siku, wanatuona ispokuwa hatuwaoni!
 
Ni wazi kuwa bado yupo na wewe kiroho na anajiskia vzr kuwa na wewe,japo si kawaida na si kwa namna ya kibinadamu.Inauma ila anatakiwa aende tu coz yeye ni mfu na wewe ni hai,hamuwezi kuwa pamoja,ingawa itamuuma sana.
Kuna rafiki yangu alifariki kifo kilicholeta shaka sana, maana aliugua ghafla kichwa mwezi Disemba 2020 na akawa anapoteza akili. Hospitali walisema ana ufa katika fuvu la kichwa ndio linalosababisha maumivu makali ya kichwa anayosikia.

Baadae familia ikaona ijaribu kumtibu kimila, likapangwa kufanyika tambiko, jamaa akafariki siku 1 kabla ya tambiko. Tukamzika kijijini kwao Januari 2021. Ilisemekana kuwa kabla ya kuugua, aliwahi kufuatwa na jamaa mmoja akamwambia kuwa anamuomba aachane na demu wake (hatujui kama alikuwa ni mke au mpenzi) ila jamaa yangu akamjibu kifedhuli kuwa mwombaji aongee na demu wake ili demu ndio amuache jamaa yetu.

Baada ya kumzika nikaanza kumuota huyu jamaa yangu marehemu, anakuja ndotoni akiwa ni msafi sana kama ilivyokuwa kawaida yake ila hazungumzi kitu. Siku ya kwanza alikuja kwenye chumba nikicholala akanifunua shuka na kuangalia usoni, kisha akafyonya na kuondoka.

Baadae nilimshirikisha mama yangu mzazi akaniambia kuwa hatushirikiani na wafu, akija tena nimkemee, kweli siku chache nikaota ndoto amekuja tena na nguo mpya safi na nikampa neno hilo kuwa yeye ni mfu sio mwenzetu, hatuchangamani nae, atoke. Aliniangalia kwa huruma sana, akatoka na kutokomea gizani, sikuwahi kumuota tena.
 
Wakuu naomba ushauri wenu Mimi ni mtoto wa pili Kati ya familia ya watoto watano Nina miaka 29 miaka mitatu nyuma nilipata msiba wa mdog angu tuliyefuatana ambaye mpaka kifo chake kinatokea alikuwa Yuko kidato Cha nne kifo chake kilitokea ghalfa tu

Shida yangu Kila siku naota ndoto Niko pamoja nae kweny mazingira mapya tukiongea au tunaenda sehemu Fulani au tupo mazingira Fulani nakosa amani kabisa

Note siku anaaga dunia akiwa mikononi mwangu aliniambia Kaka naenda Ila nitakuwa nawe siku zote😭😣
Pole sana mkuu, ni imani tu wazungu wanaita sensational life after death.
Ni kwamba wale uwapendao waliokufa utakua nao tu always.
Sio hata jambo la kusumbua akili.
Chukulia maanani tu mnaonana mnaweza kula na kuongea pamoja bila shida.
Ndio mizimu hiyo.
Kuna ndoto za ajabu na wafu wangu nikisimulia hapa kila kitu kitasimama.
Nshazikwa zaidi ya mara 3 najiona.
Ila unaamka ni ndoto
 
Wakuu naomba ushauri wenu Mimi ni mtoto wa pili Kati ya familia ya watoto watano Nina miaka 29 miaka mitatu nyuma nilipata msiba wa mdog angu tuliyefuatana ambaye mpaka kifo chake kinatokea alikuwa Yuko kidato Cha nne kifo chake kilitokea ghalfa tu

Shida yangu Kila siku naota ndoto Niko pamoja nae kweny mazingira mapya tukiongea au tunaenda sehemu Fulani au tupo mazingira Fulani nakosa amani kabisa

Note siku anaaga dunia akiwa mikononi mwangu aliniambia Kaka naenda Ila nitakuwa nawe siku zote😭😣

Inawezekana hajafa kifo Cha kawaida amefichwa. Mimi nimewahi kuexperience Jambo alikufa mtu baada ya kufa nikaomba nikashangaa kuona kwenye ndoto wakati wanamzika kwenye jeneza kulikuwa Hakuna mwili.
 
Nilitaka kumuita Mshana Jr kumbe tayari ashafika hapo juu.

Sema kuna jujuu kali sana bado anatumikia mahali mkuu amefungwa kisukule lakini akifariki hatokujia ndotoni tena. Bado yupo around.
 
Wakuu naomba ushauri wenu Mimi ni mtoto wa pili Kati ya familia ya watoto watano Nina miaka 29 miaka mitatu nyuma nilipata msiba wa mdog angu tuliyefuatana ambaye mpaka kifo chake kinatokea alikuwa Yuko kidato Cha nne kifo chake kilitokea ghalfa tu

Shida yangu Kila siku naota ndoto Niko pamoja nae kweny mazingira mapya tukiongea au tunaenda sehemu Fulani au tupo mazingira Fulani nakosa amani kabisa

Note siku anaaga dunia akiwa mikononi mwangu aliniambia Kaka naenda Ila nitakuwa nawe siku zote😭😣
Sometimes ndoto ni kumbukizi ya matukio yaliyopita. Don't take it too serious
 
Nilimpenda Sana blood brother Kuna muda nikimkumbuka moyo unauma 3 years now lkn naona Kama nmemzika juzi tu
Kama unaimani katika Kristo Yesu na nguvu zake. Mwite kwa jina lake huyo ndugu na kumwamuru apumzike pema katika Jina la Yesu. Pia kemea pepo wanaoweza kujifanya ndugu yako wakome kufanya hivyo kuanzia sasa.
 
Back
Top Bottom