Napagawa na Bati: ALAF, ANDO, DRAGON - uchaguzi mgumu. Watu wa mauzo saundi kibao!

Uongo
 
huko maktaba kuu mnapeleka OG tukija sisi mnatupa feki
 
Ngoja niwape Siri sasa hapa kuhusu bati.

Kwanza kabisa kitu ambacho unatakiwa ujue bati zote iwe ya rangi au plain material iliyotumika kutengeneza ni ile ile. Tofauti ni kwamba bati za rangi zinaenda hatua moja mbele kupakwa rangi.

Amini usiamini malengo ya rangi kwenye.bati ni kuzuia kutu na si vinginevyo. Bahati mbaya sana Sisi tunachukulia kama fashion na sifa..Kwa mantiki hiyo wale wako nje ya ukanda wa pwani ambako Hakuna humidity yenye unyevunyevu wa maji ya chumvi bati la kawaida linatosha kabisa na utapunguza gharama.

Bati za rangi zimekuja kama mbadala wa vigae amabavyo bei yale iko juu sana Makapuku hatuiwezi. Madoni bado wanaezekea vigae..hata leo hii ukifika osterbay..masaki etc huwezi kuta bati zetu hizi za rangí ni chache sana Bado wenye pesa wanatumia vigae.kujenga Nyumba zenye mvuto na kupambana na kutu.

Ubora wa Bati unategemea na quality control ya kiwanda husika..unaweza kuwa na bati.ya kampuni moja lakini kukawa na matokea tofauti huenda pengine uchakachuaji ulitokea wakati wa uzalishaji Kwa siku husika Kwa hiyo tusiwe general kwamba kampuni fulani ndo the best hapana Tanzania qualify control is very poor.

ALAF.wana mabati ya rangí aina mbili wanayotoa south na mengine Kenya na sasa wameanza kuzalisha wenyewe hapa Dar . Iko hivi Bati kutoka south Africa ndiyo imara.zaidi kiuliko Yate . Quality control South Africa wako smart sana zaidi ya Kenya na Tanzania mteja ni ngumu sana kutofautisha hilo ila kiwandani wanajua.

Bati za south africa hata bei imechangamka sana ndo hizo zinauzwa 27000/ per one metre..Kwa hiyó bati ya uhakika kutoka ALAF upate ya south Africa gauge 28 Hapo ni mkataba ndo maana wengi wakaziita msouth japo Kwa sasa bati zinatoka maeneo mbalimbali. Kuhusu ubora wa Bati kampuni zingine sijui ila ukweli ni majuto tu maana wanatengeza Kwa quality ya Chini ili Kila mtu amudu bei. Bati za quality nzuri kama za south Africa watanzania wachache sana wanaweza kununua.

Ushauri.
Kama mfuko unaruhusu chukua ALAF za south africa..Zina majina Yake kama VERSATILE..ROMATILE. TEKDEK hutajuta kwingine ni kubeti tu na utakuja kuichukia Nyumba Yako..

Herí bati nyeupe kuliko ya rangí inayopauka.
 

Attachments

  • IMG-20221002-WA0004(1).jpg
    34.2 KB · Views: 10
  • IMG-20221002-WA0007.jpg
    42.7 KB · Views: 7
  • IMG-20221002-WA0006.jpg
    41.7 KB · Views: 6
  • IMG-20221002-WA0004.jpg
    34.2 KB · Views: 11
Mariana na Ando mkuu binafsi sijutii
 

Attachments

  • IMG_9572.JPG
    749.1 KB · Views: 9
Bati bora za wakati wote ni kutoka ALUMINIUM AFRICA au ALAF
 
naomb kujua tofaut ,ya tekdek,maxcor,na covermax? na bei zao ,pia shiling ngap kwa mita varsntal,na romantic
 
naomb kujua tofaut ,ya tekdek,maxcor,na covermax? na bei zao ,pia shiling ngap kwa mita varsntal,na romantic
Bei hazina tofauti kubwa Kwa wastani ni 27000/Metre. Tofauti Yake ni migongo tu(Profiles) kama kwenye picha hapo juu.
 
Bei hazina tofauti kubwa Kwa wastani ni 27000/Metre. Tofauti Yake ni migongo tu(Profiles) kama kwenye picha hapo juu.
Na royal varsantile ,varsantile royal romatil ,na romatil mit mnauzaj hapo ALAF? Yana sentimit ngapi upana?[emoji120]
 
Fundi wangu aliniambia kama siyo ALAF ni heri nipaulie nyeupe tu nije nipake rangi.

Nikapiga ALAF,ukiyatizama mapaa ya majirani tuliopaua mwaka mmoja au baada yangu hali ni tete.

Wanapaka rangi kwa sasa huku Mimi nikipeta tu.
 
Chukua kampuni yoyote yasiyo na rangi mradi gauge iwe ile unayotaka.
Rangi utapaka baada ya 5- 10 yrs . Kinachotofautisha bati ni rangi tu na zote hupauka
ALAF hauzi rangi😁😃,anauza bati kulingana na materials,yasiyo na rangi,yaliyo na rangi,corrugate style,versatile yote bei moja
 
Fundi wangu aliniambia kama siyo ALAF ni heri nipaulie nyeupe tu nije nipake rangi.

Nikapige ALAF,ukiyatizama mapaa ya majirani tuliopaua mwaka mmoja au baada yangu hali ni tete.

Wanapaka rangi kwa sasa huku Mimi nikipeta tu.
Na uhakika hawajanunua kiwandani,mawakala hua wanachanganya makusudi..........ALAF nenda kiwandani kaweke oda uchukue mzigo wewe mwenyewe
 
Kuna bati za alaf damu ya mzee dah zina muhuri na kila nembo ya alaf lakin zimepauka hat mwaka haujaisha..sijui ni nini
Hizo nauhakika ni feki.
Bati za ALAF nenda mwenyewe kiwandani kuazinunue,kisha zisafirishe mkuu
 
Kuna bati za alaf damu ya mzee dah zina muhuri na kila nembo ya alaf lakin zimepauka hat mwaka haujaisha..sijui ni nini
Hizo nauhakika ni feki.
Bati za ALAF nenda mwenyewe kiwandani kazinunue,kisha zisafirishe mkuu
 
ALAF nimewacheki bei Yao imesimama hatari. Hivi hakuna kampuni nyingine inayozalisha mabati Bora Kwa bei ya kitanzania zaidi ya hao ALAF ?
Hapo ndio masikini tunapofeli sasa.......unataka daktari bingwa bobezi bora huku bajeti Yako ya zahanati ya serikali,......mgonjwa akifa unaanza kumlaumu huyo daktari bingwa Bora ambaye hata hayupo kwneye hiko kituo😃😄😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…