#COVID19 Napambana na COVID-19 deadly Delta

#COVID19 Napambana na COVID-19 deadly Delta

Nikiwambia watu hawaelewi wanadhani masikhara! Tatizo sio wapumbavu kufa tatizo wanasambaza na kuua wasio na hatia...
people are dying brother!

watasema watu mbona wanakufa kila siku but sasa hivi ni too much!

tembelea barabara ya arusha-dar uone vimuli muli vinavyopita..sio kawaida.

unahesabu misafara karibu 50 zinapeleka msiba halafu mtu akwambie eti hamna korona.
 
Pole sana mkuu Isa, get quick recovery 🙏 na je umeshapima kuconfirm its wave 3? Ama unajitibia kadri unavoona hizo dalili?🤔
Sijapata confirm maana daktari alinambia ni wimbi la mafua na kunipatia dawa za flu na kikohozi. | Najitibia kwa kufuata kanuni mbalimbali toka vyanzo mbalimbali.
 
zamani kufiwa ilikuwa unakaa hata miaka 5 anaondoka member 1paap!!mnatulia tena ht miaka7 ndo afatie mwingine!!

ndani ya mwezi unafiwa na members 2 halafu walikuwa wazima wa afya!bado roho iko juu juu mwezi unafuatia wengine 2 paap!

hapo mwingine akiumwa kwa mtindo ule ni mashaka yaani unakuwa moyo unakulipuka kila mda huna raha.
Nakuelewa mkuu! Inauma mno huwa nafikiria maisha yamekua mafupi sana lolote linatokea muda wowote😪 Mungu atusaidie waja wake
 
Nilifikiri umekufa kumbe bado unapambana tu! Kelele nyingiiii kumbe hata kupima hujapima!!

Wewe umeshatia timu.

Bila shaka wale wanaoona anapigania mikopo na misaada ya imf, watakuwa bado wanamvutia kasi.
 
Sasa we jamaa sijakuelewa,kwa kuumwa huko ndo umesha jipima kwamba una ka Covid-19?

Sioni maelezo ya kupimwa kwako na kutuaminisha kwamba uliugua huo ugonjwa, hivi wa Tanzania mna nini?
 
Awamu ya pili nilikumbana na huu ugonjwa, kiukweli ugonjwa huu unatesa sana mgonjwa, ni gharama hata kama una hela, kwa asie na hela hali yake ni ngumu sana....
Toka juzi hadi muda huu nimekwisha tumia TZS 150k+ madawa mbalimbali na vyakula hivi vya kusaidia kupambana. Naamini nitapona mapema kabla hali yangu ndogo ya uchumi kusumbua.
 
Wewe umeshatia timu.

Bila shaka wale wanaoona anapigania mikopo na misaada ya imf, watakuwa bado wanamvutia kasi.
Vipi Mama yako anaendeleaje na Covid 19 si ulisema wiki iliyopita kuwa amepatwa na Covid 19?
 
daahh rangi ya bluu ni kwamba oxgen level ilikuwa chini sana.
huu ugonjwa toka mwaka umeanza umeshaondoka na 4 family members akiwemo mamaangu!!
na hapa sshv naongea mwingine amelazwa na ventilator juu...
acheni maskhara kbs.
Wave two iliondoka na mzee wangu
 
Toka juzi hadi muda huu nimekwisha tumia TZS 150k+ madawa mbalimbali na vyakula hivi vya kusaidia kupambana. Naamini nitapona mapema kabla hali yangu ndogo ya uchumi kusumbua.
Piga nyungu. Covid haina dawa
 
kwani haijawafikia tayari?? mbona viongozi kina Kijazi waliondoka nayo?? basi tu hatuna waziri wa afya makini..alikua anahimiza nyungu..sasa hivi Rais yuko makini ndio kaanza kuhuburi watu wachukue tahadhari...matokeo yake watu wanapuuza guidelines...chanjo inaonekana kama sijui duddu gani
Kupambana na COVID-19 hutakiwi kucheka na watu wapumbavu, unaweka strictly rules na ni lazima kufuatwa ndio tutaweza kuondosha.
 
Sasa mbinu zilizofeli uzichukue upeleke wapi? We mama na wewe unazeeka vibaya 😂😂😂😂
mnhhhh....ngoja upatwe na nduguyo mgonjwa ndio utatia akili, hujaangalia nchi zilizou contain ugonjwa kwa kufuata guidelines,umechoose kuwa biased kuangalia only zilizofeli...pole we! hao Italia pamoja na kufeli kwao je wameacha kuvaa barakoa??..
 
Back
Top Bottom