#COVID19 Napambana na COVID-19 deadly Delta

#COVID19 Napambana na COVID-19 deadly Delta

Toka juzi hadi muda huu nimekwisha tumia TZS 150k+ madawa mbalimbali na vyakula hivi vya kusaidia kupambana. Naamini nitapona mapema kabla hali yangu ndogo ya uchumi kusumbua.
hiyo pesa ndogo sana.
Kuna bilionea mmoja alikufa kwa kukosa ventilator na alikuwa tayari kuilipia kwa kuikodi au kuinunua kwa gharama yoyote.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Peleka ujinga wako ulipo utoa kwa hiyo kwa kuvaa barakoa unajiona umefuzu kuwakebehi wengine? Unadhani Italy walishindwa kununua barakoa au kunawa na maji tiririka?
Sio lazima kukubali au kuchukua kila shauri, ikiona na kuamini hakuna UVIKO we endelea na mikutano, mikusanyiko, kutokuchukua tahadhari na shughuli zako ulivyopanga.
 
mnhhhh....ngoja upatwe na nduguyo mgonjwa ndio utatia akili, hujaangalia nchi zilizou contain ugonjwa kwa kufuata guidelines,umechoose kuwa biased kuangalia only zilizofeli...pole we! hao Italia pamoja na kufeli kwao je wameacha kuvaa barakoa??..
Nahisi nakuonea maana maelezo yako yamedhihirisha kiwango cha maarifa yako. Na kwa kuwa umechagua kupokea taarifa bila kuzifanyia utafiti hivyo nikushauri tu, wewe endelea kuvaa barakoa kama njia ya kijikinga na virus maana ndicho ulichokariri.
 
Nahisi nakuonea maana maelezo yako yamedhihirisha kiwango cha maarifa yako. Na kwa kuwa umechagua kupokea taarifa bila kuzifanyia utafiti hivyo nikushauri tu, wewe endelea kuvaa barakoa kama njia ya kijikinga na virus maana ndicho ulichokariri.

Achana na kiwango changu cha maarifa, weka hapa hizo tafiti za kutokuvaa barakoa na maambukizi (kama unazo, i bet huna)
 
Pole sana mkuu and thanks for sharing , corona itaendelea kuenea sababu moja wapo ndiyo hiyo uliyoitaja kuna baadhi ya watu ni "Empy set" yaani wapo wapo tu hawajui kitu kinachoitwa tahadhari nadhani mwendazake aliwa_brainwash sana.
Hakika! Watu hawaelewi kabisa ukisema neno Corona au UVIKO, ukivaa barakoa au kunawa mikono unaangaliwa mita 100.
 
Peleka ujinga wako ulipo utoa kwa hiyo kwa kuvaa barakoa unajiona umefuzu kuwakebehi wengine? Unadhani Italy walishindwa kununua barakoa au kunawa na maji tiririka?

Unavaa barakoa kwa usahihi? Watu wanavaa barakoa halafu kutwa kulivua kulishika shika unatarajia hapo anajikinga au anajiambukiza?
 
Habari 👋🏾

Kumekuwa na hali ya watu wengi kupuuza na kutokuchukua tahadhari ya ugonjwa wa UVIKO na wengine wakienda mbali kudai hakuna ugonjwa kama huo. Napenda kuwaambia COVID-19 deadly Delta yupo Tanzania na kila mahali, nimepatwa na ugonjwa ilhali nipo eneo lilotengwa na pembezoni katika nchi...
Huu ndio ukweli, hakuna namna utaweza kujikinga kwa ukamilifu kama jamii yako haifanyi hivyo. Uwezekano wa kupambana na ugonjwa huu ni kwa jamii kwa uwingi wake kujikinga na kufuata masharti sawa. (Refer first phase, ila tusiwe na lockdown, kabla hatujakengeuka na kusema maombi yametuokoa).

Kitu hicho hicho ni kwa chanjo, ukichanja halafu jamii nzima haichanji ni kazi bure kwani Virus watakao kuwa wako mitaani wataongezeka nguvu na chanjo uliyopata haita kuwa na maana kwa variant mpya ya virus.

Pole sana mkuu.
 
Acha maigizo wewe!

Hivi nyie madalali wa chanjo ni lini mtaacha janja janja za kitapeli?

Kwanza haka kahadithi chako hakana ithibati yoyote. Umejitungia tu!

Kama hujatunga THIBITISHA!
 
Wewe nawewe chawa wa mwendazake umeshatia timu. Tunajua kama mlivyo:

1. Corona haipo
2. Hamtaki katiba mpya.

Tunasubiri wale wa mambo ya mikopo na misaada ya IMF. Bila shaka wako njiani.
Wanamambo ya ajabu sana hawa, sasa nidanganye kuwa na COVID-19 kusudi inisaidie nini?!
 
Wewe nawewe chawa wa mwendazake umeshatia timu. Tunajua kama mlivyo:

1. Corona haipo
2. Hamtaki katiba mpya.

Tunasubiri wale wa mambo ya mikopo na misaada ya IMF. Bila shaka wako njiani.
Katiba iliyopo inatosha mkuu sasa hivi tunahangaika na kuimarisha uchumi. Kuhusu Corona tutaishi nayo kwa muda mrefu hata Baba zako WHO wameshasema. Hivyo fanyakazi achana na corona
 
Huu ndio ukweli, hakuna namna utaweza kujikinga kwa ukamilifu kama jamii yako haifanyi hivyo. Uweekano wa kupaambana na ugonjwa huu ni kwa jamii kwa uwingi wake kujikinga na kufuata masharti sawa...
Watu hawaelewi hili, wanadai tunalipwa kusambaza propaganda. Fikra zao zimefungwa tayari, kitakacho wakumbusha ni uhalisia.
 
Wanamambo ya ajabu sana hawa, sasa nidanganye kuwa na COVID-19 kusudi inisaidie nini?!

Mkuu achana nao.

Kwa sasa pumzika uugue pole. Ujumbe wako tumeupokea. Kwa hali ilivyo nasi usipotusikia ujue parapanda yaweza kuwa imeshaimbwa pande za kwetu.

Nani yuko salama?
 
people are dying brother!
watasema watu mbona wanakufa kila siku but sasa hivi ni too much!
tembelea barabara ya arusha-dar uone vimuli muli vinavyopita..sio kawaida.
unahesabu misafara karibu 50 zinapeleka msiba halafu mtu akwambie eti hamna korona.
Kwahiyo ulitaka watu wasife? Kwani hii dunia ni ya baba yako?

Vifo vipo miaka nenda rudi, na watu wataendelea kufa kila siku.

Tapeli wa COVID wewe!
 
Back
Top Bottom